Matukio : Rais Dk. Magufuli Aongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki, Jijini Arusha - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


2 Mar 2016

Matukio : Rais Dk. Magufuli Aongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki, Jijini Arusha

Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiweka saini ya Kanuni za Madili ya Mfuko wa Sekta Binafsi wakati wa Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Mashariki jijini Arusha leo Machi 2, 2016
Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda akijiandaa kuweka saini ya Kanuni za Madili ya Mfuko wa Sekta Binafsi wakati wa Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Mashariki jijini Arusha leo Machi 2, 2016
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya akiweka saini ya Kanuni za Madili ya Mfuko wa Sekta Binafsi wakati wa Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Mashariki jijini Arusha leo Machi 2, 2016
Rais Paul Kagama wa Rwanda  akiweka saini ya Kanuni za Madili ya Mfuko wa Sekta Binafsi wakati wa Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Mashariki jijini Arusha leo Machi 2, 2016
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akihutubia katika Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Mashariki jijini Arusha leo Machi 2, 2016
Wanafunzi walioshinda mashindano ya Insha ya EAC wakipata selfie na viongozi baada ya Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Mashariki jijini Arusha leo Machi 2, 2016.
Kijana Simon Sahaya Mollel (18) wa Shule ya Sekondari ya Mzumbe ya mjini Morogoro akionesha dola 1500 alizopewa kama zawadi baaya ya kuibulka mshindi wa kwanza wa kuandika Inshawakati wa Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Mashariki jijini Arusha leo Machi 2, 2016. PICHA NA IKULU.

Na Vero Ignatus - Arusha,
Liberate Mfumukeko Ateuliwa Kuwa Katibu Mkuu Mpya wa Jumuiya Hiyo

Wakuu wa mataifa wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wameikubalia Sudan Kusini kuwa mwanachama wa jumuiya hiyo ya kikanda.

Mkutano wa kilele wa Jumuiya hiyo jijini Arusha leo  Jumatano (Machi 2) umepitisha  pendekezo la baraza la mawaziri juu ya uwanachama wa Sudan Kusini na pia hali ya usalama nchini Burundi.

Kikao hicho kilichodumu kwa muda wa takribani masaa matano kimelikubalia taifa hilo changa kabisa barani Afrika kuwa mwanachama wake wa sita, kuungana na Tanzania, Rwanda, Burundi , Uganda na Kenya.

Rais  Magufuli  ambaye ndiye  mwenyekiti wa kikao hicho, amewaambia wajumbe wa mkutano huo wa kilele kwamba sasa "Sudan ya Kusini ni mwanachama halali wa jumuiya" hiyo.

Mkutano huo pia umezungumzia kwa kina masuala ya maendeleo ndani ya jumuiya ikiwemo mipango ya kujengwa kwa viwanda vya nguo na bidhaa za ngozi ili kuondoa kabisa biashara ya uagizaji wa nguo kuukuu, maarufu kama mitumba, katika nchi hizo katika miaka michachache ijayo

Mkutano huo pia umeshuhudia uzinduzi wa pasi ya kusafiria ya kielektroniki itakayotumiwa katika eneo la Afrika Mashariki pamoja na mwongozo maalum wa kimaaadili katika biashara kwenye nchi wanachama wa jumiya hiyo.

Akizungumzia kuhusu maendeleo ya jumuiya hiyo, Katibu Mkuu anayemaliza muda wake, Dk. Richard Sezibera, amesema kuwa jumiya hiyo inasonga mbele kwani itifaki mbalimbali zimepitishwa kuanzia ushirikiano katika soko la pamoja, ushuru wa forodha na sasa wanaelekea kufikia hatua ya Afrika Mashariki kuwa na sarafu moja itakayotumika katika nchi zote wanachama.

Amesema kuwa tayari jitihada zinaendelea katika kuondoa vikwazo mbalimbali katika sekta za mawasiliano, biashara na usafiri "ili kuwapa wananchi wa Afrika Mashariki fursa ya kuufurahia na kufaidi muungano" huo.

Katika mkutano huo, Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi hakuhudhuria na badala yake alimtuma makamu wake wa pili, Joseph Butore, huku serikali ya Sudan Kusini ikiwakilishwa pia na makamu wa pili wa rais, James Waniiga.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad