Matukio : Dk. Liberate Mfumukeko ateuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


3 Mar 2016

Matukio : Dk. Liberate Mfumukeko ateuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Jumatano Machi 2, 2016 kwa kauli moja umemteua Dkt Libérat Mfumukeko (pichani) kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo. 

 Dkt Mfumukeko, ambaye anayetarajiwa kuanza kazi rasmi mwezi ujao, kuchukua nafasi ya Dkt. Richard Sezibera aliyemaliza muda wake baada ya kufanya kazi tokea April 2011, awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, akishughulikia fedha na utawala, nafasi aliyoteuliwa mwaka jana. 
 Kabla ya kujiunga na EAC, Dkt. Mfumukeko alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nishati na Madini la Burundi (REGIDESO) na pia alikuwa mwenyekiti wa Kamati Endeshaji ya Nishati ya Afrika Mashariki - East African Power Pool (EAPP). 
 Mkutano huo, ukiendeshwa chini ya Mwenyekiti wake Rais Dkt John Pombe Joseph Mgufuli, pia uliridhia nchi ya Sudani ya Kusini kuingizwa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, kungana na Rwanda, Uganda, Kenya, Burundi na Tanzania.

Post Top Ad