Meneja
Mawasiliano wa TPA, Bibi Janeth Ruzangi (kulia) akikabidhi vitanda 20,
magorodo 20 na mashuka 100, vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni
13 kwa hospitali ya Wilaya ya Kisarawe mwishoni mwa wiki. Anayekabidhiwa
vifaa hivyo ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Bwana
Hamis Likupotile (kushoto) na Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dkt
Elizabeth Oming'o. Makabidhiano hayo yaliyafanyika hospitali hapo.
Meneja
Mawasiliano wa TPA, Bibi Janeth Ruzangi (kulia) akikabidhi vitanda 20,
magorodo 20 na mashuka 100, vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni
13 kwa hospitali ya Wilaya ya Kisarawe mwishoni mwa wiki. Anayekabidhiwa
vifaa hivyo ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Bwana
Hamis Likupotile (kushoto) na Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dkt
Elizabeth Oming'o. Makabidhiano hayo yaliyafanyika hospitali hapo.
Mamlaka
ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imetoa msaada wa Vitanda 20,
Magodoro 20 na Shuka 100 kwa Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe Mkoani
Pwani.
Vitanda
hivyo vya kisasa aina ya ‘Cardiac’, mashuka pamoja na magodoro yake
vilivyokabidhiwa katika hospitali hiyo ya wilaya vina thamani ya
shilingi za kitanzania milioni 13.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Meneja Mawasiliano wa TPA, Bibi Janeth
Ruzangi alisema msaada huo ni sehemu ya wajibu wa Mamlaka kuisaidia
jamii ya Watanzania.
“Pamoja
na shughuli zake za kupakua na kupakia mizigo, Mamlaka pia ina wajibu
wa kurudisha kile inachokipata kutokana na huduma zake kwa kuisaidia
jamii na ndio maana leo hii tumekuja kutekeleza wajibu huo,” alisema
Ruzangi.
Bibi
Ruzangi alisema pamoja na kwamba msaada huo ni mdogo lakini wana imani
utasaidia kupunguza changamoto za uhaba wa vitanda katika hospitali hiyo
ya wilaya. Kwa mujibu wa Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dkt Elizabeth
Oming’o hospitali hiyo ina uhaba wa vitanda 94 na mashuka 1,200.
“Hiki
kilicholetwa na Mamlaka ya Bandari ni zaidi ya msaada kwani vitanda hivi
ni vya kisasa na ni vya gharama sana,” alisema Dkt Oming’o.
Dkt
Oming’o alisema kwamba wanashukuru sababu msaada huo utaenda kupunguza
pengo la uhaba wa vitanda na mashuka walilonalo hospitalini hapo.
Alisema kwamba mbali ya vitanda na mashuka hayo, pia wana changamoto ya
vitanda vya upasuaji. Vilivyopo sasa katika hospitali hiyo vimechakaa na
hivyo havikidhi mahitaji yao.
Akizungumzia
vitanda walivyokabidhiwa na TPA, Dkt Oming’o alisema ‘Cardiac bed’ ni
vitanda vya kisasa kabisa ambavyo hospitali hiyo ilikuwa haina.
“Vitanda hivi ni gharama sana kiasi kwamba kama tungeamua kwenda kuvinunua kwa pesa yetu, hakika tusingeweza,” alisema.
Alisema wamefarijika na ujio wa vitanda hivyo kwani vitarahisisha kazi zao kwa kiasi kikubwa.
Naye
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Bw. Hamis Likupotile alisema
wanaishukuru Mamlaka kwa msaada huo kwani hospitali yao ina upungufu
mkubwa wa vitanda.
Vitanda
hivi 20 na magodoro yake pamoja na mashuka ni msaada mkubwa kwetu kwani
umesaidia kutatua tatizo sugu la uhaba wa vitanda katika hospitali
hiyo. Alisema kwamba changamoto walizo nazo ni nyingi na walishapeleka
maombi sehemu mbalimbali ili wasaidiwe lakini kote bado hawajibiwa.
“Kwa
kweli tunawashukuru sana TPA kwani katika mashirika yote tuliyoomba,
bandari ndio wamekuwa wa kwanza kutujibu na kutusaidia kwa wakati,”
alisema. Hospital hiyo kwa sasa imekuwa chombo muhimu si kwa Kisarawe tu
bali hata kwa wananchi wa mikoa jirani kwani kwasasa wanahudumia watu
wengi sana kutoka Gongo la Mboto, Pugu na Mbagala.
Kwahiyo
alisema msaada huo umesaidia jamii kubwa ya watanzania na si Kisarawe
pekee, hivyo kuiomba Mamlaka iendelee kuwasaidia vifaa tiba vingine,
kwani ujio wa wagonjwa wengi pia huleta changamoto nyingi.
No comments:
Post a Comment