Kumbukumbu : Ni miaka 5 sasa toka Mama Yetu Apumzike. - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


24 Mar 2016

Kumbukumbu : Ni miaka 5 sasa toka Mama Yetu Apumzike.

Ni Miaka 5 ya Uchungu , Huzuni na Masikitiko Kwa Kumpoteza MAMA YETU. Namshukuru Mungu Kwa kumpumzisha Mama YETU. Ulisema, Tumshike Mungu , Tuwe na Upendo Kwa kila MTU , Tutafute Kwa Bidii kuwa na Amani na watu wote ....na kusoma neno la Mungu. Mama tunaendelea kutekeleza yale yote Mazuri Uliyotuachia ; Nilikupenda sana MAMA. Mungu Akakupenda Zaidi. I love you Mama Forever. @danielurioh @neema_pallangyo @upendogadiel

ASANTE MAMA, ASANTE MAMA, ASANTE MAMA.
NI MIAKA MITANO BAADA YA MAMA KUTUTOKA… nimekumbuka neon la Asante ambalo ndilo lilikuwa likinitoka pamoja na maumivu mazito moyoni….
Simu yangu iliita siku ya Jumatano majira ya saa tisa mchana…. Kuiangalia simu ni Mke wangu ananipigia…. Kupokea namsikia anaongea kwa hofu, anasema mama anaumwa … Mama ameniambia niwaite vijana wake wampeleke Hospitali… Haraka nikamjibu chukua tax wampeleke Hospitali ya Dr. Mhando na mimi natoka kazini tukutane huko.
Gafla simu inaita tena ni namba nisiyoifahamu….. nikapokea… halooo … halooo wewe ndio Dani nikajibu ndio mimi, mimi ni dereva tax tupo na mama kwenye gari tunaelekea Mount Meru, …. Nikajibu hapana mama huwa anatibiwa hospitali ya moyo ya Dr Mhando…. Dereva tax ananiambia nisikilize wewe ni mwanaume mama amefariki…..
Sitasahau sauti hiyo …. Nikamwambia nakuja hapo Mount Meru…. Nikatoka darasani nilipokuwa nafundisha nikaelekea kwa mtaaluma na kumuaga nikamweleza Mama yangu amefariki naelekea Mount Meru….
Nilipotoka kufika barabarani nikamwita bodaboda …. Nakamwambia nipeleke Mount Meru … akajibu hapana siendi…. Nikamfuata mwingine aisee nifikishe Mount Meru nae pia akakataa…… ikabidi nipande hiace kuelekea Mount Meru….. nikampigia tena dereva tax aisee nakutumia namba za kaka yangu yupo hapo AICC nikamrushia namba wakaendelea kuwasiliana.
Nilipofika Mount Meru nipokelewa na mke wangu akilia sana, nawaona kaka zangu Ombeni na Goodluck usoni mwao wamejaa huzuni na hofu nitafanyanini, nikaona gari la kaka kuna watu watatu kulisogelea namwona mama amelala kifuani mwa mama mwenye nyumba yangu, pembeni yupo jirani yangu mama Kevi… nikamshika mama Mkono mikono imelegea… neon lililonitoka mdomoni ni Asante Mama, mama mwenyenyumba yangu ananiambia alikuwa amejikaza sana… ulipofika tu amelegea… moyo ukiwa umejaa huzuni ninaendelea kusema Asante Mama.
Tukaelekea Nkoaranga Hospitali…. Tukaingia Mortuary, ndio ilikuwa siku yangu ya kwanza kufika mortuary, kubema maiti na kuingiza mwili kwenye Jokofu la Mortuary. Tulimpeba tukiwa watatu yaani Ombeni, Goodluck na Daniel.
Mwisho ninakushukuru Mungu sana kunipa mama aliyenilea, kunisomesha na kunifikisha hapa nilipo. Ninakumbuka kabla ya kifo aliniahidi siku akiondoka ameomba aondoke kwa amani, tusipate shida, ni kweli siku ya mazishi ilikuwa mara yangu ya kwanza kuhudhuria mazishi bila kulia hadharani, japo uchungu ulikuwa mkubwa, hatahivyo Kaburini nilipewa shada la maua nikiwa na mke wangu nikiliweka kaburini … neno lililonitokea ni ASANTE MAMA.
LEO ni siku ya kukumbuka wewe Mama yangu… ulifanya mambo makuu ma tatu, Umisionari, Ualimu na Uongozi Bora… ni ahadi yangu kwa Mungu na kwako mama kuanzisha Dreams Foundation, kuwezesha wale wote wenye Ndoto za Umissionari, Vipaji na Uongozi Bora… Mungu nisaidie.
ASANTE MAMA, NAKUPENDA MAMA, ASANTE MAMA, NAKUPENDA MAMA.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad