1: KUPUNGUZA UZITO:
Kunywa maji mengi kunasaidia kupunguza uzito, kwani maji hayana mafuta, kalori wala sukari.
2: AFYA YA MOYO:
Unywaji wa maji mengi kunaweza kupunguza hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo. Utafiti wa miaka sita uliofanywa Marekani umeonesha kuwa watu wanaokunywa glasi za maji zisizopungua 5 kwa siku, hujiepusha na uwezekano wa kupatwa na ugonjwa wa moyo kwa asilimia 41 zaidi ya wale wanaokunywa glasi 2 au chini ya hapo.
3: NISHATI YA MWILI:
Mwili unapopungikiwa maji, hukufanya ujisikie mchovu, hivyo kwa kunywa maji ya kutosha daima utakuwa mwenye nguvu. Pendelea kunywa maji badala ya vinywaji baridi kama soda, juisi au bia.
4:TIBA YA KICHWA:
Dalili ya mtu kupungukiwa maji mwilini ni pamoja na kuumwa kichwa. Kunywa maji ya kutosha na hutasumbuliwa sana na kuumwa kichwa mara kwa mara.
5:NGOZI NYORORO:
Unywaji maji ya kutosha kila siku unaweza safisha ngozi yako na kuifanya ionekane nyororo.
6: MATAZIZO YA CHOO:
Maji ni dawa ya kutibu ukosefu wa choo, kunywa maji ya kutosha kila siku na utajiepusha na tatizo la ukosefu wa choo mara kwa mara.
7: USAFISHAJI WA MWILI:
Maji husaidia kuondoa sumu mwilini kwa kutoa uchafu wote kwa njia ya mkojo na haja kubwa.
8: SARATANI:
Utajiepusha na saratani ya tumbo kwa kunywa maji, kwani maji husaidia suala la usagaji wa chakula tumboni na hivyo wakati wote tumbo lako litakuwa safi. Utajiondoa katika hatari ya kupata saratani ya tumbo kwa asilimia 45 na asilimia 50 kwa saratani ya kibofu cha mkojo.
9: MAZOEZI:
Mwili unapokuwa na maji ya kutosha, yatakufanya uwe na nguvu ya kufanya mazoezi yako ya kutosha, hivyo kupata faida ya mazoezi ipasavyo.
No comments:
Post a Comment