Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akizungumza na Wadau wa Utalii mkoa wa Kilimanjaro alipokutana nao katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi.
Baadhi ya Wadau wa Utalii wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii (hayupo pichani) alipokutana nao. |
Mhifadhi Mkuu mpya wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) Betrita Loibooki akiwa katika kikao hicho ambapo alitamburishwa rasmi akichukua nafasi ya Erastus Lufunguro aliyehamishiwa Makao Makuu, Mhifadhi Loibooki alikuwa Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Arusha (ANAPA).
Baadhi ya wamiliki wa kampuni za Utalii wakiwa katika mkutano huo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Amosi Makala akizungumza wakati wa kikao hicho.
Aliyekuwa Mhifadhi Utalii katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, (KINAPA) Eva Mallya ambaye kwa sasa amehamishiwa Hifadhi ya Taifa ya Manyara akiteta jambo na Mhifadhi mkuu mpya wa KINAPA,Betrita Loibooki.
Katibu wa Chama cha Waongoza Watalii mkoa wa Kilimanjaro (KGA) James Mong'ateko akiwasilisha malalamiko ya wapagazi mbele ya Waziri wa Maliasili na Utalii .(hayupo pichani)
Waziri Maghembe na Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Allan Kijazi wakimsikiliza kwa makini katibu wa Chama cha Waongoza watalii mkoa wa Kilimanjaro (KGA) James Mong'ateko (hayupo pichani ) alipokuwa akieleza changamoto.
Mkurugenzi Mkuu Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) Allan Kijazi akizungumza wakati wa kikao cha Waziri wa Utalii na Wadauu wa Utalii kilichofanyika mkoani Kilimanjaro.
Katibu wa KGA,James Mong'ateko akikabidhi kwa Waziri Maghembe taarifa iliyohusu Changamoto mbalimbali wanazopata katika shughuli za kupanda Mlima Kilimanjaro.
Baadhi ya Wadau wa Utalii katika kikao hicho.
Na Dixon Busagaga wa Kanda ya Kaskazini.
No comments:
Post a Comment