Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(katikati) akifuatana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu
(kulia) na Jiji Mkuu Tanzania Mohammmed Chande Othman wakati
alipowasili viwanja vya Victoria Garden katika sherehe za kilele cha
siku ya sheria Zanzibar.
Kikundi
cha sanaa na maigizo cha Blackroot walipotoa igizo lao leo katika
sherehe za kilele cha siku ya Sheria Zanzibar zilizofanyika leo katika
viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja mbele ya mgeni rasmi Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
Mwanasheria
Mkuu zanzibar Said Hassan Saidi akitoa maelezo mafupi na kumkaribisha
jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu wakati wa sherehe za kilele
cha siku ya Sheria Zanzibar zilizofanyika leo katika viwanja vya
Victoria Garden Mjini Unguja.
Jaji
Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu akitoa hutuba yake wakati
wa sherehe za kilele cha siku ya sheria Zanzibar kabla ya kumkaribisha
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein kuzungumza na wananchi katika sherehe za siku hii ya sheria.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akionesha kitabu cha Sheria ya mwaka Zanzibar (ZANZIBAR YEARBOOKOF LAW)
Volume 4 baada ya kukizindua rasmi leo katika sherehe za kilele cha
siku ya sheria Zanzibar katika viwanja vya Victoria Garden Mjini
Unguja,(kulia)Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu,(kushoto) naibu
Spika wa Baraza la Wawakilishi Ali Abdalla,Makamo wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Jaji Mkuu wa Tanzania Mohammed Othman
Chande.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
alipokuwa akitoa hutuba yake leo kwa Wananchi katika sherehe za kilele
cha siku ya sheria Zanzibar zilizofanyika katika viwanja vya Victoria
Garden Mjini Unguja,(kulia)Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu
na Jaji Mkuu wa Tanzania Mohammed Othman Chande.
Baadhi ya
majaji waliohudhuria katika sherehe za kilele cha siku ya sheria
Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake leo kwa
Wananchi katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja.
{Picha na Ikulu.]
No comments:
Post a Comment