Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa akigawa vyandarua vya bila malipo
kwa wananchi wa kijiji cha Chamwino Ikulu wakati wa uzinduzi wa kampeni
ya ugawaji vyandarua Mkoani humo Februari 9, 2016.
Kikundi
cha ngoma za asili ya kigogo cha Chamwino Ikulu Dodoma kikitumbuiza
wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Mkoa wa Dodoma ya kugawa vyandarua vya
bila malipo kwa kaya Februari 9, 2016.
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa akiwafundisha wananchi wa Chamwino
Ikulu namna bora ya kuwakinga watoto dhidi ya mbu na malaria kwa
kuwalaza kwenye vyandarua wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ugawaji
vyandarua Mkoani humo Februari 9, 2016.
Waliohudhuria
uzinduzi wa kampeni ya ugawaji vyandarua vya bila malipo wakifuatilia
onesho alilolifanya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma (hayupo pichani)la namna bora
ya kuwakinga watoto dhidi ya mbu na malaria kwa kuwalaza kwenye
vyandarua.
Maafisa
wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Dodoma wakiwaonesha Wananchi wa
Chamwino Ikulu namna bora ya kujikinga dhidi ya mbu na malaria kwa
kulala kwenye vyandarua wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ugawaji
vyandarua vya bila malipo Mkoani humo Februari 9, 2016.
Wananchi
wa mitaa mbalimbali ya Mkoa wa Dodoma wakiwa wamejipanga kwenye mistari
ya kusubiria kugawiwa vyandarua vya bila malipo Februari 9, 2016.
No comments:
Post a Comment