Junior Mwemezi wa Azam Tv na Faustine Ruta
Magari yaliyowasili hii leo katika Uwanja wa Kaitaba yaliyoleta vifaa kwa ajili ya Umaliziaji wa Ujenzi wa Uwanja ambao ujenzi wake ulikuwa ukisua sua kutokana na kukwama kwa Vifaa hivyo Jijini Dar es salaam.
Magari yaliyowasili hii leo katika Uwanja wa Kaitaba yaliyoleta vifaa kwa ajili ya Umaliziaji wa Ujenzi wa Uwanja ambao ujenzi wake ulikuwa ukisua sua kutokana na kukwama kwa Vifaa hivyo Jijini Dar es salaam.
Mesh rubber crumb
Mshauri
wa ufundi Bwana Rutayunga Peregrinus akiteta jambo na waandishi wa
habari(kulia) leo kwenye Uwanja wa Kaitaba juu ya Umaliziaji wa Uwanja
huo muda mfupi baada ya Vifaa hivyo kuwasili hii leo. Picha Na Faustine Ruta wa bukobasports.com
Mshauri wa ufundi Bwana Rutayunga Peregrinus
Ndipo
akafafanua kwamba Uwanja baada ya Vifaa kuwasili umaliziaji utaanza
mara moja huku akisisitiza kwamba Mwezi huu wa februari kama mambo
yaenda vyema utamalizika. Na Timu ya Kagera Sugar itamalizia michezo
yake ya Msimu huu kwenye Uwanja huu. Pia Bukobasports imeweza kupata
habari zaidi kuwa Rais wa TFF Bw. Jamal Malinzi nae yupo Mjini hapa
Bukoba akifuatilia Mradi huo wa Uwanja unavyoendelea na kesho Jumamosi
atakutana na Viongozi wengine na kuteta nao na hatimae kukamilisha
Ujenzi huo wa Uwanja Mwezi huu wa Februari.
Afisa utamaduni wa Mkoa wa Kagera Bw. Rugeiyamu nae alikuwepo katika Uwanja huo. Picha Na Faustine Ruta wa bukobasports.com
Junior Mwemezi wa Azam Tv akiteta jambo na Mshauri wa ufundi Bwana Rutayunga Peregrinus
Swala zima ni juu ya Umaliziaji wa Uwanja wa Kaitaba ndicho kilichokuwa kikisisitizwa leo baada ya Vifaa kuwasili.
Sehemu ya Uwanja huo kama unavyoonekana ukiwa ulishawekwa nyasi bandia
Sehemu ya Ukingo ambayo ukutanisha maji na kuyatoa nje kupitia kwenye bomba maalum.Junior Mwemezi wa Azam Tv na Fausti Ruta Taswira ya Uwanja wa Kaitaba ulivyo kwa sasa.Junior
Mwemezi wa Azam Tv na Fausti Ruta wa bukobasports walipata muda
wakapumzika japo kwa uchache katika Uwanja huo ambao unaelekea
kumalizika ujenzi wake.
No comments:
Post a Comment