Mfuko wa Jamii : Waziri Simbachawene Atembelea mfuko wa Pensheni wa LAPF Mjini Dodoma - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Friday, 5 February 2016

Mfuko wa Jamii : Waziri Simbachawene Atembelea mfuko wa Pensheni wa LAPF Mjini Dodoma


WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simba chawene ametembelea ofisi za Mfuko wa Pension wa LAPF mjini Dodoma. Katika ziara hiyo mh. Waziri amepongeza jitihada za Mfuko kuongeza Wanachana kila mwaka pamoja na huduma bora zinazotolewa kwa wanachama hasa katika kulipa mapema madai ya wananchama.

Akiongea na watumishi wa Mfuko wa LAPF amepongeza jitihada za watumishi kwa utendaji wao mzuri unaopelekea utendaji bora wa Mfuko. Mh. waziri amepongeza uwekezaji unaofanywa na LAPF katika kuhakikisha Mfuko unakuwa endelevu . 

Pia ameahidi kushirikiana na Mfuko ili kuhakikisha unaendelea kufanya vizuri zaidi.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simba chawene akisalimiana na kiongozi wa LAPF alipotembelea ofisi za Mfuko wa Pension wa LAPF mjini Dodoma.
 Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simba chawene akisaini kitabu cha wageni alipotembelea ofisi za Mfuko wa Pension wa LAPF mjini Dodoma.

Wafanyakazi wa Mfuko wa Pension wa LAPF  wakimsikiliza Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simba chawene alipotembelea ofisi za Mfuko huo mjini Dodoma.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simba chawene akizungumza na wafanyakazi wa  Mfuko wa Pension wa LAPF alipotembelea ofisi za Mfuko huo mjini Dodoma. 

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simba chaweneakizungumza na wafanyakazi wa mfuko huo alipotembelea ofisi za Mfuko wa Pension wa LAPF mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment