Na Ferdinand Shayo wa Wazalendo 25 Blog,Arusha.
Naibu Waziri
wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Susan Kolimba amezitaka mamlaka zinazofanya kazi katika mpaka kati ya
Kenya na Tanzania wa Holili kuhakikisha kuwa wanatatua matatizo ya uchache wa
wafanyakazi,uhaba wa vitendea kazi ili kuhakikisha kuwa wanatatua kero za
wananchi wanaofanya biashara na shughuli za kijamii katika ukanda wa Afrika
mashariki.
Akizungumza
mara baada ya kufanya ziara yake mwishoni mwa wiki katika mpaka wa Holili
ambapo alizungumza na wafanyakazi wa vitengo mbali mbali vya serikali ikiwemo
TBS,TFDA,Uhamiaji,Polisi pamoja na idara nyingine ambazo ziliwasilisha
changamoto zao mbele ya waziri huyo ambaye aliahidi kuzifikisha kwa mamlaka
husika ili ziweze kutatuliwa.
“Tunahitaji kuboresha huduma katika
mipaka ili biashara zienfdelee na kukuza mahusiano mazuri katika jumuiya ya
Afrika mashariki “
Alisema Kolimba
Mkaguzi wa
TFDA ,Edward Mwamilawa amesema kuwa licha ya unyeti wa mpaka huo bado ofisi
yake inakabiliwa na uhaba wa vifaa vya kitaalamu vya kupima ubora wa vyakula na
vipodozi jambo ambalo linazorotesha utendaji hivyo ameiomba serikali isaidie
kitengo hicho ili kiweze kufanya kazi kwa ufanisi.
Mkuu wa
kituo cha TRA mpaka wa Holili Mwaikalobo Aden na Afisa wa Mamlaka ya Kukusanya
kodi nchini Kenya (KRA) Dan Nyambaka wamesema kuwa ukusanyaji wa mapato katika
mpaka huo umekua ukiongezeka kutokana na biashara inayofanyika kati ya Tanzania
na Kenya .
Kuanzishwa kwa kituo kimoja Mpakani
(One Stop Border Post) kimerahisisha upatikanaji wa huduma za kiutawala na
kurahisisha biashara kati ya nchi Mwanachama wa jumuiya ya Afrika
Mashariki .
No comments:
Post a Comment