Jaji Mkuu wa Tanzania, Othuman Chande, akikaribishwa kutembea mabanda mbalimbali kwenye maonesho hayo.
Mkurugenzi
Msaidizi Ukaguzi na Maadili Mahakama ya Tanzania, Warsha Ng'humbu
(kushoto), akimuelekeza jambo Balbina Mrosso (kulia), kutoka Babati
mkoani Manyara aliyetembelea banda la Idara ya Malalamiko kuomba msaada
wa kisheria katika maonyesho hayo.
Jaji
Mkuu wa Tanzania, Othuman Chande, akisoma moja ya daftari katika banda
la Idara ya Malalamiko kwenye maonyesho hayo. Kulia ni Mkurugenzi
Msaidizi Kitengo cha Malalamiko Mahakama ya Tanzania, Happiness
Ndesamburo.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Othuman Chande (kulia), akielekezwa jambo katika banda la Divisheni ya Biashara katika maonesho hayo.
JAJI
Mkuu wa Tanzania Othuman Chande ametoa siku saba kwa mahakimu 508 watoe
maelezo ni kwanini wasifunguliwe mashtaka ya nidhamu na kuwajibishwa,
baada ya kufanya kazi chini ya kiwango.
Jaji
Chande ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari
katika Viwanja vya Mnanzi Mmoja jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya
kuadhimisha Wiki ya Sheria.
Alisema
kiwango cha kesi kwa kila Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi na
Mahakama ya Wilaya ni 250, ambapo Mahakimu Wakazi 121 kwenye mahakama
hizo wameamua kesi chini ya 100 mwaka jana.
Alibainisha
kuwa kiwango cha kwa kila Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo ni 260, ambapo
mahakimu Wakazi na Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo 387 wameamua kesi
chini ya 100 mwaka jana.
"Ukiondoa wale ambao wameajiriwa karibuni, wanaofanya kazi kwenye
mahakama za mwanzo zisizokua na mashauri mengi au waliyokwenda masomoni
kati kati ya mwaka au likizo za ujauzito hawatahusika katika sakata la
kujieleza.
"Majaji Wafawidhi nimewaagiza wachambue na kuanisha mahakimu wote
walioshindwa kufikia kiwango cha kesi walizopaswa kuamua kesi 250 na
kesi 260 kwa mwaka jana na kuwataka watoe maelezo ndani ya siku saba kwa
nini wasichukuliwe hatua," alisema Jaji Chande
Jaji Chande alitoa muda wa kukamilika kwa mchakato huo, ambapo
walizitaka idara husika ndani ya siku 21 kila kitu kiwe kimekamilika ili
ijulikane ni hatua gani wanachukuliwe.
"Mahakama haikubali hakimu ambaye anabembeleza kesi. Hakimu
hatakiwi kufanya hivyo anatakiwa asikilize kesi hizo naazimalize.
Haiwezekani katika mahakama moja hakimu mmoja anamaliza kesi 800
mwingine anamalizia chini ya 100 hilo halitakubalika kutokana na kasi
ambayo tunayo," alisema
Jaji Chande alisema mahakimu hao watapelekwa katika kamati zao kwa
hatua ya kujieleza. Kazi kuu ya kamati hizo ni kupeleleza, kuchunguza
na kushughulikia mashtaka yote ya nidhamu ya mahakimu.
"Mahakimu wote walioshindwa kufikia malengo ya mwaka la kesi na
kushindwa kutoan sababu za kuridhisha kwa nini wameamua idadi ndogo ya
kesi kuliko walivyopaswa, ambapo itashughulikiwa haraka na Kamati za
Maadili za Mahyakimu kwa mujibu wa sheria na taratibu za haki," alisema
Hata hivyo, Jaji Chande alitoa pongezi kwa mahakimu ambao wamevuka
kiwango, ambapo mahakimu 14 wameamua zaidi ya kesi 700 kwa mwaka jana
na mahakimu wengine wamesikiliza kesi 915,789 na 778.
Alisema mkakati wao ni kuanza kesi sifuri mwaka unapoanza, kwa
sababu kuna baadhi ya mahakama za mwanzo zimekuwa zikimaliza kesi na
kuanza mwaka upya.
Jaji Chande alisema Januari 1, 2015 mahakama za mwanzo zilianza na
kesi 34,126 na mwaka huu Januari 1 zilianza na kesi 20,431. Kiwango cha
kumaliza kesi ukilinganisha na idadi ya kesi zilizosajiliwa 2015 nni
zaidi ya asilimia 100. Mahakama ya Mkuranga asilimia 141, Rufiji
asilimia 121 na Bukoba Mjini asilimia 224.
No comments:
Post a Comment