Na Mwandishi Wetu,
Mgodi
wa dhahabu wa Buzwagi umeikabidhi timu ya ambassador FC ya wilayani
Kahama kitita cha shilingi milioni kumi na laki tano kama sehemu ya
msaada kwa ajili ya
maandalizi ya kushiriki michuano ya ligi daraja la pili ngazi ya mkoa -
Shinyanga.
Msaada
huo ambao ulikabidhiwa na meneja mkuu wa Mgodi wa Buzwagi, Mhandisi Asa
Mwaipopo umetolewa kwa timu hiyo ili kuiwezesha kufanya vizuri katika
michuano ya ligi
daraja la pili inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi mfano wa hundi, meneja mkuu wa Buzwagi amesema
msaada huo kwa timu ya ambassador ni mwendelezo wa harakati zinazofanywa
na kampuni
yake katika kuhakikisha makundi mbalimbali yanayozunguka maeneo ya
mgodi huo yananufaika na fursa mbalimbali zilizopo.
“Lengo
letu kubwa la kutoa msaada huu ni kutekeleza ahadi yetu ya kuisaidia
Jamii inayotuzunguka na tungependa kuona hata kupitia michezo vijana
wanajitengenezea
ajira, kama mnakumbuka tumetoa udhamini kwa timu ya Stand Utd
inayoshiriki Ligi kuu ya Vodacom na sasa tumetoa msaada huu wa fedha ili
kuisaidia timu hii ili nayo iweze kufanya vizuri katika mashindano
yaliyo mbele yao”.alisema Mwaipopo.
Kwa
upande wake katibu wa timu ya Ambassador FC, Bakari Khalid ameushukuru
uongozi wa mgodi wa Buzwagi kwa msaada huo ambao amesema utasaidia
kuongeza hali ya mchezo
kwa wachezaji wa timu yake.
“Natoa
shukrani kwa uongozi wa Buzwagi kwa msaada huu, niwaahidi kwamba sisi
kama Ambasador tutafanya vizuri nakuwa mabalozi wa kuitangaza Kahama
katika sekta
ya michezo, kwani tunao vijana wazuri wenye uwezo wa kucheza mpira na
kwa kufanya hivi tunawahakikishia baadhi ya vijana ajira kupitia
michezo” Alisema Bakari.
Katika hatua nyingine timu hiyo ya ambassador FC ambayo iko chini ya kocha Karume Songoro ambaye amewahi kuzichezea timu za Yanga na timu ya taifa ya Tanzania, ilimenyana na timu ya mpira ya Buzwagi mchezo ambao uliisha kwa Ambassador iliibuka na ushindi wa goli 2-1
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo
(kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi katibu mkuu wa Ambassador FC,
Bakari Khalid kwa ajili ya maandalizi ya ligi daraja la pili mkoa wa
Shinyanga..
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo
(kushoto) na Bakari Khalid Katibu mkuu wa timu ya Ambassador wakati wa
hafla ya kukabidhi msaada kwa timu hiyo.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kukabidhi hundi timu
ya Ambassador FC.
Katibu wa timu ya Ambassador FC, Bakari Khalid akizungumza mara baada ya kukabidhiwa hundi na Uongozi wa Mgodi wa Buzwagi.
Kikosi cha wachezaji wa Ambassador FC.
Kikosi cha timu ya Buzwagi FC
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo
(mwenye kofia) akisalimiana na Captain wa timu ya Buzwagi, Saimon Sanga
wakati wa mchezo wao wa kirafiki na timu ya Ambassador FC.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo (mwenye kofia) akisalimiana na wachezaji wa timu ya Ambassador FC.
Kikosi cha timu ya soka ya mgodi wa Buzwagi kikiwa
katika picha ya pamoja wakati wa hafla ya kukabidhi hundi kwa timu ya
Ambassador FC. Katika mchezo huo timu ya Ambassador FC iliibuka mshindi
kwa kuwafunga wenyeji wao Buzwagi FC, 2-1.
No comments:
Post a Comment