Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa,
Balozi Dkt. Augustine Mahiga, (wanne kutoka kushoto), Naibu Waziri wa Wizara
hiyo, Dkt. Susan Kolimba, (watatu kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja
na Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, EALA, kutoka Tanzania, Mh. Shy-Rose
Bhanji, 9wakwanza kushoto), Mh. Makongoro Nyerere (wapili kushoto), Mh. Angella
Kizigha, (Wasita kutoka kushoto), naMh. Bernard Murunya). Wabunge hao
walikwenda kumsalimia waziri Mahiga na kujitambuslisha ikiwa ni siku chache
kabla ya kuanza vikao vya bunge hilo jijini Arusha Januari 24, 2016. (K-VIS
MEDIA/Khalfan Said)
NA
K-VIS MEDIA/Khalfan Said
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa,
Balozi Dkt. Augustine Mahiga, mapema leo Ijumaa Januari 15, 2016
amekutana na Wabunge
wa Bunge la Afrika Mashariki, (EALA), kutoka Tanzania waliokwenda kujitambulisha
na kubadilishana mawazo ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Wabunge
hao waliongozwa na mwenyekiti wa wabunge wa Tanzania, Mh. Makongoro Nyerere,
Mh. Shy-Rose Bhanji, Mh. Angella Kizigha, na Mh.Bernard Murunya.
Naibu
Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Susan Kolimbanaye alikuwepo wakatiwa kikao hicho
kifupi cha kutambuana.
Akizungumza
na Waandishi wa habari mara baada ya kikao hicho, Mwenyekiti wa wabunge wa EALA
kutoka Tanzania, Mh. Makongoro Nyerere, alisema, “Tumefika kujitambulisha kwa
Mh. Waziri kama ujuavyo yeye ni mgeni kwenye wizara hiyo, tulikuwana Dkt.
Mwakyembe na sasa tunaye Dk. Augustine Mhiga, kwa hivyo tuliona ni
vyematukafika kujitambulisha na kutambuana.” AlisemaMh. Makongoro na
kuongeza, “Lakini
pia lazima utambue kuwa vikao vya EALA, vinaanza Januari 24 pale Arusha na Mh.
Mahiga ndiye mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki, kwa hivyo
sio busara tukakutanie kule ndio maana tumeona ni vema tukaja kumsalimia hapa
atutambue na kubadilishana mawazo hapa na pale.” Alimaliza Mh.
Makongoro.
Bunge
la Afrika Mashariki, EALA, ni chombo cha kutunga sheria cha Juamuiya ya Afrika
Mashariki na linaundwa na nchiwanachama wa Jumuiya hiyo ambaonipamoja na
Tanzania, inayoshikilia uenyekiti kwa sasa, Uganda, Kenya, Rwanda na
Burundi.
Dkt. Mahiga, akisaliamiana na
mmoja wa wabunge hao, Mh. Shy-Rose Bhanji
Mh. Shy-Rose Bhanji akiwa katika
picha ya pamoja na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na
Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga, (wakwanza kushoto) na maafisa wengine wa
wizara hiyo, mara baada ya kikao hicho
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dkt. Susan Kolimba, akisalimiana na Mh. Shy-Rose Bhanji |
Mh. Makongoro Nyerere, akipeana
mikono na Bi. Mindi Kasiga
No comments:
Post a Comment