Matukio :Halmashauri ya jiji La Arusha yaweka mkakati wa kuboresha makazi ya wananchi wake. - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Tuesday, 19 January 2016

Matukio :Halmashauri ya jiji La Arusha yaweka mkakati wa kuboresha makazi ya wananchi wake.





Afisa Uhusiano wa Jiji la Arusha, Bi. Ntegenjwa Hosea.

 Na Vero Ignatus wa Wazalendo 25 Blog , Arusha.
ARUSHA: Jiji la Arusha limeingia mkataba na wa makubaliano na kampuni ya Bondeni service ya kuendeleza shambalao lenye ukubwa wa hekari 750 lililopo katika kata ya Murieti. Hayo yamesemwa na Afisa uhusiano nwa Halmashauri hiyo bi Ntegenjwa Hosea alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa shamba hili litagawanywa viwanja ambavyo vitauzwa kwa wananchi wote wa ndani na wa nje wa jiji la Arusha. Amesema kuwa lengo kubwa la kuuza viwanja hivyo ni kupunguza makazi holela katika Jiji la Arusha na mji unakuwa kimkakati,uwe umepangikakwa nyakati zote na kwa utaratibu unaoeleweka na kuhakikisha kwamba eneo kubwa la mji linakuwa limepimwa. 

Aidha amesema kuwa mkataba huo ni wa kwanza wao kama jiji ,na amesema kuwa ni mlango mzuri kwa wananchi wote pamoja na makampuni wenye maeneo yao makubwa kwa kuyaongeza thamani,kwa kuingia makubaliano na Halmashauri na wakaweza kusimamiwa taratibu zote za mpango mji na utazamaji wa ramani ya eneo husika na upimaji wa viwanja. Amesema kuwa viwanja vikiwa vimepimwa vinaongezeka thamani tofauti na ambavyo havijapimwa,hivyo amewataka wananchi wote wa jiji la Arusha kutumia fursa hii ipasavyo,na amesema kuwa baada ya halmashauri ya jiji la Arusha kusaini mkataba huo utekelezaji unaanza mara moja na amewataka wananchi wategemee mambo mazuri kutoka kwenye mradi huo. 

Katika hatua nyingine mkurugenzi wa jiji la Arusha Iddi juma amwewataka viongozi wote waliochaguliwa na wananchi kuhakikusha kuwa wanashirikiana nao ktk kuleta maendeleo katika jiji la Arusha bila kujali itikadi za vyama vyao. Sambambana hayo kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya arusha imepiga marufuku uuzwaji holela wa vyakula visivyozingatia kanuni za afya,ikiwemo uuzaji wa matunda kwenye mikokoteni,uuzwaji wa vyakula hovyo katika maeneo ya masokoni na kwenye mikusanyiko ya watu,ambayo mazingira siyo rafiki na hupelekea kuchochea maambukizo ya ugojwa wa kipindupindu. 

Hii ni kutokana na ugonjwa wa kipindupindu kulisumbua jiji la Arusha tangia octoba 2015 hadi hadi sasa januari 2016 bado ugonjwa huo upo ,wananchi wote wametakiwa kuzingatia usafi wao binafsi haswa kunawa mikono kwa sabuni na maji safi na salama mara baada ya kutoka chooni kabla na baada ya kula chakula

No comments:

Post a Comment