Maisha : Balozi Paul Rupia Afanya Misa ya Kutimiza Miaka 80 - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Sunday, 10 January 2016

Maisha : Balozi Paul Rupia Afanya Misa ya Kutimiza Miaka 80

Pauline Rupia akiwa na Wajukuu wa Balozi Paul Rupia katika Misa ya kutimiza miaka 80 katika kanisa la Anglikana Dar es Salaam.
Balozi Paul Rupia akiwa pamoja na familia yake katika misa ya kutimiza miaka 80 iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Anglican Dar es Salaam.
Judge Augustino Ramadhani (kushoto) akimpongeza Balozi Paul Rupia kwa kutimiza miaka 80 wakati wa Misa Maalumu ya Shukrani iliyofanyika jana katika Kanisa Kuu la Anglikana Dar es Salaam.
Balozi Paul Rupia akiwa na Mkewe Rose Rupia kabla ya kuanza kwa Misa Maalum ya Shukrani ya kutimiza miaka 80 ya kuzaliwa jana katika kanisa la Angalikana.
Familia ikimsindikiza Balozi Paul Rupia kupata Baraka kutoka kwa Askofu Valentino Mokiwa katika Misa ya Shukrani ya kutimiza miaka 80 ya kuzaliwa iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Anglikana Dar es Salaam.
Askofu Valentino Mokiwa akianza kutoa Baraka kwa Balozi Paul Rupia na familia yake.
Mzee Balozi Paul Rupia (kulia) akizungumza katika Misa ya shukrani iliyoongozwa na Askofu wa Dayosisi ya Dar es Salaam ya Kanisa la Kianglikana Tanzania Valentino Mokiwa (kushoto) iliyofanyika katika Kanisa la St. Alban Posta Dar es Salaam jana. Misa hiyo ya shukrani ilifanyika katika kuadhimisha sikukuu ya kuzaliwa ambapo jana alitimiza miaka 80. Katika ni Mke wake Mama Rose Paul Rupia.
Askofu Valentino Mokiwa akitoa Baraka kwa Balozi Paul Rupia, familia yake na ndugu na jamaa waliohudhuria misa ya shukrani ya kutimiza miaka 80 ya kuzaliwa katika Kanisa Kuu la Anglikana la Mtakatifu Albano Dar es Salaam.
Balozi Paul Rupia akiwashukuru ndugu na jamaa waliohudhuria ibada ya shukrani ya kutimiza miaka 80 iliyofanyika katika Kanisa kuu la Mtakatifu Albano Dar es Salaam jana.
Balozi Paul Bomani akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Wananchi wa Dar es Salam (DCB) Bwana Edmund Mkwawa (katikati) nje ya Kanisa la Kianglikana la Mtakatifu Albano baada ya kumalizika kwa ibada ya shukrani ya kutimiza miaka 80. Balozi Rupia ni Mwenyekiti wa DCB.
Simon Mihayo Rupia (katikati) akiwa na Mama yake Mdogo (kushoto) na Shemeji yake Peter mara baada ya ibada.
Mtoto wa kwanza wa Balozi Paul Rupia Bwana Peter Rupia (wa tatu kulia) akiwa na wadogo zake baada ya misa ya shukrani ya kutimiza miaka 80 ya Baba yake iliyofanyika jana Kanisa la Kianglikana Mtakatifu Albano Dar es Salaam.
Balozi Paul Rupia (katikati) akiteta jambo na Askofu Valentino Mokiwa (kulia) na Jaji Msataafu Joseph Sinde Warioba (kushoto) baada ya misa ya shukrani ya kutimiza miaka 80 ya kuzaliwa.
Balozi Paul Rupia akiwa na Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba.
Mama Rose Paul Rupia akiwa na wanawe baada ya misa ya shukrani ya kutimiza miaka 80 ya Balozi Paul Rupia. Kulia ni Susan Kidha - Rupia na kushoto ni Chris Kalunde Rupia.
Balozi Paul Rupia (kulia) akiwa na mwanae wa mwisho Chris Kalunde Rupia mara baada ya misa ya shukrani ya kutimiza miaka 80 ya kuzaliwa iliyofanyika jana katika Kanisa la Anglikana Mtakatifu Albano Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment