Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis
Kigwangala leo majira ya jioni amefanya ziara ya kushtukiza katika
kituo kinachotoa tiba mbadala cha Foreplan Clinic kinachomilikiwa na Dk.
Mwaka Juma Mwaka kilichopo Ilala Bungoni na kujionea hali halisi ya
kituo hicho. Mara baada ya kufika alianza kufanya ukaguzi kuanzia sehemu
ya Mapokezi mpaka kwenye vyumba vya matabibu lakini katika vyumba vyote
hakuna daktari aliyekuwa anatoa huduma.
Akizungumza
na wagonjwa waliokuwa wakisubilia tiba alisema kuna waliofika katika
kituo hicho ili kutibiwa lakini kituo hicho hakina uwezo wa kuwahudumia
wagonjwa hao. Na kuwataka wagonjwa hao waende kwenye hospitali ili
wapate matibabu yanayoendana na magonjwa wanayoumwa.
Akizungumza
msaidizi wa Dk. Mwaka, Bi Teddy L. Mbuya alisema yeye hawezi kusema
kuhusu kituo hicho maana yeye sio msemaji mkuu bali alimwomba Naibu
waziri kufanya ukaguzi katika kituo hicho pamoja na kuwaliza maswali
wahusika mbalimbali wa vitengo vya ktuo hicho.
Baada
ya ukaguzi wa kituo hicho Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala amemwagiza Mkurugenzi
Msaidizi Tiba Asilia na mbadala Dk.Paul Mhame ndani ya wiki moja kufanya
ukaguzi kwa kituo cha Dk. Mwaka na aletewe taarifa iliyokamilika
kuhusu taaruma yeke pamoja na washirika wake na pia dawa anazozitumia
kama ni rafiki kwa wananchi wanaotumia dwa hizo pamoja na kufanya
ukaguzi wa vituo vyote vinavyotoa tiba mbadala na tiba asilia kama Dk.
Ndodi, Dk. Rahabu nk. ili kuwabaini wanaowalaghai wananchi.
Pia
amesema Dk Mwaka Juma Mwaka amekuwa akijitangaza kupitia vyombo
mbalimbali hapa nchini ambavyo ni kosa la kutangaza kama unafanya kazi
za tiba tabibu. Alisema madaktari wana miiko na katika miiko hiyo ambayo
inatumika na mojawapo ikiwa ni kutojitangaza. Naibu waziri aliendelea
kusema kuwa Dk. Mwaka amekuwa akijiita Dokta na amekuwa akichambua mwili
wa binadamu kama vile ameusomea udakitari wakati sheria ya tiba asilia
na tiba mbadala hairuhusu watu wa tibaAsilia na Tiba Mbadala kutumia
maneno ya tiba ya kisasa.
Pia
Naibu Waziri amamtaka Dk. Mwaka Juma Mwaka kufika wizarani kesho saa
mbili asubuhi akiwa na nyaraka zake zote zinazohusu utoaji wa huduma ya
Tiba Mbadala kwani amekuwa akijiita majina ya tiba za kisasa na pia
kutibu kwa njia ya kisasa badala ya kutibu kwa njia ya Asilia au Tabibu.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis
Kigwangala akiwasili katika kituo cha Foreplan Clinic kinachotoa tiba
mbadala kilichopo Ilala Bungoni, jijini Dar es Salaam alipofanya ziara
ya kushtukiza katika kituo hicho leo jumatatu kulia ni Mkurugenzi
Msaidizi Tiba Asilia na tiba Mbadala Dk.Paul Mhame kutoka wizara ya Afya
na Ustawi wa jamii.(Picha na Geofrey Adroph wa Pamoja Blog)
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis
Kigwangala akipokelewa na mmoja wa wauguzi wa kituo hicho ambapo jina
lake halikupatikana kwa haraka baada ya mkurugenzi wa kituo hicho Dk.
Mwaka Juma Mwaka kutokuwepo kwenye kituo chake cha Foreplan Clinic
kilichopo Ilala Bungoni, jijini Dar es Salaam
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis
Kigwangala akipata maelezo kutoka kwa baadhi ya wananchi waliofika
kupata matibabu katika kituo cha Foreplan Clinic kuhusu huduma
zitolewazo katika kituo hicho kinachomilikiwa na Dk. Mwaka Juma Mwaka.
Masaidizi
wa Dk. Mwaka, Bi Teddy L. Mbuya akimtolea ufafanuzi Naibu Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala
kuhusu huduma zitolewazo katika kituo cha Foreplan Clinic mara baada ya
kuanza kukagua kituo hicho kinachotoa Tiba
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis
Kigwangala akikikagua kifaa kinachotumika kufanyia vipimo kwenye kituo
cha Foreplan Clinic wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika kituo
hicho leo jioni siku ya jumatatu
Hiki ndicho kifaa kinachotumika kupimia wagonjwa kwenye maabara ya kituo hicho cha Tiba Mbadala.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis
Kigwangala akiwauliza maswali wasaizizi wa kituo hicho wakiongozwa na
Bi Teddy L. Mbuya mara baada ya kukuta hari ya sintofahamu katika kituo
hicho.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis
Kigwangala akikagua moja ya dawa zinazotolewa kwa wangonjwa wanaokuja
kutibiwa katika kituo hicho cha tiba Mbadala.
Bi.
Rozaria Antoni ambaye ni muhudumu wa dawa akikaa kimya baada ya
kuulizwa maswali na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala na kukosa la kujibu.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis
Kigwangala akimpa maelekezo Mkurugenzi Msaidizi Tiba Asilia na mbadala
Dk.Paul Mhame kutoka wizara ya Afya na Ustawi wa jamii.
No comments:
Post a Comment