Mkurugenzi
wa maendeleo ya Utamaduni Profesa. Hermas Mwansoko akizungumza na
watumishi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni wakati akiwaaga rasmi jana
ofisini kwake. Mkurugenzi huyo anastaafu rasmi kuanzia tarehe 25 Desemba
2015.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Maendeleo ya Utamaduni sehemu ya Sanaa Bibi. Leaha Kihimbi
akielezea jambo wakati wa hafla ya kumuaga Mkurugenzi wa Maendeleo ya
Utamaduni anayemaliza muda wake Profesa Hermas Mwansoko (kulia) jana
jijini Dar es Salaam.
Afisa
Utamaduni wa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw.
Msami akitoa neno kwa niaba ya watumishi wa Idara ya Utamaduni wakati wa
hafla ya kumuaga Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni anayemaliza muda
wake katika utumishi wa umma Profesa. Hermas Mwansoko jana jijini Dar es
Salaam.
Baadhi
ya watumishi wa Idara ya Utamaduni wakifuatilia matukio mbalimbali
yaliyokuwa yakiendelea wakati wa hafla ya kumuaga Mkurugenzi wa
Maendeleo ya Utamaduni anayemaliza muda wake katika utumishi wa umma
Profesa. Hermas Mwansoko jana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa maendeleo ya Utamaduni Profesa. Hermas Mwansoko akipokea zawadi ya
picha inayoonyesha maisha ya kijijini wakat wa hafla kumugaa jana jijini
Dar es Salaam.anayemkabidhi zawadi hiyo ni Mkurugenzi Msaidizi wa
Maendeleo ya Utamaduni sehemu ya Sanaa Bibi. Leaha Kihimbi . Mkurugenzi
huyo anastaafu rasmi kuanzia tarehe 25 Desemba 2015.
Mkurugenzi
wa Maendeleo ya Utamaduni Profesa. Hermas Mwansoko akiwa katika picha
ya pamoja na baadhi watumishi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni wakati
hafla ya kumuaga rasmi Mkurugenzi huyo anayemaliza muda wake jana
ofisini kwake.
Picha na Frank Shija,WHVUM
No comments:
Post a Comment