MTANDAO
wa Wanawake na Katiba na Uchaguzi umeitaka Serikali ya Awamu ya Tano
iliyopo chini ya Rais Dk. John Pombe Magufuli ijenge misingi imara
itakayoondoa mazingira kandamizi kwa jamii ya chini hasa kwa akinamama.
Aidha
umeitaka serikali kuhakikisha inasimamia ipasavyo suala zima la
uwajibikaji na kupambana na vitendo vya kifisadi ambavyo ndivyo
vinavyowakandamiza wananchi.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na jopo la viongozi
wanaounda mtandao huo likiongozwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Mtandao,
Profesa Ruth Meena walipokuwa wakitoa tathmini juu ya mtazamo wa mtandao
huo baada ya Uchaguzi Mkuu na suala zima la usawa wa jinsia kwa
wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari.
Akizungumza
katika mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Wanawake Tanzania,
Mary Rusimbi ambaye ni mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba na
Uchaguzi alisema serikali ya awamu ya tano ina kila sababu ya kumjali
mwanamke na kutambua kuwa anamchango mkubwa katika maendeleo ya uchumi.
Alisema
Serikali hainabudi kujenga misingi imara ya uwajibikaji wa kweli na
kutambua makundi mbalimbali ya jamii kwa jinsia zote. "...Tunataka haki
yetu iwe haki kweli kweli na itambulike huku ikiwa nautekelezaji wa
vitendo na kwa uhakika," alisisitiza Bi. Rusimbi.
Mwenyekiti
wa Umoja wa Wanawake na Katiba na Uchaguzi, Profesa Ruth Meena
(kushoto) akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari leo
jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha
Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Wanawake Tanzania, Mary Rusimbi (kushoto) ambaye ni mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba na Uchaguzi akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake na Katiba na Uchaguzi, Profesa Ruth Meena.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Wanawake Tanzania, Mary Rusimbi (kushoto) ambaye ni mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba na Uchaguzi akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake na Katiba na Uchaguzi, Profesa Ruth Meena.
Mjumbe wa Mtandao huo, Dk. Ave-Maria Semakafu (kulia) akizungumza na
wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania
akisisitiza jambo kwenye mkutano na wahariri wa vyombo mbalimbali vya
habari leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji
wa Mfuko wa Wanawake Tanzania, Mary Rusimbi na Mwenyekiti wa Umoja wa
Wanawake na Katiba na Uchaguzi, Profesa Ruth Meena.
Alisema
kuwa wangependa kushuhudia idadi ya kutosha ya wanawake inaingia katika
ngazi mbalimbali za uongozi na vyombo vya maamuzi ili waweze kuingiza
changamoto zao na kuzisemea ipasavyo kwa lengo la kupatiwa ufumbuzi.
Kwa upande wake Prof. Meena akizungumzia mtazamo wa mtandao baada ya
Uchaguzi Mkuu juu ya ushirikishwaji wa wanawake katika kugombea nafasi
anuai za uongozi alisema bado kuna changamoto kubwa kwa kundi hilo kwani
kulingana na matokeo ya sasa Tanzania itafikia usawa wa 50/50 mwaka
2055.
Alisema
licha ya ongezeko la fursa ya vitimaalum kupandishwa hadi kufikia
asilimia 40 bado fursa hizo zinachangamoto kubwa kwani viti hivyo ndani
ya vyama hutolewa kwa wanawake kama aina fulani ya zawadi jambo ambalo
huwazuia wanawake hao kusimamia ajenda zao za msingi kwa kuhofia
kuonekana wasaliti.
"...Viti
hivi maalum hutolewa na vyama na vyama ndio vyenye ushawishi na
misimamo hivyo wanawake hawawezi kusimamia hoja zao ipasavyo...,"
alisema Prof. Meena.
Aidha Profesa Meena alivitaka vyombo vya habari kusaidia kubeba ajenda
za wanawake na kukemea mfumo dume ili kuibadili jamii ambayo bado
inamtazamo hasi juu ya wanawake na uwezo wao.
Alisema
wanawake walijitokeza kwa wingi katika uchaguzi huu licha ya kwamba
ndani ya vyama vyao bado kuna aina fulani ya ugumu katika kuwapa nafasi
kundi hilo.
Naye Mjumbe wa Mtandao huo, Dk Ave-Maria Semakafu aliitaka serikali
kuendelea kuondoa vikwanzo na changamoto mbalimbali katika jamii ambazo
bado zinamtesa mwanamke.
Alisema
huduma za elimu bado mtoto wa kike anachangamoto jambo ambalo
linamnyima kufikia malengo yake huku huduma nyingine za maji na
utafutaji wa nishati ya kuni ikiwa ni mzigo kwa mwanamke.
Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia mkutano
wao na viongozi wa Mtandao wa Wanawake na Katiba na Uchaguzi leo jijini
Dar es Salaam.
Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia mkutano
wao na viongozi wa Mtandao wa Wanawake na Katiba na Uchaguzi leo jijini
Dar es Salaam. *Imeandaliwa na www.thehabari.com
No comments:
Post a Comment