Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi
akipokea ngao yenye picha ya chui ikiwa ni ishara ya tuzo ya Shirika la
Nyumba la Taifa kwa Waziri huyo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC,
Nehemia Kyando Mchechu kwa kuonyesha utendaji uliokuwa wa kasi usiochoka
wakati Waziri Lukuvi alipotembelea katika Shirika hilo kuaga rasmi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi

akipokea kadi ya pongezi ya Shirika la Nyumba la Taifa kutoka kwa Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa Jamii, Susan Omari kwa
kuonyesha utendaji uliokuwa wa kasi usiochoka wakati Waziri Lukuvi
alipotembelea katika Shirika hilo kuaga rasmi.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza
na Wakurugenzi na Mameneja wa Makao Makuu ya Shirika hilo wakati Waziri
Lukuvi alipotembelea katika Shirika hilo kuaga rasmi.
Baadhi
ya mameneja wa Makao Makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)
wakifuatilia mazungumzo wakati Waziri Lukuvi alipotembelea katika
Shirika hilo kuaga rasmi.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza
na Wakurugenzi na Mameneja wa Makao Makuu ya Shirika hilo wakati Waziri
Lukuvi alipotembelea katika Shirika hilo kuaga rasmi.
Waziri Lukuvi akizungumza na Wakurugenzi na Mameneja wa Makao Makuu ya Shirika hilo wakati alipotembelea katika Shirika hilo kuaga rasmi kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu.

Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani, Fatma Chillo akizungumza kwa niaba ya Wakurugenzi
na Mameneja wa Makao Makuu ya Shirika hilo kumshukuru Waziri huyo
wakati Waziri alipotembelea katika Shirika hilo kuaga rasmi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi
ameiagiza Menejimenti ya Shirika hilo kuhakikisha inaendeleza kasi ya
ujenzi wa nyumba za makazi na biashara bila kusahau misingi iliyoliunda
shirika hilo.
Akizungumza
leo wakati akiaga rasmi Shirika hilo alisema amejifunza mengi katika
uwepo wake ndani ya Wizara na hasa dhamira na utendaji wa kasi wa
Shirika hilo na akaiagiza menejimenti ya Shirika hilo kufanya kazi bila
kuchoka likihakikisha linapigania makazi bora kwa kila mtanzania.
"Kabla
ya kuingia katika Wizara , na hata nilipoingia sikuwa nafahamu kwa kina
kwamba Shirika la Nyumba limebadilika kutoka lile la kuangalia nyumba
za msajili wa majumba na kuwa sasa limejenga nyumba nyingi na kuziuza
kwa Watanzania, sasa nimefahamu kwa kujifunza kwamba Shirika letu hili
limebuni utaratibu unaolifanya lifanye kazi kwa kasi kubwa kibiashara
lakini pia likibakia na 'human face', "alisema Lukuvi.
Alisema
Serikali inafahamu changamoto linazokabiliana nazo Shirika hilo za
ulipaji wa VAT mara mbili na gharama za miundombinu kama maji, umeme na
barabara ambazo mara kadhaa zimekuwa zikirudi kwa mnunuzi wa mwisho na
kwamba zinafanyiwa kazi pia akaliagiza Shirika na mamlaka hizo kukaa
pamoja na kuweka mipango yao pamoja ili angalau kuliwezesha Shirika
kuwafikia Watanzania wengi.
Waziri
Lukuvi alisema kuwa Serikali inaitambua sekta ya nyumba kuwa ni sekta
mtambuka kwa kuwa hukuza uchumi, huongeza ajira na kusaidia kudumisha
amani ya nchi yetu. Hivyo, alilihimiza Shirika hilo liendelee na mipango
yake kabambe ya kujenga nyumba za gharama nafuu ili kuwawezesha
wananchi wengi kumiliki nyumba.
Alisema
wananchi wengi wakimiliki nyumba utakuwa mkakati mmojawapo wa kupunguza
umaskini nchini maana wananchi hao wataweza kutumia nyumba zao kupata
mikopo benki ya kuendeleza shughuli zao za kiuchumi.
Akiungumzia
Serikali ya awamu ya Tano ijayo alisema kama kuna watumishi wa umma
ambao walikuwa wakifanya mambo kwa mazoea katika awamu zilizopita basi
awamu hii wahakikishe wanakuwa mguu sawa kwani Serikali ya Magufuli
ambayo inaingia madarakani ni serikali isiyotaka mchezo wala lele mama
na kwamba wala rushwa, na wazembe watatafuta mlango wa kutokea.
Akimkaribisha
Waziri Lukuvi, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia
Kyando Mchechu alisema Shirika hilo linatekeleza miradi yake ili
kuhakikisha linaweka makazi bora kwa Watanzania
Alisema kwa shirika hilo lonafanya hivyo kwa kuwa sekta ya nyumba ni sekta mtambuka katika maendeleo ya uchumi.
Sekta
ya nyumba husaidia kuleta maendeleo ya haraka ya sekta zinginena kutoa
ajira. Taifa linalozingatia sekta ya nyumba huwezesha nchi yao kuwa na
amani, kwani mtu mwenye makazi bora, huthamini uwepo wa amani.
No comments:
Post a Comment