Afya Zetu : Mtaalamu wa Upasuaji wa Uti wa Mgongo na Magonjwa ya Mfumo wa Fahamu kutoka Hospitali za Apollo kutoa Huduma Mwezi Novemba, Jijini Dar - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Tuesday, 10 November 2015

Afya Zetu : Mtaalamu wa Upasuaji wa Uti wa Mgongo na Magonjwa ya Mfumo wa Fahamu kutoka Hospitali za Apollo kutoa Huduma Mwezi Novemba, Jijini Dar

Dk. Alok Ranjan, Mkuu wa idara ya upasuaji wa uti wa mgongo na mfumo wa fahamu  Hospitali ya Apollo Hyderabad.

Na Mwandishi Wetu,

Kulingana na upungufu mkubwa wa wataalamu wa magonjwa ya mfumo wa fahamu Tanzania, vichanga 1000 kati ya 4000 wanaozalliwa na tatizo la mfumo wafahamu hupatiwa matibabu. Ina maanisha vichanga vilivyobaki huku ana tatizo la mfumo wa neva. Kutokana na ongezeko la watanzania kwenda nje kutafuta matibabu yanayohusisha mfumo wa fahamu na uti wa mgongo, na uwepo wa uhitaji wa wataalamu wa magonjwa ya jinsi hii kwa wingi zaidi, ujio wa mkuu wa idara ya upasuaji wa uti wa mgongo na mfumo wafahamu Dk.AlokRanjan kutoka Hospitali za Apollo Hyderabad utakuwa na msaada mkubwa sana kwa watanzania.

Watanzania wanashauriwa kutumia fursa hii kupata msaada wa kimatibabu kutoka kwa mtaalam huyu anayetambulika kimataifa. Dk.AlokRanjan kutoka Hospitaliza Apollo Hyderabad   atawaona wale wagonjwa wake wa awali aliowafanyia upasuaji katika hospitali ya Apollo ya mjini Hyderabad  lakini pia atatoa ushauri kwa wagonjwa wote hapa Tanzania wenye magonjwa yanayohusu mfumo wafahamu na uti wa mgongo.

Kliniki hii ya siku 3 itaanza tarehe 11, nakuendelea tarehe 12 na 13 mwezi Novemba 2015 kwa muda wa nusu siku pale kwenye hospitali ya Hindu Mandal Dar es Salaam.
Kutokana na takwimu zilizotolewa mwaka 2012, kwa afrika mashariki ndani ya watu milioni 9 kulikuwa na mtaalam mmoja tu wa magonjwa ya mfumo wafahamu. Shirika la afya ulimwenguni (WHO) wanashauri kila nchi iwe na walau mtaalam mmoja wa magonjwa ya fahamu kuhudumia watu 100,000, ila kwa Tanzania wastani ulikuwa 1:13,000,000. Watanzania wengi, hasa maelfu ya watoto, wanafariki kila mwaka kutokana na magonjwa kama kichwa kujaa maji (hydrocephalus), tatizo la kuzaliwa la fuvu (encepheloceles), matatizo ya kichwa yanayoleta shida kwenye uti wa mgongo na magonjwa mengine yanayofanana na hayo.
Kwa sasa Tanzania ina wataalam tisa, ambao saba wanafanyakazi hospitali ya taifa ya muhimbili na wengine wawili wapo hospitali ya rufaa ya Bugando.

Kwa uzoefu wa kutibu zaidi ya wagonjwa 1500 wa kitanzania kwa miaka 10 iliyopita katika sekta ya ubongo na viungio vya uti, Dk. AlokRanjan ni mzoefu mkubwa katika upasuaji wa mfumo wafahamu kwenye hospitali za Apollo zilizopo Hyderabad. Amefanya zaidi operesheni kubwa 5000. Amejikita zaidi katika upasuaji wa uti wa mgongo, uvimbe mdogo katika neva za mifumo ya fahamu katika maeneo ya ubongo, fuvu na uti wa mgongo, upasuaji wa uti wa mgongo kwa watoto, na upasuaji katika ateri. Dk. Alok Ranjan ni mwanachama katika kundi la mabingwa wa upasuaji wa mfumo wafahamu kutoka Hospitali za Apollo na chini ya usimamizi wake ameweza kufanya zaidi ya operesheni 1000 kwa mwaka.

Katika hizo siku 3 za kliniki hiyo, Dk. Alok Ranjana tajikita kwenye maeneo ya msingi yanayohusisha matatizo magumu katika ubongo na mfumo wa uti wa mgongo kwa watoto na watu wazima pia. Upasuaji katika neva za mfumo wa fahamu, upasuaji katika mfumo wa uti wa mgongo, uvimbe, upasuaji mdogo wa mfumo wafahamu kwa upande wa ubongo na uti wa mgongo, upasuaji katika fuvu, upasuaji kwa watoto kwenye viungio vya uti wa mgongo na ateri.

Hii sio ziara ya kwanza kwa daktari huyu mjini Dar es salaam. Huu ni mwendelezo wa ushirikiano na hospitali za Hindu mandal na unadhihirisha ni jinsi gani hospitali za Apollo zimejikita kwenye kutoa huduma bora za afya kwa watanzania wote ambao hawana uwezo/kipato cha kuwawezesha kwenda India kwa ajili ya matibabu.

Huduma hii ya kliniki, ni fursa ya pekee kwa wagonjwa wote wanaosumbuliwa na magonjwa yanayohusisha mfumo wa fahamu na uti wa mgongo, wenye uhitaji wa matibabu na hawana uwezo wa kusafiri kwenda  hospitali za Apollo. Dk. Alok Ranjan atafanya kazi kwa karibu kabisa na timu ya madaktari wa hospitali ya Hindu Mandal kwa kutoa huduma madhubuti na ushauri bora katika afya.
Hivyo watanzania wanashauriwa kuweka miadi mapema na hospitali ya Hindu mandal kupitia mawasiliano haya; +255 22 2114991 - 4.


No comments:

Post a Comment