Na Anna Nkinda – Maelezo, Lindi
VIJANA
wametakiwa kutokubali kutumiwa vibaya na baadhi ya wanasiasa kwa
maslahi ya watu wachache huku hao wanaowatumia wanasonga mbele
kimaendeleo na wao wanazidi kurudi nyuma.
Rai
hiyo imetolewa jana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea
kwa nyakati tofauti na wananchi wa kijiji cha Kikomolela
kilichopo jimbo la Mchinga na mtaa wa Likotwa uliopo Jimbo la Lindi
mjini waliohudhuria kampeni ya kuwanadi wagombea wa nafasi za udiwani,
ubunge na urais kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mama
Kikwete ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM
kupitia wilaya ya Lindi mjini alisema kuna baadhi ya wanasiasa
wanawatumia vijana kufanya vurugu ambazo hazina faida katika
jamii zaidi ya kuleta hasara kwani wanaharibu miundombinu ikiwa ni
pamoja na barabara, majengo na hivyo kurudisha maendeleo nyuma.
Kuhusu
uchaguzi aliwaomba wananchi wote wa maeneo hayo wakiwemo wanachama
wa vyama vya upinzani kuwachagua wagombea wa CCM ambao
watazidi kuwaletea maendeleo kwani Serikali ya CCM imefanya mambo mengi
ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma za afya, elimu, maji
na barabara.
“Siku
ya uchaguzi ikifika chukua kadi yako ya kupigia kura wahi mapema kituoni
kachague viongozi bora utakaoona watakuletea maendeleo na viongozi hawa
wanapatikana ndani ya CCM. Msiogope! siku hiyo kutakuwa na usalama wa
kutosha”, MNEC huyo alisisitiza.
Kwa
upande wake mgombea ubunge wa jimbo la Mchinga Saidi Mtanda alisema
Serikali ya CCM imefanya mambo mengi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na
kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma ya umeme na katika eneo hilo
vijiji 40 kati ya 47 vikiwemo vijiji vya Nangaru na Kitomanga karibu
vitawasha umeme kwa gharama ya shilingi 45,000/=.
Mtanda
alisema, “Nawaomba wenzetu kutoka vyama vya upinzani dumisheni hali ya
Amani na utulivu iliyopo kwani kuna baadhi yenu mnatoa kauli za
kuwatisha wanachama wa CCM kitendo ambacho siyo kizuri”,.
Naye
mgombea Ubunge wa Jimbo la Lindi mjini Kaunje Selemani aliwaomba
wananchi waliohudhuria mkutano huo kumpigia kura ya ndiyo na kuwaahidi
kusimamia Ilani ya uchaguzi ya CCM ambayo itawaletea maendeleo katika
sekta mbalimbali zikiwemo za nishati na madini, kilimo, elimu, afya,
maji, umeme na barabara.
Katika mikutano hiyo jumla ya wanachama watatu walihama kutoka chama cha Wananchi (CUF) na kujiunga na CCM.
Wakati
huo huo akiwa njiani kuelekea kijiji cha Kikomolela msafara wa Mama
Kikwete ulisimama Shule ya Msingi Moka ambapo walimu na wanafunzi
walikuwa wamesimama pembeni ya barabara wakiwa wameshika bango
lililoandikwa SHULE YA MSINGI MOKA TUNAUJUMBE KWA MAMA KIKWETE.
Mwalimu
Mkuu Msaidizi wa shule hiyo Abdala Mkanjima alimuomba Mama Kikwete
ambaye kitaaluma ni Mwalimu awasaidie kufanya wire ring katika shule yao
kwani umeme umepita shuleni hapo.
Mama
Kikwete aliahidi kulishughulikia suala la umeme katika shule hiyo.
Pia aliwaasa wanafunzi wasome kwa bidii ili waweze kujikomboa kimaisha
na kuwa viongozi wazuri hapo baadaye ambao watalisaidia taifa lao na
jamii inayowazunguka.
No comments:
Post a Comment