Matukio /Siasa : CHADEMA Monduli Wasema Wao Wataanza na Elimu - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Wednesday, 7 October 2015

Matukio /Siasa : CHADEMA Monduli Wasema Wao Wataanza na Elimu



Mgombea udiwani monduli mjini kwa Tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Isaac Joseph akihutubia mamia ya wakazi wa mji wa Monduli juzi katika viwanja vya  soko la alhamis  wakati akizindua rasmi kampeni za mgombea huyo.
************
Wagombea Udiwani na Ubunge jimbo la Monduli kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wametaja sekta ya elimu kuwa moja ya vipaumbele watakapofanikiwa kushinda uchaguzi mkuu ujao.

Akihutubia mkutano wa kampeni mjini Monduli juzi, mgombea ubunge kupitia Chadema Julius Kalanga alisema elimu ni msingi wa maendeleo katika sekta zote kwa sababu ndio huzalisha wataalam na watendaji katika miradi yote ya maendeleo.


"Aliyekuwa mbunge wa Monduli, Mheshimiwa Edward Lowassa amefanya makubwa katika sekta ya elimu, siyo tu Monduli, bali eneo lote la jamii ya wafugaji wa Kimaasai ambao kihistoria walionekana kubaki nyuma kieleimu. Nitaendeleza yote," alisema Kalanga


Alitaja vipaumbele vingine kuwa ni afya, miundombinu, mawasiliano, uwezeshaji na uimarishaji wa miradi midogo midogo kupitia vikundi vya ujasiriamali pamoja na uhamasiahaji wa umma kushiriki harakati za maendeleo kwa kupanga, kuchangia, kitekeleza na kusimamia miradi katika maeneo yao.


Kwa upande wake, mgombea udiwani kata ya Monduli mjini, Isack Joseph "Kadogoo" anayetetea nafasi yake aliahidi kuendelea kuwalipia ada wanafunzi wote watakaofauli kuendelea na elimu ya sekondari ndani yakata yake, lakini wazazi au walezi hawana uwezo wa kugharamia elimu yao.


"Tangu niwe diwani mwaka 2010 hadi sasa nimeshawalipia zaidi ya wanafunzi 75 wanaosoma shule mbalimbali za sekondari ndani na nje ya wilaya ya Monduli. Nitaendelea kufanya hivyo," alisema Joseph

Alisema awali alikuwa akitumia fedha zake binafsi kabla ya kuingiza programu hiyo katika mipango ya matumizi ya fedha za maendeleo ya kata ili kuwezesha mradi wa ada kwa wanafunzi kuwa endelevu kwa kila diwani atakayefuata badala ya kubaki jambo lake binafsi.

No comments:

Post a Comment