Kampeni za UKAWA : Taswira mbalimbali za Mikutano ya Mgombea Urais wa CHADEMA, Edward Lowassa Mkoani Geita Leo - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


13 Oct 2015

Kampeni za UKAWA : Taswira mbalimbali za Mikutano ya Mgombea Urais wa CHADEMA, Edward Lowassa Mkoani Geita Leo

Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa akiwahutubia wananchi wa Busanda, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mnadani, Katika Mji wa Katoro, Mkoani Geita leo Oktoba 13, 2015.

Wazee wa Kabila la Wasukuma wa Mkoa wa Geita, waliongozwa na Mzee Petro Manyema (mwenye kipaza sauti) wakimsimika Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, kuwa Kiongozi wa Kabila la Wasukuma, wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mnadani, Katika Mji wa Katoro, Mkoani Geita leo Oktoba 13, 2015.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Busanda kwa tiketi ya Chadema, Alphonce Mawazo, akiwahutubia wananchi wa Busanda, katika Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mnadani, Katika Mji wa Katoro, Mkoani Geita leo Oktoba 13, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa akiwahutubia wananchi wa Mji wa Geita, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Magereza, Mkoani Geita leo Oktoba 13, 2015.

Mwanasiasa Mkongwe nchini, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, akihutubia wananchi, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Magereza, Mjini Geita leo Oktoba 13, 2015.

Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Geita waliokuwa wamefurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Magereza, wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, leo Oktoba 13, 2015.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad