Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo ambaye alimwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara katika maonyesho ya magari akisaini kwenye kitabu cha wageni katika banda la Cheki.co.tz mara baada ya kuwasili katika kiwanja cha Biafra jijini Dar wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya magari na bidhaa shirikishi ya Auto Fest.
Tarehe 19 Mwezi wa septemba 2015 Mtandao wa magari unaoongoza nchini Tanzania Cheki.co.tz umetimiza mwaka mmoja wa utoaji huduma ya kipekee na iliyo salama ya biashara ya kuuza na kununua kwa njia ya mtandao pande zote za Tanzania.
Ndani ya kipindi cha mwaka mmoja wa utendaji wetu, maelfu ya watu wamekuwa wakitembelea tovuti yetu kila siku na maelfu ya magari yamenunuliwa. Msingi wetu wa wateja umeongezeka mara 21% tangu uzinduzi . 90% ya wafanyabiashara wa magari nchini utumia mtandao cheki.co.tz kuuza magari yao na zaidi ya 50 ya majengo ya kuuzia magari nchini yana nembo ya Cheki.co.tz katika sehemu zao
“Nayaweka mafanikio yetu katika mambo mawili: Kwanza, unatokana na urahisi wa kununua, kwani tumewezesha wateja kununua gari wakati wowote, na mahali popote wanapohitaji. Sababu ya pili, ni mahusiano mazuri na wauzaji wa magari uliotokana na ubora wa biashara” alisema Bwana Mori Bencus, Meneja wa Cheki.co.tz nchini Tanzania.
Naye Juliana Ntemo, Msaidizi wa Masoko wa Cheki.co.tz alisema, “ tuna shauku ya kuboresha zaidi huduma yetu kwa miaka ijayo kwa kuendelea kutoa huduma ya uuzaji na ununuzi kwa njia ya mtandao iliyo salama na ya kipekee kabisa”.
Ushuhuda wa kipekee kutoka kwa wateja kwa mwaka 2015
Cheki wameturahisishia biashara, tunapata wateja kutoka nchi nzima.Wateja wanaingia moja kwa moja cheki.co.tz na kuona magari yakiwa na maelezo muhimu,na kama mtu anahitaji anawasiliana nasi- Ramadhani Makame, Planet Motors
Cheki.co.tz ni duka la kimtandao, ambapo wanunuzi wa magari na wauzaji wa Kitanzania hukutana. Ndani ya tovuti hii magari ya kila aina yanapatikana kwa wanunuzi Tanzania nzima huku wauzaji wakipata fursa ya kuuza zaidi.
Tembelea www.Cheki.co.tz
Mfanyakazi wa kampuni ya Cheki.co.tz akitoa maelezo kwa mgeni rasmi Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo (kulia) kuhusu ununuaji na hata kuuza gari kupitia mtandao.
Msaidizi wa Masoko wa Cheki.co.tz, Juliana Ntemo (kushoto) akimkabidhi zawadi mgeni rasmi Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo (kulia) wakati wa ufunguzi wa maonyesho.
Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo akikata keki ya kuadhimisha mwaka mmoja wa kampuni ya kuuza na kununua magari ya Cheki.co.tz. Kushoto ni Meneja wa Cheki.co.tz nchini Tanzania Mori Bencus akiwa na Msaidizi wa Masoko wa Cheki.co.tz, Juliana Ntemo (katikati).
Meneja wa Cheki.co.tz nchini Tanzania Mori Bencus (kushoto) akimlisha keski mgeni rasmi wa maonesho hayo ambaye ni Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo (kulia).
Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo(kulia) akimlisha keki Meneja wa Cheki.co.tz nchini Tanzania Mori Bencus baada ya kampuni ya Cheki.co.tz kutimiza mwaka mmoja.
Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo akimlisha keki Bw. Ally Nchahaga kwa niaba ya watu wote waliofika kwenye ufunguzi huo.
Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo ambaye alimwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara katika maonyesho ya magari akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa maonyesho hayo.
Bw. Ally Nchahaga ambao ni waandaaji wa tamasha la magari Tanzania (Autofest) akizungumza jambo wakati wa ufunguzi huo uliofanyika katika viwanja vya Biafra Jijini Dar.
Mkurugenzi wa CW Net Tanzania, Desmond Andrew(kushoto) akitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo kuhusu matumizi ya modem za CW Net wakati alipitembelea banda hilo.
Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo (kushoto) akitizama modem ya CW Net zinazotengenezwa na watanzania na kutumia laini ya mtandao wowote ndani na nje ya nchi.
Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo akipata maelezo kutoka kwa Bw. Zohail Hassanali (kushoto) kuhusu uzibaji wa pancha kwenye magari na vifaa gani mtu anabidi kuvitumia.
Bw. Athman Hamis ambaye ni mwakilishi wa Auto Mobile akitoa ufafanuzi kwa Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo alipokuwa anatembelea mabanda hayo
Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo ambaye alikuwa ni mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa maonesho hayo akipata ufafanuzi kuhusu uoshaji wa magari kutoka kwa Afisa Mauzo wa KARCHER, Josephine Scarion.
Mfanyakazi wa Kampuni ya TFL Motor Group, Maria C. Sangiwa (wa kwanza kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo kuhusu uuzaji wa magari na hata kufanya service ya magari yote. Katikati ni Khalid Abdallah.
Maonesho ya uendeshaji wa magari yakiendelea katika viwanja vya Biafra jijini Dar. (Picha na Geofrey Adroph wa Pamoja Blog)
No comments:
Post a Comment