Na Woinde Shizza,Arusha
Jiji la Arusha limeendelea kuwa kinara katika mchezo wa
tenisi baada ya wachezaji wake kuibuka kidedea kwa kutwaa ushindi katika umri
tofauti tofauti ,mashindano yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya
Arusha Tenisi gymkhana klabu.
Mashindano hayo yalidhaminiwa na Jubilee tyres ikiwa ni
mwaka wa tatu sasa, yalishirikisha jumla ya wachezaji 90 ambao 28 kati yao ni
wasichana kutoka Dar es salaam gymkhana klabu,Kijitonyama tenisi klabu kutoka
Dar es salaam,Morogoro tenisi klabu, ISM –Moshi campus, AICC klabu –Arusha
pamoja na Arusha tenis gymkhana klabu.
Katika umri wa miaka 6 kwa wasichana Schaefer Swantje kutoka
ISM Moshi campus alifuatiwa na Suhana
Patel kutoka Arusha gymkhana klabu,huku kwa upande wa wavulana wa umri huo Sahil Shah
kutoka ISM moshi campus na kufuatiwa na Yuvraj Sidhu kutoka Arusha gymkhana
klabu.
Wasichana walio na umri wa miaka 8 Asha Ali aliibuka mshindi
na nafasi ya pili kumwendea Bahati Mdee wachezaji wote kutoka klabu ya AICC na
kwa upande wa wavulana mika 8 Johnson Peter alibuka mshindi na kufuatiwa na
Yasin Yusuph wote kutoka klabu ya AICC na kwa wasichana walio na umri wa miaka
10 Vanessa Emmanuel kutoka AICC aliibuka kidedea na kufuatiwa na Caroline
Mwangata wa ISM Moshi campus, huku kwa wavulana miaka hiyo Rashid Abdallah
kutoka Arusha gymkhana klabu na kufuatiwa na Abdumarik Kudra kutoka Morogoro
klabu.
Kwa umri wa miaka 12
wasichana Shana Martin aliongoza na kufuatiwa na Fei Amon wote kutoka Arusha gymkhana klabu na
wavulana Damas Felex na nafasi ya pili kumwendea Benjamini Laurance wote kutoka
AICC ,Huku kwa umri wa miaka 14 kwa wasichana Jackline Kayuga kutoka
kijitonyama Tenisi klabu na nafsi ya pili Anikaa Aggarwal kutoka Arusha Gymkhana klabu na kwa wavulana
wa umri huo Deogratius Felex na kufuatiwa
na Yusufu Laurance wote kutoka AICC.
Jackline Kayuga kutoka
Kijitonyama Tennis klabu alishika nafasi ya kwanzana kufuatiwa Hawa
Yahya kutoka Dar es salaam gymkhana klabu katika umri wa miaka 16 kwa wasichana
na kwa wavulana Omari Sulle
Arusha Gymkhana klabu na kufuatiwa na Hassan Hamisi - AICC Club Arusha.
Kwa upande wa umri wa miaka 18 kwa wasichana hawakuwepo ,na
walicheza wavulana pekee ambapo Emmanuel Mallya- Arusha Gymkhana Club
alifuatiwa na - Frank Menard -Arusha
Gymkhana Club.
Nicholaus Leringa Kocha mkuu
wa klabu ya AGC alisema kuwa
mashindano hayo hufanyika kila mwaka yakiwa na lengo la kuwaimarisha vijana katika dhana nzima
ya kunyanyua vipaji vyao.
No comments:
Post a Comment