Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi
Kida akiingia katika ukumbi wa mkutano hoteli ya Double Tree by Hilton
kwa ajili ya warsha ya vijana na ajira iliyofadhiliwa na Mpango wa
Shirika la Utafiti ya Maendeleo ya Kimataifa kutoka Canada (IDRC) na
kuratibiwa na ESRF.
Na Mwandishi wetu
VIJANA
nchini Tanzania wanatakiwa kujitambua, kuacha kuwa kigeugeu na kufanya
papara ya kupata fedha kama wanataka kuendelea na kufanikiwa kibinafsi
na kiuchumi.
Kauli
hiyo imetolewea jana na Meneja Ajira za Kifundi kwa vijana na Mratibu
Kazi wa Shirika la Kimataifa la Kazi (ILO) Dk. Annmarie Kiaga kwenye
warsha ya wadau wa kitaifa ya kujadili suala la ajira kwa vijana
Tanzania .
Kauli
yake hiyo kwa vijana hao waliojumuika katika hoteli ya DoubleTree by
Hilton, Dar es salaam, ilitokana na tafiti mbalimbali zilizofanyika
nchini ambazo zinaonesha kwamba vijana wengi hawana msimamo wa maisha,
hawana maono, hawana malengo binafsi wala kutambua matarajio.
Amesema:
“ Usipojitambua, leo nikija nikakueleza habari za kuanzisha biashara ya
matofali utachangamkia. Kesho akija mtu mwingine akakueleza kuhusu
uchimbaji wa madini utaacha kutengeneza tofali na kukimbilia
machimboni”.
Akizungumza
kwa ufasaha kabisa kuhusu vijana na ajira, alisema kila mmoja ana
nafasi yake katika kuleta maendeleo yake na taifa na kwamba lazima
kujituma na si kubweteka na kulalamika tu.
Akizungumza
kwa mfano alimzungumzia kijana mmoja Joseph ambaye alikuwa mwadilifu
sana na mwenye kumwamini Mungu. Anasema Kila siku Joseph aliamka asubuhi
na kumuomba Mungu amsaidie aondokane na umaskini alionao.
Alifanyakazi hivyo kwa miaka 30 lakini maombi yake hayakumsaidia kuondokana na umaskini.
Siku
moja, alisema, Mungu alimuona Joseph akiwa na masikitiko makubwa
akamuuliza kulikoni, Joseph akamjibu: “Mungu ni miaka 30 leo tangu
nianzie kukuomba uniwezeshe nishinde bahati nasibu. Mimi nimeishi maisha
yangu kwa uadilifu nawe wajua . Lakini mbona maombi hayatimii?”
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi
Kida akifungua warsha ya vijana na ajira iliyofadhiliwa na Mpango wa
Shirika la Utafiti ya Maendeleo ya Kimataifa kutoka Canada (IDRC).
Kushoto ni Meneja Ajira za Kifundi kwa vijana na Mratibu Kazi wa Shirika
la Kimataifa la Kazi (ILO) Dk. Annmarie Kiaga na kulia ni Kiongozi
Mpango wa Ukuaji na Ajira wa Taasisi wa Mpango wa Shirika la Utafiti ya
Maendeleo ya Kimataifa kutoka Canada (IDRC) Dk. Arjan de Haan.
Naye Mungu akatabsamu akamwambia, Joseph, si ununue tiketi basi?
Dk
Kiaga alisema kwa kuzingatia hadithi yake kila mmoja anatakiwa kufanya
kitu na Joseph alisahau kwamba huwezi kushinda bahati nasibu bila
kununua tiketi.
“Kumbuka
haitoshi kuwa na elimu na ujuzi kama hutaweza kuweka elimu hiyo au
ujuzi ulionao katika vitendo” alisema na kuongeza kuwa Joseph alikuwa
anajua anahaitaji fedha ya kianzio lakini hakuchukua hatua ya kupata
hela hiyo.
Alisema
pamoja na ukweli kuwa asilimia 40 ya watu wasio na ajira duniani ni
vijana, kwa maana ya kwamba kuna vijana wapatao milioni 75 duniani kote
wanatafuta ajira huku vijana wa kike wakiwa na changamoto kubwa zaidi,
ipo shida kubwa ya vijana kukata tamaa.
Aidha alisema kwamba hali ya kukata tamaa imewapeleka vijana kuongezeka katika soko la vijana wanaopata kazi zisizo na staha.
Alisema pamoja na sera zilizopo vijana wanatakiwa kuwa na shauku na kazi na pia kujitambua.
“Vijana
wa siku hizi hawana mitazamo sahihi kuhusu ajira. Kwamba vijana hawana
shauku na kazi na wana mitazamo hasi (ili mradi kazi..mkono uende
kinywani?) . Matokeo yake ni kwamba vijana hawatumii ubunifu wowote
katika kuboresha uwezekano wao wa kupata kazi zenye staha” alisema.
Amesema mtaji unahitaji kujiboreshea seti ya ujuzi katika kutafuta kazi ikiwa ni pamoja na uwezo, uzoefu na elimu.
Meneja Ajira za Kifundi kwa vijana na Mratibu Kazi wa Shirika la Kimataifa la Kazi (ILO) Dk. Annmarie Kiaga akizungumza kwenye warsha ya vijana na ajira iliyofadhiliwa na Mpango wa Shirika la Utafiti ya Maendeleo ya Kimataifa kutoka Canada (IDRC) na kuratibiwa na ESRF.
Alisisitiza
kuwa vijana waliowengi hawajitambui na kujiuliza ‘mimi ni nani’ au
hawana malengo binafsi na matarajio mimi nataka kuwa nani na kusema bila
kuyafanyia kazi mambo hayo mawili ya shauku ya kazi na kujitambua
hakutakuwepo na mabadiliko.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii
(ESRF), Dk Tausi Kida, akifungua warsha hiyo alisema pamoja na taifa
kuwa mstari wa mbele kushughulikia ajira kwa vijana kwa kutunga sera
zilizolenga kukidhi haja ya ajira,ikiwemo Sera ya Taifa ya Maendeleo ya
Vijana ya mwaka 2007, Sera ya Taifa ya Ajira ya mwaka 2008 na na mpango
wa utekelezaji wa sera ya taifa ya ajira kwa vijana iliyo chini ya
mtandao wa ajira unaofadhiliwa na shirika la kazi la Umoja wa Mataifa,
changamoto bado zipo.
Aliwataka washiriki wa warsha hiyo wakiwemo vijana waliofanikiwa kueleza siri za fursa na kujiajiri ili kutoa mwanga kwa wenzao.
Pamoja
na warsha hiyo kutoa nafasi kwa vijana kujadili namna ya kutambua na
kutumia fursa za kuichumi zilizopo nchini, kutoa ujuzi kwa vijana wa
namna ya kuingia katika soko la ajira ikiwa ni pamoja na kujiajiri,
kukuza ujasiriamali na kuendeleza biashara, Dk Kida aliwasihi vijana
kujitafutia riziki yake na kushiriki ipasavyo katika shughuli za
kiuchumi na maendeleo.
Aliwataka kujijengea uwezo wa kufanyakazi pamoja na kubaini na kuzitumia fursa za kiuchumi na kibiashara zilizopo nchini.
Warsha
hiyo iliyofadhiliwa na Mpango wa Shirika la Utafiti ya Maendeleo ya
Kimataifa kutoka Canada (IDRC) ilikutanisha vijana kutoka mikoa
mbalimbali nchini Tanzania na kuwezeshwa kwa sehemu kubwa na Taasisi ya
tamasha ambapo Mkurugenzi wake Mtendaji Richard Mabala alikuwa
Mchokozaji mkuu.
Akiwasilisha
salamu kutoka IDRC, kiongozi Mpango wa ukuaji na ajira wa taasisi hiyo.
Dk Arjan de Haan alisema kwamba taasisi hiyo ya serikali ya Canada
imekuwa ikitoa ushirikiano katika tafiti zilizolenga kuangalia utatuaji
wa tatizo la ajira kwa namna inavyofaa.
Mtafiti Mwandamizi ESRF, Dk. Georgina Ole Saibul akiwasilisha mada katika semina ya vijana na ajira.
Alisema
kwamba kwa kawaida taasisi yake husaidia pale inapoona utafutaji wa
mbinu za kutatua tatizo unashirikisha na wahusika ili kupata suluhu
endelevu ya tatizo husika.
Alisema
ameridhishwa na kuona kwamba warsha hiyo imezingatia kanuni za IDRC za
kutaka kutatua tatizo la ajira kwa kushirikisha vijana wenyewe,
kuangalia na kushauri namna bora ya kukabili tatizo la ajira ambao kwa
sasa ni changamoto kubwa duniani.
Alisema
kwamba ipo haja ya kubadili baadhi ya sera kulingana na mahitaji ya
sasa ili kuwezesha vijana wengi zaidi kuingia katika soko la ajira.
Wakati
wa utambulisho na kuelezea kero zao katika ajira wengi wa vijana
waligusia kuwapo kwa sera ambazo si rafiki zinazotengeneza urasimu
mkubwa katika kusaidiwa.
Ingawa
wengi walisema fursa zipo, walizungumzia kutopata ushirikiano kutoka
kwa wazazi , viongozi na taasisi mbalimbali zinazodai kupambana na
ukosefu wa ajira kwa vijana.
Aidha
vijana wengine walisema kwamba ni kweli kuna mtazamo hasi kwa vijana
hasa kukata tamaa na pia kutaka maendeleo ya kasi huku wakikosa ubunifu.
Joachim
Fanuel kutoka singida Youth Entrepreneurs and Consultants Cooperative
Society (SYECLOS) alisema kwamba ingawa wao wanaendesha miradi ya kuku
wa kienyeji na asali kama fursa zilizopo wanakabiliwa na tatizo la
kukata tamaa kutokana na kuona kwamba inachukua muda mrefu kupata vitu
wanavyotaka.
Aidha
alisema kwamba wamekuwa hawasikilizwi na serikali na taasisi mbalimbali
kwa kuwa hawana mali za kuwakilisha kama dhamana katika mambo
mbalimbali.
Johari
A. Sadik kutoka kampuni inayotengeneza nguo za kitamaduni Binti Africa,
akitoa ushuhuda kwamba vijana wanaweza kama watajitambua katika warsha
ya siku mbili vijana na ajira inayofanyika hoteli ya DoubleTree by
Hilton.
Kijana
Musa Mohammed kutoka Zanzibar alisema kwamba japo wana fursa za
usindikaji wa vyakula, mizizi na matunda wamekuwa na tatizo la ujuzi
katika uchakataji, sera duni zisizojibu mahitaji yao na kuwalinda katika
soko.
Binti
mmoja kutoka Binti Africa Kampuni inayotengeneza nguo za kitamaduni
alisema kwamba kuna shida ya kukata tamaa miongoni mwa vijana lakini pia
hawajali kutafuta taarifa wanazohitaji wakisubiri kutafuniwa.
Vijana
wengine walizungumzia ugumu wa mitaji, ukosefu wa taaluma na mfumo wa
elimu kwuatengeneza kupata ajira katika serikali na taasisi zake.
Mshiriki
Leticia Mango kutoka Kigoma alisema kwamba ipo shida ya vijana wenye
vipaji ambao hawana elimu vijijini kudharaulika na kutothaminiwa kwa
kile kinachoonekana sio wasomi.
Alisema
vijana wasomi wakiunganika na wenye vipaji wanaweza kuwa mbali zaidi na
kusisitiza ipo haja vijana kuwa pamoja kwa maendeleo yao.
Joachim
Fanuel kutoka Singida Youth Entrepreneurs and Consultants Cooperative
Society (SYECCOS) akionesha chupa ya asali kutoka kwa mradi wa kikundi
cha vijana ambao waliamua kujiajiri katika warsha ya vijana na ajira.
Joachim
Fanuel kutoka Singida Youth Entrepreneurs and Consultants Cooperative
Society (SYECCOS) akizungumza na washiriki wa warsha ya vijana na
ajira.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi
Kida (kushoto) akiwa na Kiongozi Mpango wa Ukuaji na Ajira wa Taasisi
wa Mpango wa Shirika la Utafiti ya Maendeleo ya Kimataifa kutoka Canada
(IDRC), Dk. Arjan de Haan wakiwa katika warsha ya vijana na ajira.
Vijana wakishiriki kazi za vikundi kwenye warsha hiyo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi
Kida akiwa katika picha ya pamoja na vijana walioshiriki warsha ya
vijana na ajira hoteli ya Double Tree by Hilton jijini Dar.
No comments:
Post a Comment