Michezo /Kitaifa :Yanga Yaifunga Simba kwa Bao 2 - 0 Katika uwanja wa Taifa ,Jijini Dar - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Sunday, 27 September 2015

Michezo /Kitaifa :Yanga Yaifunga Simba kwa Bao 2 - 0 Katika uwanja wa Taifa ,Jijini Dar


MABINGWA wa soka Tanzania Bara, Yanga ya Dar es Salaam yenye maskani yake mtaa wa Jangwani leo imefuta rasmi uteja wake kwa Simba.

Yanga imefuta uteja huo baada ya kuwachapa watani wao hao wa jadi bao 2-0 katika mchezo wa raundi ya nne ya Ligi kuu ya Soka Tanzania bara uliopigwa leo uwanja wa taifa Dar es Salaam.

Mabao ya Yanga yalifungwa na Hamisi Tambwe kunako dakika ya 44 na kipindi cha kwanza baada ya kumalizia mpira wa Malimi Busungu aliengia muda mfupi kuchukua nafasi ya Simon Msuva.

Katika dakika ya 44 kipindi cha kwanza Hamisi Tambwe anaipatia Yanga goli la kwanza katika kipindi cha kwanza baada ya kumalizia kazi nzuri ya Malimi Busungu aliyeingia baada ya kutolewa nje Simon Msuva. 

Malimi Busungu aliwanyanyua tena mashabiki na wapenzi wa Yanga katika dakika ya 79 alipoiandikia timu yake goli la pili na lakuongoza.

Hadi kipenga cha mwisho cha Mwamuzi Izrael Mkongo Yanga 2 Simba 0.

Michezo mingine iliyochezwa leo matokeo ni:- 
Coastal 0 - 0 Mwadui 
 Prisons 1 - 0 Mgambo 
Kagera 0 - 0 Toto Africans 

No comments:

Post a Comment