Matukio / Msiba Kitaifa : Taswira ya Mwili wa Marehemu Celina Kombani Ulivyowasili Jijini Dar es Salaam - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


27 Sept 2015

Matukio / Msiba Kitaifa : Taswira ya Mwili wa Marehemu Celina Kombani Ulivyowasili Jijini Dar es Salaam


Mwili wa Marehemu Celina O. Kombani umewasili muda huu katika uwanja wa ndege wa kimatifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam. Utaratibu wa msiba unasimamiwa na serikali na ofisi za Bunge. Tutaendelea kuwafahamisha ratiba kila tutapopata taarifa. 
Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani umewasili muda huu Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam
 Familia ya marehemu, viongozi mbalimbali na wananchi wakisubili mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani  ulipowasili jioni hii Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam. Aliyeshikwa bega wa tatu kushoto ni Mume wa Marehemu Mzee Kombani.
 Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani  ukitelemshwa baada ya kuwasili jioni hii Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
  Msafara wa mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani  ukipelekwa kwenye ambulance  baada ya kuwasili jioni hii Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Msafara wa mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani  ukipakiwa  kwenye ambulance  baada ya kuwasili jioni hii Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Spika wa Bunge Mhe Anne Abdallah na viongozi wengine wakiwa Uwanja wa ndege kupokea mwili wa marehemu Kombani. 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad