Muwakilishi
wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchi Kenya Dkt. Custodia Mandlhate
akuitoa hotuba ya ufungua wa semina ya inayohusu namna ya kuimarisha
mawasiliano na utoaji wa taarifa sahihi zinazohusiana na magonjwa ya
mafua makali katika ukanda wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa
siku tatu unaoendelea jijini Nairobi.
Baadhi
ya washiriki wa semina ya inayohusu namna ya kuimarisha mawasiliano na
utoaji wa taarifa sahihi zinazohusiana na magonjwa ya mafua makali
katika ukanda wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa siku tatu
unaoendelea jijini Nairobi.
Muwakilishi
wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchi Kenya Dkt. Custodia Mandlhate
(aliyesimama katikati mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na
washiriki wa semina ya inayohusu namna ya kuimarisha mawasiliano na
utoaji wa taarifa sahihi zinazohusiana na magonjwa ya mafua makali
katika ukanda wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika mara baada ya
ufunguzi wa Semina hiyo.
Nchi
za Afrika zimeaswa kuimarisha mawasiliano katika utoaji wa taarifa
zinazohusiana na magonjwa ya mafua makali yanayosababishwa na virusi vya
influenza ili kuokoa maisha ya watu kwa haraka unapotokea mlipuko wa
magonjwa hayo.
Kauli
hiyo imetolewa na Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini
Kenya Dkt. Custodia Mandlhate alipokuwa akifungua semina ya inayohusu
namna ya kuimarisha mawasiliano na utoaji wa taarifa sahihi
zinazohusiana na magonjwa ya mafua makali katika ukanda wa nchi za
Mashariki na Kusini mwa Afrika, semina hiyo inayoendelea jijini Nairobi.
Mawasiliano
ya haraka wakati wa dharura za kiafya yanahusu ngazi zote kuanzia
kimataifa wakati wa hatari ni yetu sote, ni ya kimataifa, kikanda na
kitaifa, hivyo basi kipaumbele cha WHO ni kuhamasisha watu, mashirika na
serikali kushiriki katika kutoa taarifa na elimu juu ya namna ya kuokoa
maisha ili kuchukua hatua sahihi za kuzuia, kujikinga na kujilinda
dhidi ya vitisho ugonjwa huo” alisema Dkt. Custodia.
Dkt.
Custodia alisema kuwa hatua ya kupata elimu sahihi ya namna ya kujikinga
na magonjwa hayo inatekelezwa kwa kupitia matumizi bora ya mawasiliano
ya umma juu ya afya, ushiriki wa jamii na uhamasishaji wa kijamii kwa
kutumia vyombo vya habari, sera na tafiti zinazofaywa ili kuokoa maisha
ya watu katika eneo husika.
Malengo
ya mkutano huo ni kuwajengea uwezo washiriki ambao utaimarisha
mawasiliano kwa watoa maamuzi muhimu ya kitaifa na kikanda katika
kuimarisha hatua za dharura katika kuzuia, kujikinga na kujilinda dhidi
ya vitisho ugonjwa wa mafua makali.
Malengo
mengine ni pamoja na washiriki kupata uelewa juu ya njia bora za kutoa
taarifa wakati inapotokea hatari ya magonjwa ya mlipuko yanayoweza
kusababisha madhara makubwa ya kiafya ambayo yanahitaji dharura katika
utekelezaji wake pamoja na kuimarisha mitandao ya kikanda ya watoa
maamuzi na watendaji ili kubadilishana uzoefu na utaalamu kupitia nchi
wanazoziwakilisha.
Kwa
upande wake muwakilishi kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
Tanzania Dkt. Vida Makundi alisema kuwa semina hiyo ina manufaa makubwa
kwa taifa hilo kwa kuwa nchi hiyo tayari ina viashiria vya kuapata
yanayotokana na wanyama yakiwemo mafua makali ya ndege na mengine hivyo
hivyo ni vema kujifunza na kuchukua tahadhari ikiwaa ni pamoja na
kuelimisha jamii namna ya kujikinga majanga mbalimbali ya magonjwa na
matukio yanayoathiri afya ya binadamu yanapotokea.
Dkt.
Vida alisisitiza kuwa wataalamu wa afya na sekta nyingine zinzohusika na
afya ya binadamu wakaelewa kuwa ili kufanikisha mawasiliano kwa jamii
hawana budi kushirikiana kwa karibu na wanahabari kutoa habari kwa
jamii ili kuokoa maisha ya watu kwa haraka unapotokea mlipuko wa
magonjwa ambapo kunahitajika kuwepo na uelewa mpana wa kisiasa, kijamii
na kiutamaduni na kuzingatia eneo lililoathiriwa na ugojwa wa mlipuko.
Mkutano
huo unaoendelea Nairobi nchini Kenya unaongozwa na kaulimbiu inayosema
“Okoa maisha na zuia ugonjwa kuenea” unajumisha ya zaidi ya washiriki 65
kutoka nchi 21 zilizopo katika ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika
ambapo washiriki wanatoka katika Wizara za Afya, Habari na Muwakilishi
mmoja wa WHO kutoka nchi anayowakilisha katika ukanda huo.
Nchi
hizo ni pamoja na Tanzania, Uganda, Msumbiji, Malawi, Botswana, Lesotho,
Sudani ya Kusini, Madagaska, Visiwa vya Shelisheli, Comoro, Swaziland,
Rwanda, Mauritius, Eritrea, Namibia, Ethiopia, Afrika Kusini na
Zimbabwe.na Kenya ambayo ni mwenyeji wa semina hiyo.
No comments:
Post a Comment