Rais wa Baraza Kuu la 69 la Umoja wa Mataifa, Bw. Sam Kutesa akigonga
nyundo maalum kuashiria kukamilika kwa Mikutano ya Baraza hilo ambalo
ameliongoza kwa mwaka mzima. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa Ban Ki Moon akiwa mwenye furaha wakati wa kuhitimishwa Baraza
la 69 ambapo alimpongeza Bw. Sam Kutesa kwa kuliongoza Baraza kwa
uhodari uliopelekea kupitishwa kwa maazimio mbalimbali.
Na Mwandishi Maaalum
New York
Mkutano
wa
69 wa Baraza Kuu la Umoja wa
Mataifa, uliokuwa chini ya urais wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda
Bw, Sam Kutesa umefikia ukingoni siku ya jumatatu kwa kupitisha
maamuzi ya kihistoria ambayo pamoja na mambo mengine
yanatoa mwelekeo wa majadiliano kuhusu marekebisho na mageuzi ya Baraza
Kuu la
Usalama la Umoja wa Mataifa.
Maamuzi
hayo
ambayo kwa mara ya kwanza yanaingizwa rasmi katika nyaraka muhimu za
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na yaliyopewa namba A/69/L.92
yalipitishwa
kwa kauli moja na wajumbe kutoka nchi 193 wanaounda Baraza Kuu la
Umoja wa Mataifa.
Maamuzi
hayo
ambayo baadhi ya wazungumzaji waliyapachika jina kama maamuzi ya
Kutessa ikiwa ni ishara
ya kutambua mchango wake katika kusimamia kidete majadiliano kuhusu
mageuzi ya Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa yanatoa msingi
au maandishi ambayo kwayo yatawawezesha nchi wanachama kujadiliana
kwa kupitia maamuzi hayo.
Ingawa
maamuzi
hayo yamepita bila la
kupigiwa kura na kupongezwa kwa kufungua
ukursa mpya katika kuendeleza mchakato wa majadiliano ya mageuzi na
upanuzi wa Baraza Kuu la Usalama, baadhi ya nchi zimeyaelezea
maamuzi hayo kuwa na ni ya kiufunzi zaidi na hivyo yasikuchukuliwe
kama maamuzi ya mwisho kwa
madai kwamba ,maandalizi na majadiliano ya
maamuzi hiyo hayakuwa jumuishi na hivyo hayawakilishi maoni na hisia za
makundi yote.
Akiungana na wazungumzaji wengi waliounga mkono
kupitishwa kwa maamuzi hayo Mwakilishi
wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi
Tuvako
Manoni, amesema , majadiliano yaliyopelekea kupatikana kwa maamuzi
hayo hayakuwa rahisi, lakini yameasisi hatua mpya ya mwendelezo wa
ajenda ya kulifanyia mageuzi Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa
Mataifa ili
liwe jumuishi kuendana mazingira ya
sasa.
Akasema hapana shaka kwamba majadiliano Zaidi yanapashwa kuendelea ili kijibu kiu ya
kila upande na kwamba nchi wanachama wanapashwa kujivunia hatua hiyo
muhimu hataka kama ni hatua ndogo.
Akatumia
fursa hiyo kuwapongeza Bw.Sam Kutesa na Mwakilishi wa kudumu wa Jamaica
Balozi Rattray kwa kazi nzuri , kubwa na
iliyokuwa na changamoto nyingi lakini
iliyofanikisha kupatika kwa maamuzi
hiyo.
Majadiliano
kuhusu namna ya kuboresha na kupanua
wigo wa wajumbe wa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, ni majadiliano yaliyoanza
mwaka 2008 lakini ni katika
Mkutano wa 69 wa Baraza Kuu la Umoja wa Maifa ambapo matokeo ya majadiliano miongoni
mwa wanachama yameweza kupitishwa rasmi katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Muundo
wa sasa wa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo linawajumbe wa kudumu na wenye kura ya turufu watano na
wajumbe 10 wanaoingia kwa mzunguko
wa uwakilishi wa kikanda haujaitendea
haki Afrika bara ambalo licha ya
kwamba asilimia kubwa ya maamuzi
yanayofanywa na Baraza Kuu la Usalama yanaihusu
Afrika lakini Afrika si mwanachama wa
kudumu na hiyvo imekuwa ikipigania kupata
nafasi ya uwakilishi wa kudumu
pamoja na kura ya turufu.
Kumalizika
kwa Mkutano wa 69 wa Baraza Kuu la Umoja
wa Mataifa, kunafungua kuanza kwa
Mkutano wa Baraza Kuu la 70 ambalo kwa mwaka mzima litakuwa chini ya Urais wa
Bw.Monges Lykketoft
No comments:
Post a Comment