Kampeni za UKAWA : Lowassa Awashukuru Wananchi wa Masasi kwa Mapokezi Makubwa Aliyoyapata - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Friday, 25 September 2015

Kampeni za UKAWA : Lowassa Awashukuru Wananchi wa Masasi kwa Mapokezi Makubwa Aliyoyapata

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Masasi, Mkoani Mtwara, waliofikia kusikiliza sera zake katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Boma,  Septemba 22, 2015. Ambapo amewashukuru wananchi wa Mji wa Masasi kwa mapokezi makubwa waliyompatia.
Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye akizungumza machache na wananchi wa Jimbo la Masasi Mjini, Mkoani Mtwara waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Boma, Septemba 22, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwasili kwenye Uwanja wa Boma, Mjini Masasi Mkoani Mtwara, kulikifanyika Mkutano wake wa Kampeni za kuomba ridhaa ya wananchi kugombea nafasi, uliofanyika  Septemba 22, 2015.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI, MASASI.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwapungia mkono wananchi wa Mji wa Masasi, Mkoani Mtwara, muda mfupi baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Boma, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni, Septemba 22, 2015.
Uwanja wa Boma mjini Masasi, palikuwa hapatishi pale Mgombea Urais alipowasili uwanjani hapo.

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akizungumza jambo na Mke wa Mwenyekiti wa Chama cha NLD, Dkt. Emmanuel Makaidi (kulia), Mama Modesta Makaidi, wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Boma, Septemba 22, 2015.
Chademaaaaaa.........
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akipokea karatasi ya Shairi kutoka kwa Msoma Mashairi, Mohamed Ally (kushoto) mara baada ya kughani Shairi lake.
Mgombea wa Ubunge anaekubalika na wananchi wa Masasi kupitia Mwamvuli wa Chama cha Wananchi CUF, Ismail Makombe (Maarufu kwa Jina la Kundambada), akizungumza machache na wananchi hao waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Boma, Septemba 22, 2015.
Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa kupitia Chama cha NLD, Dkt. Emmanuel Makaidi akiwa ameambatana na Mkewe, wakiwasalimia wananchi wa Mji wa Masasi, Mkoani Mtwara Septemba 22, 2015.

Magambo yenye jumbe mbali mbali.
Sehemu ya Wananchi wa Mji wa Masasi, Mkoani Mtwara wakiwa katika Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Boma, Septemba 22, 2015.
Mmoja wa Wazee wa Mji wa Masasi, akiendeleo kuchukua taswira kupitia simu yake, katika Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Boma, Septemba 22, 2015.
Umati wa Wananchi wa Mji wa Masasi, Mkoani Mtwara wakiwa katika Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Boma, Septemba 22, 2015.































No comments:

Post a Comment