Kampeni za CCM : Mgombea Mwenza Samia Suluhu akiwa Mtwara Vijijini - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Thursday, 17 September 2015

Kampeni za CCM : Mgombea Mwenza Samia Suluhu akiwa Mtwara Vijijini

 Wananchi wakimsikiliza Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, alipozungumza na walipozuia msafara wake njiani, katika eneo la Makonga wilayani Newala, wakati akieda kuhutubia mkikutano ya kampeni katika jimbo la Newala Vijijini mkoani Mtwara jana, Septemba 16, 2015.
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimnadi Mgombea Ubunge jimbo la Liwale mjini, George Mkuchika, katika mkutanowa kampeni uliofanyika jana, Septemba 16, 2015, katika jimbo hilo mkoani Mtwara
 Mgombea Ubunge jimbo la Newala Vijijini, Rashid Akbar akiomba kura baada ya kunadiwa na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo hilo, jana Septemba 16, 2015
 Wagombea Udiwani katika jimbo la Newala Vijijini wakionyesha mikono walipotambulishwa na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo hilo leo. Kushoto ni Mjumbe wa kampeni za mgombea mwenza wa Urais Mama Samia, Angela Kizigha.
 Kina Mama wakimpatia zawadi Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Newala Vijijini mkoani Mtwara.
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia akizungumza na wananchi waliozuia msafara wake katika eneo la Chaume, akiwa njiani kwenda jimbo la Liwale Vijijini kuhutubia mkutano wa kampeni jana, septemba 16, 2015
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama samia Suluhu Hassani akihtubia wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Newala mjini mkoani Mtwara.
 Wananchi wakiahidi kuipigia kura CCM, Wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Newala mjini mkoani Mtwara.
 Mbunge anayesubiri kuapishwa baada ya kupita bila kupingwa katika jimbo la Nanyamba, mkoani  Mtwara, Abdallah Chikota, akimuombea Kura mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo hilo.
 Kijana akiwa amejinakshi kuhamasisha mkutano wa kampeni uliofanyika jimbo la Mtwara Vijini.
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, akipokea kadi za vyama vya upinzani baada ya vijana kutoka vyama hivyo kuamua kuhamia CCM wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika jimbo la Mtwara Vijini.
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama samia Suluhu Hassan akimnadi mgombea Ubunge jimbo la Mtwara Vijijini Hawa Ghasia katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo hilo, jana, Septemba 16, 2015. (Picha zote na Bashir Nkoromo).

No comments:

Post a Comment