Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Mhandisi Mussa Natty
wapili (kushoto) akiwakabidhi ufagio Mwenyekiti wa bodi wa Benki ya Covenant Balozi,
Salome Sijaona, wa pili (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Sabetha
Mwambenja wakati Uzinduzi wa kampeni ya kupambana na kipindupindu katika
Manispaa hiyo ambapo benki hiyo imetoa basi kuwatembeza wananchi waliojitolea
kutoa elimu kuhusu ugonjwa wa Kipindupindu na kufanya usafi, kulia ni Mratibu
wa Federation Taifa, Khadija Kingi.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Covenant, Sabetha Mwambenja,
wapili (kushoto) akimkabidhi gari Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Mhandisi
Mussa Natty wapili (kulia) kwaajili ya Wanachama wa Taasisi ya Federation
waliojitolea kutoa elimu elimu ya ugonjwa
wa Kipindupindu na kufanya usafi katika Manispaa hiyo (kulia) Mwenyekiti wa
bodi wa Benki hiyo Balozi, Salome Sijaona na Mratibu wa Federation Taifa, Khadija
Kingi.
Mwenyekiti wa bodi wa Benki ya Covenant Balozi, Salome
Sijaona, kwa Pamoja na Mkurugenzi wa Benki hiyo Sabetha Mwambenja(Kushoto)
wakikabidhi vinywaji kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Mhandisi Mussa
Natty, na Mratibu wa Taasisi ya Federation Taifa Khadija Kingi, Ikiwa ni sehemu
ya kuwezesha kampeni ya kupambana na kipindupindu kwa Manispaa hiyo.
NANE
wafa kwa kipindupindu kinondoni
Dar
es Salaam, 17 Sep 2015... Benki ya Covenant imetoa msaada
wa basi maalumu kwa ajili ya kuwasafirisha wanachama wa taasisi ya Federation
waliojitolea kufanya usafi na kutoa elimu kwa ajli ya kutokomeza ugonjwa wa
kipindupindu katika manispaa ya Kinondoni iliyoko jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Covenant bank, Balozi
Salome Sijaona amesema kuwa benki hiyo imekuwa Msitali wa mbele katika
kuisaidia jamii ya Watanzania wasio katika sekta Rasmi ambao kwa kiasi kikubwa
ndio wanaoishi katika Mazingira magumu na hatarishi.
“Wateja wetu sisi ni wale wa hali ya chini ambao
hawako katika maisha bora, tumejenga misingi yetu katika kuwakuza kiuchumi ila
uchumi bila kuwa na afya njema hauwezi kufikia malengo ndio maana tumeona ni
vyema sasa kuwaaidia kwa kuwawezesha kupata elimu namna ya kupambana na ugonjwa
huo na kuutokomeza kabisa ikiwa ni pamoja na kuweka utaratibu wa kuwa na
matibabu ya uhakika kwa kuwa na Bima za Matibabu” Alisema Balozi Sijaona.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Sabetha
Mwambenja amesema wametoa basi ambalo litatumika kuwafikisha watoaji wa elimu
ya afya maeneo yote ya manispaa ya kinondoni pamoja na vinywaji na mahitaji
mengine kwa wakufunzi hao wa kujitolea ili kuhakikisha Kampeni hiyo inafanikiwa
na kumuahidi Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kuwa watakuwa bega kwa began a manispaa
hiyo katikamutoaji wa huduma za jamii.
Kwa Upande wake, Mratibu wa shughuli wa taasisi ya Federation, Hadija Kingi akaiku benki
na manispaa kwa jitihada kuuwanga mkono
kutokomeza ugonjwa huo.
Awali, mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni Injia Musa
Natty alisema idadi waliokufa kwa
Ugonjwa wa kipindupindu katika manispaa hiyo imefikia wanane, huku wagonjwa
wanaoendelea kutibiwa wakiwa zaidi ya 356.
Alisema ili kuzuia ugonjwa huo, manispaa hiyo
imechukua hatua mbalimbali ikiwamo kuzuia uuzwaji holela wa chakula pamoja na
kutoa agizo maalumu kwa wananchi kuzingatia usafi katika maeneo yao ili
kuendelea kukabiliana na ugonjwa huo ambao bado umeendelea kutesa wakazi wa
maeneo kadhaa.
Mkurugenzi huyo, ametanabaisha hayo wakati
akihitimisha mafunzo na kupokea msaada wa basi maalum na Vitendea kazi
vilivyotolewa na Covenant Bank, vitakavyotumika na wananchi waliojitolea kutoa
elimu na kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Manispaa hiyo ili kutokomeza
Ugonjwa huo .
“Kipindupindu ni Ugonjwa unaosambaa kwa kasi sana,
tumejitahidi kuudhibiti kwa kiasi cha kutosha na ndio maana madhara hayajawa
makubwa sana, pamoja na hilo bado tumekuwa na changamoto kwa kuwafikia wananchi
wengi kulingana na wingi wa watu na ukubwa wa Manispaa yetu, hivyo kwa kuzindua
mpango huu wa kutoa elimu na usafi kwa wananchi kwa kushirikiana na Taasisis ya
Federation na kwa kusaidiwa na Covenant Bank, tunaamini tutaweza kutokomeza
Ugonjwa huu, alisema Mkurugenzi huyo na kuongeza.
“Ugonjwa huu bado upo na sasa tuna wagonjwa zaidi
ya 300 ambao bado wanaendelea kupata matibabu katika kanda maalum, na kesi mpya
bado zimeendelea kupatikana hivyo natoa wito kwa wananchi licha ya kasi
kupungua bado wanahitajika kuendelea kuzingatia usafi na kuepuka kula hovyo
pamoja na kunawa mikono kabla ya kula na kila wanapotoka chooni”
Mkurugenzi huyo aliongeza kwa kuwapongeza
wanachama wa Taasisi ya Federation ambao
watatoa elimu na kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Manispaa kwa kujitolea
na kutoa wito kwa wananchi kuwapokea na
kuwapa ushirikiano ili kuwezesha kutokomeza kabisa Ugonjwa huo.
No comments:
Post a Comment