Balozi
wa China nchini Tanzania Dr.Lu Youqing (katikati) akipata maelekezo
kuhusu bidhaa za Huawei wakati wa mkutano wa watanzania waishio uhaibuni
(Tanzania Diaspora).Kushoto ni Afisa mahusianao na habari,Jimmy na
kulia ni Meneja wa bidhaa na huduma wa Huawei hapa nchini, Joseph Lyimo
Huawei walikua ni wazamini wakuu wa mkutano huo ulifanyika jijini Dar es
salaam katika hoteli ya Serena Augost 14 mwaka huu.
Dr.Lu Youqing lieleza
kuwa sasa hivi China na Tanzania wana ushirikiano mzuri ambapo China
imekuwa ikisaidia ukuaji wa uchumi wa Tanzania kwa kuwawezesha
watanzania waliopo nchini China.
Mbali na hayo wamekuwa wakisaidia Tanzania kwa njia nyingi moja wapo kwa makampuni ya nchi yao kuwekeza nchini Tanzania.
Huawei
ni moja ya kampuni hizo ambapo ina wafanyakazi wengi watanzania na
imekuwa ikisaidia watanzania katika mambo mengi ya kielimu na
kiteknolojia na kupelekea kukuza uchumi wa tanzania.
Huawei
Tanzania walikua moja ya wadhamini wa kongamano hili la siku mbili
ambapo kampuni ya Huawei walionyesha jinsi Kamera za CCTV zinavyofanya
kazi katika lango kuu la kuingilia katika kongamano hilo ambapo kamera
hizo zilionyesha vyema jinsi ya kumwona mtu ambaye anaweza kufanya
uharifu wowote mahali pale.
Pia
Huawei walikuwa na redio za 4G ambazo walikuwa wakizionyesha katika
mabanda kabla na baada ya wanatanzania waishio ughaibuni kuingia na
kutoka kujionea vifaa hivyo vinavyofanya kazi.
China
imekua na ushirikiano mzuri na Tanzania na imetoa kipaumbele
kwakufadhili kongamano la wanaDiaspora nje ya nchi kwa kuwapatia elimu
na vitu vingine.
Mbali na Hapo China imewekeza mambo mbalimbali nchini Tanzania hasa katika Elimu na Teknologia.
Waziri
wa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa,Bernad Membe
amwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho
Kikwete kufungua mkutano uliowakutanisha watanzania waishio ughaibuni
uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Katibu
mkuu wa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa, Balozi
Liberata Mulamula akizingumza na watanzania waishio Ughaibuni,(Diaspora)
kuhusiana na watanzania hao kuwekeza hapa nchini na kupenda kwao katika
mkutano uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya watanzania waishio ughaibuni (Diaspora) wa wizara
ya Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa,Rosemary Jain ambaye
alikuwa mwenyekiti wa mkutano huo uliowakutanisha watanzania waishio
ughaibuni (Diaspora) akizungumza katika mkutano huo uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Msanii
wa nyimbo za bongo freva,Peter Msechu akiwaongoza watanzania waishio
Ughaibuni maarufu kama Diaspora kuimba wimbo wa Taifa katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Watanzania waishio ughaibuni maarufu kama Diaspora wakisikiliza watoa maada hawapo pichania katika mkutano uliowakutanisha uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Meneja
wa sheria wa mamlaka ya uhifadhi katika hifadhi ya Ngorongoro, Julius
akaibebe akiwaasa watanzania waishio ughaibuni kuwekeza hapa nchini hasa
katika buga za wanyama ili kuchangia uchumi wa nchi hapa nchini
aliyasema hayo katika mkutano uliowakutanisha watanzania waishio
ughaibuni(Diaspora) uliofanyika jana na leo katika hoteli ya serena
jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa kampuni ya Choice Coffee.co.tld, Rose Swai akizungumza na
wanadiaspora waishio ughaibuni kuwekeza kwenye viwanda vinavyotengeneza
bidhaa mbalimbali kwa kutengeneza vifaa vya kuhifadhia(Packeging
product) vitu mbalimbali kwa wajasiliamali hapa nchini ili waweze kupata
masoko kwa urahisi aliyasema hayo katika kutano uluiwakutanisha
watazania waishio ughaibuni uliofanyika katika hoteli ya serene jijini
Dar es Salaam.
Waziri
wa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa, Bernad Membe
akiwa katika picha ya pamoja na watanzania waishio ughaibuni (Diaspora)
mara baada ya mapumziko ya mkutano uliowakutanisha watanzania hao
ulifanyika katika hoteli ya serena jijini Dar es Salaam.
(Picha na Avila Kakingo)
(Picha na Avila Kakingo)
No comments:
Post a Comment