Na Teresia Mhagama
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage amefanya ziara ya kukagua
utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini Awamu ya Pili inayotekelezwa
pembeni ya bomba kubwa la gesi katika mkoa wa Mtwara.
Pamoja
na kukagua miradi hiyo inayofadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini
(REA) na kutekelezwa na shirika la Umeme nchini (TANESCO), Naibu Waziri
pia amekagua maendeleo ya kituo cha kuchakata gesi kilichopo kijiji cha
Madimba katika mkoa wa Mtwara.
Katika
ziara hiyo Mwijage ameagiza kuwa vifaa vya umeme vinavyohitajika katika
utekelezaji wa miradi hiyo ya umeme, viwasilishwe ndani ya wakati
uliopangwa ili miradi hiyo itekelezwe kwa ufanisi.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage ( mwenye suti ya bluu,
kulia) akiangalia zoezi la uwekaji nguzo za umeme katika kijiji cha
Sinde B, mkoani MTWARA wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua
utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage ( mwenye suti ya bluu,
kulia) akiangalia zoezi la uwekaji nguzo za umeme katika kijiji cha
Sinde B, mkoani MTWARA wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua
utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (mwenye suti ya bluu )
akisalimiana na wafanyakazi wa kampuni ya Kusambaza Gesi (GASCO) walioko
katika kituo cha kuchakata gesi cha Madimba mkoani Mtwara mara
alipowasili kituoni hapo kukagua mitambo ya kuchakata gesi.Kushoto kwake
ni Kaimu Meneja wa Kampuni ya Kusambaza Gesi (GASCO), Kapuulya Musomba
.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (kushoto) akimsikiliza
mwananchi wa kijiji cha Mnaweni mkoani Mtwara, Bakari Oga ambaye alikuwa
akimweleza Naibu Waziri kuhusu changamoto ya
utekelezaji wa miradi ya umeme kijijini hapo.
Baadhi
ya mitambo ya kuchakata gesi katika kituo cha Madimba mkoani Mtwara.
Gesi asilia itasafishwa katika kituo hicho kabla ya kusafirisha kwa
bomba la Gesi.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (wa tano kushoto mstari wa
mbele ) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya
Kusambaza Gesi (GASCO) walioko katika kituo cha kuchakata gesi cha
Madimba mkoani Mtwara. Kushoto kwa Naibu Waziri ni Mkuu wa wilaya ya
Mtwara, Fatma Ally na kulia kwa Naibu Waziri ni Kaimu Meneja wa Tanesco,
mkoa wa Mtwara, Daniel Kyando na (aliyevaa kizibao cha rangi ya
machungwa) ni Kaimu Meneja wa Kampuni ya Kusambaza Gesi (GASCO),
Kapuulya Musomba .
Naibu
waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage akisaini kitabu cha wageni
katika ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara kabla ya kuanza ziara ya
kukagua miradi ya umeme vijijini mkoani Mtwara.Kushoto ni Katibu Tawala
mkoa wa Mtwara, ALfred Luanda.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage akisaini kitabu cha wageni
mara alipowasili katika kijiji cha Msanga Mkuu mkoani Mtwara, akiwa
katika ziara yake ya kukagua miradi ya umeme vijijini Awamu ya Pili
inayofadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Naibu
waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (wa pili) kushoto
akijadiliana jambo na wataalam wa Wizara ya Nishati na Madini
alioambatana nao katika ziara ya kukagua miradi ya umeme vijijini
inayofadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika mkoa wa
Mtwara.Kutoka kushoto ni Mjiolojia Mkuu, Sebastian Shana, Eng. Robert
Dulle na Eng. Christopher Bitesigirwe.
No comments:
Post a Comment