Na MatukiodaimaBlog
CHAMA Cha
mapinduzi ( CCM) mkoa wa Iringa kimefuta matokeo ya kata tatu za jimbo
la Kilolo matokeo yaliyokuwa yakimpa ushindi mkubwa mbunge anaemaliza
muda wake Prof Peter Msola na kuagiza uchaguzi huo kurudiwa kesho
Matokeo
hayo ambayo yamekataliwa na wagombea wote yanadaiwa kupachikwa katika
vituo vya kata hizo tatu japo hata hivyo hayana uhalisia ukilinganisha
na idadi ya wanachama wa maeneo husika .
Katibu wa
CCM mkoa wa Iringa Bw Hassan Mtenga alisema kuwa kutokana na
dosari mbali mbali ambazo zilijitokeza katika kata hiyo ambazo ni
Nyalumbu , Lugalo na Uhambingeto alisema kilichoonyeshwa ni matokeo
hayo kuwa tofauti na matokeo halisi ambayo mawakala wa wagombea
walikuwa nayo na katika kata hiyo makatibu matawi na kata wa CCM
hahakuweza kupeleka matokeo kwa wakati kwa msimamizi mkuu wa uchaguzi
hadi alipoyafuata na kuona kasoro hiyo .
Katibu
huyo alisema karatasi zilizoonyesha ushindi wa mgombea mmoja Prof
Msolla zilikuwa ni tofauti na karatasi halisi zilizotolewa na chama
hivyo kutokana na utofauti huo wagombea wengine waliweza kugomea
matokeo hayo .
Hata
hivyo mgombea Francis Mkokwa alisema kuwa walishangazwa kuona ghafla
mbunge Prof Msola akiongoza katika vituo vya kata hizo ambazo hata
matokeo Yake hayakusainiwa na mawakala wa wagombea wengine na ndizo kata
ambazo matokeo Yake yalikuwa na utata na wakati wa kampeni mbunge
huyo alikuwa hakubaliki katika maeneo ya kata hizo .
Kwani
walisema kimsingi matokeo halali ya kata zaidi ya 21 Mwamoto ndie
alikuwa akiongoza kwa kura nyingi zaidi kuliko za mgombea mwingine
yeyote huku mbunge anaemaliza muda wake akimfukuza kwa mbali na ajabu
kushangazwa kuona udanganyifu mkubwa katika kura hizo.
Bila
kutaja matokeo hayo alisema walitegemea matokeo ya jumla Mshindi kuwa
Mwamoto ila ilitaka kuwa tofauti kwa ambae hakuongoza ktk vituo kutaka
kuongoza kwa matokeo ya jumla hivyo kulazimika kuchunguza matokeo hayo
na kubaini Wizi huo .
Kwani
katika vituo idadi ya kura ni nyingi kuliko ile ya wanachama na wakazi
wa eneo husika hata kama wana kijiji wote hadi watoto wa mwaka mmoja
wangepiga kura bado kura zilikuwa nyingi kuliko wakazi wa eneo husika
kuwa kosa walilolifanya ni kuongeza idadi ya kura za mbunge Prof Msola
bila kufuta idadi ya kura za Mwamoto ama idadi ya wapiga kura ya jumla
"ukitazama
idadi halisi ya wapiga kura ,kura zilizopigwa na kura zilizoharibika
bado ni vitu viwili tofauti na kufananisha Wizi huo ni sawa na Wizi bila
mahesabu ....lazima chama kuchukua hatua kali kwa katibu wa chama
wilaya na wote waliohusika "
.Mgombea
huyo alisema mbali ya kuwa yeye ni mgombea bado kwa sasa
wameamua kuungana kupinga wizi huo na kuona mshindi wa kweli
anapatikana na sio udanganyifu huo ambao umefanyika.
Kwa
upande wake mgombea Ashrafu Chusi pia alisema katika kata hizo
kumefanyika udanganyifu mkubwa na kuwa kuna mazingira ya rushwa
yalifanyika usiku wa kuamkia siku ya kupiga kura kwa eneo hilo la
mji wa Ilula lenye shida kubwa ya maji watu kupewa rushwa na huduma
ya maji kwa kufungulia bomba za maji kwa kituo kimoja baada ya kingine
na katika vituo hivyo inasemekana walikuwa wakigawa pia kanga na
pesa na pale mbinu hiyo inapobainika walikuwa wakifunga maji kituo
husika na kufungua kituo cha pili.
Bw
Chusi alisema jambo hilo wanaomba vyombo husika kuweza kuchunguza
zaidi ili kuwachukulia hatua wahusika na kuwa hana shaka hata
kidogo kuwa mshindi wao katika mchakato alikuwa ni Mwamoto.
Mwenyekiti
wa CCM kata ya Nyalumbu Bw Bruan Mbululo alisema kuwa kimsingi
wao walikamilisha kazi yao kwa kwenda kukabidhi matokeo kwa katibu
wa CCM wilaya ya Kilolo na kama kuna dalili za udanganyifu wao
hawahusiki japo alisema katika kata yake Prof Msola alishinda ila
hakumbuki ni kwa kura ngapi.
Kamanda
wa taasisi ya kuzuia na kuopambana na rushwa mkoa wa Iringa Yunith
Mmari akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu
alisema kuwa wanaendelea kuchunguza mchakato huo wa kura za maoni
katika kata hizo tatu za jimbo la Kilolo.
No comments:
Post a Comment