Kamanda
Mpinga, akishiriki dua ya pamoja na wachezaji wa timu ya Kamati ya
Amani ya Viongozi wa Dini, baada ya mazoezi yao timu hiyo yanayoendelea
kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya maandalizi ya
mchezo wa kirafiki na timu ya Kamati ya Amani ya Mkoa wa Arusha
unaotarajia kuchezwa mwezi ujao jijini Arusha na ule wa kirafiki kati
yao na timu ya Mabalozi hivi karibuni. Kamanda Mpinga alifika
kuwatembelea wachezaji hao kujionea maendeleo ya mazoezi yao.
Kamanda
Mpiga akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Kamati ya
Amani ya Viongozi wa Dini ya Mkoa wa Dar es Salaam,baada ya mazoezi ya
timu hiyo yaliyofanyika leo asubuhi kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar
es Salaam. Kamanda Mpinga alifika kuwatembelea wachezaji hao kujionea
maendeleo ya mazoezi yao.
5:-
Kamanda Mpinga, akisalimiana na walimu wa timu hiyo, baada ya mazoezi
yao kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, leo asubuhi.
6
hadi 10:- Kamanda Mpinga akisalimiana na wachezaji wa timu hiyo baada
ya mazoezi yao kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, leo
asubuhi.
Mchungaji
wa Kanisa la Penuel Healing Ministry Ubungo Kibangu, Mch. Alphonce
Temba (kulia) akimramba chenga Mchungaji wa Kanisa la KKKT Mashariki ya
Pwania, George Fupe, wakati wa mazoezi yao yaliyofanyika kwenye Uwanja
wa Karume jijini Dar es Salaam, leo asubuhi kwa ajili ya kujiandaa na
michezo kadhaa ya kirafiki kwa ajili ya kuimarisha amani na mshikamano
kwa watanzania.
Ustaadh
Sale (katikati) akimiliki mpira katikati ya mabeki wa timu pinzani,
wakati wa mazoezi ya timu ya Kamati ya Amani ya Viongozi wa dini
yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, leo asubuhi
kwa ajili ya kujiandaa na michezo kadhaa ya kirafiki kwa ajili ya
kuimarisha amani na mshikamano kwa watanzania.
Picha ma www.sufianimafoto.com
No comments:
Post a Comment