|
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira, Mhe. Binilith Mahenge
akiwahutubia wananchi (hawapo pichani) kwa niaba ya Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal wakati
wa tukio la upandaji miti ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 70 ya
Ummoja wa Mataifa lilofanyika katika Kijiji cha Marua, Mkoani
Kilimanjaro. Mhe. Waziri aliwaasa wananchi waliojitokeza na Watanzania
kwa ujumla kulinda na kuhifadhi mazingira |
|
Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wakimsikiliza kwa makini Mhe. Waziri Mahenge (hayupo pichani). |
|
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, naye
akizungumza katika maadhimisho hayo. |
|
Balozi
wa Ummoja wa Ulaya nchini, Mhe. Filiberto Sebregondi aye alipata fursa
ya kuzungumza katika maadhimisho hayo na kuwapongeza wananchi wa mkoa
wa Kilimanjaro kwa kutunza mazingira |
|
Juu ni wananchi wa kijiji cha Marua waliojitokeza kwenye maadhimisho hayo |
|
Mkuu
wa Wilaya ya Moshi Mjini, Bw. Novatus Makunga akizungumza kwa niaba ya
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro wakati wa tukio la upandaji miti ikiwa ni
Maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa |
|
Sehemu
nyingine ya wananchi wakifuatilia hotuba mbalimbali zilizokuwa
zikitolewa na viongozi mbalimbali waliohudhuria maadhimisho hayo (hawapo
pichani) |
|
Mhe.
Waziri Mahenge (mwenye koti la kijivu) akikata utepe kuashiria uzinduzi
wa upandaji miti rasmi (wapili kushoto mstari wa mbele) ni Mhe. Alvaro
pamoja na Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa nchini. |
|
Mhe.
Waziri akipanda mti kuzindua zoezi la upandaji miti katika Vijiji vya
Marua na Rua vilivyopo pembezoni mwa Mlima Kilimanjaro |
|
Mhe. Alvaro naye akipanda Mti wake kwenye maadhimisho hayo |
|
Mhe. Waziri (katikati mstari wa Mbele) pamoja na viongozi wengine wakipanda miti kwa pamoja. |
|
Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Celestene Mushy akiwa katika zoezi la kupanda Mti |
|
Mkurugenzi
Msaidizi katika Idara ya Afrika, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa, Bw. Omar Mjenga naye akishiriki zoezi la kupanda miti |
|
Burudani za ngoma mbalimbali zilitolewa na Wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Marangu |
|
Viongozi waliopo meza kuu wakiwapongeza kwa kuwapigia makofi kikundi hicho cha ngoma (hakipo pichani). |
|
Burudani zikiendelea |
|
Mhe. Waziri akizindua Jiwe la Msingi katika maadhimisho hayo |
|
Maafisa Mambo ya Nje nao walishiriki kikamilifu katika maadhimisho hayo |
|
Mhe.
Waziri Mahenge akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi Mbalimbali
wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini pia Watendaji mbalimbali kutoka
Serikalini na Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini |
|
Picha ya Pamoja |
|
Balozi
Mushy (kushoto) wakimsikiliza Balozi wa Ireland nchini Mhe. Fionnuala
Gilsenan (katikati), kulia ni Babozi Juma Halfan Mpango |
|
Balozi
Mpango akiwa na Bw. Omar Mjenga, Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya
Afrika, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. |
|
Balozi
Mushy akijibu moja ya maswali aliyoulizwa na Bw. Pascal Mayala wakati
Viongozi hao walipozungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya
miaka 70 ya Umoja wa Mataifa |
============================================
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mohamed Gharib
Bilal amewaasa Watanzania hususan wakazi wa eneo la Hifadhi ya Mlima
Kilimanjaro kufanya jitihada za makusudi kutunza maeneo yanayozunguka
Mlima huo ili uendelee kuwa kivutio kikubwa cha utalii nchini kwa ajili
ya maendeleo yao na kwa Taifa kwa ujumla.
Hayo
yamesemwa kwa niaba yake na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa
Rais-Mazingira, Mhe. Binilith Mahenge (Mb.) alipowasilisha hotuba wakati
wa tukio la upandaji miti ambalo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa lililofanyika leo katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, Kijiji cha Marua, Mkoani Kilimanjaro.
Mhe.
Bilal alisema kuwa, Mlima Kilimanjaro ambao ni mrefu zaidi Afrika,
unaosimama peke yake na wenye barafu kwa mwaka mzima pamoja na kwamba
hali ya hewa ya Tanzania ni joto sana ni moja ya vivutio vikubwa vya
utalii ambavyo vinachangia kwenye pato la taifa na hata kipato cha
mwananchi mmoja mmoja kwa Kilimanjaro na maeneo yanayozunguka mkoa huo.
“Nawaasa
wazee wangu na wakazi wote wa Kilimanjaro kuwa na jitihada za makusudi
kutunza maeneo yanayozunguka mlima huu na tusisubiri watu kutoka Dar es
Salaam na maeneo mengine ya mbali kufanya kazi hiyo”, ilisisitiza sehemu
ya hotuba ya Dkt. Bilal.
Akizungumzia
matukio kuelekea maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa ambayo
yatafikia kilele tarehe 24 Oktoba mwaka huu, Mhe. Bilal alipongeza na
kuwashukuru waandaji wa shughuli hiyo wakiongozwa na Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Timu ya Umoja wa Mataifa hapa nchini na
TANAPA kwa kuwekea msisitizo umuhimu wa kulinda na kutunza mazingira.
Aliongeza kuwa
japo hapo awali, Umoja wa Mataifa uliundwa kutokana na vita na mapigano
yaliyojitokeza duniani miaka ya nyuma anafarijika kuona Umoja huo kwa
sasa umebadilika na umekuwa ni chombo cha kupigania na kutetea haki za
binadamu na utunzajia wa mazingira.
“Nichukue
fursa hii kupongeza Kaulimbiu ya Maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa
Mataifa inayosema “Umoja wa Mataifa wenye Nguvu, Dunia Bora” na ile
kaulimbiu yetu ya hapa nchini inayosema:”Dunia Moja Watu Bilioni Saba;
Kutunza Mazingira ni Wajibu Wetu”. Hivyo ni wajibu wa kila mmoja wetu
kutunza mazingira ili kuhakikisha watu hao bilioni saba hawaangamii,”
alisema Mhe. Dkt. Bilal.
Mhe.
Dkt. Bilal aliongeza kusema kuwa, wakati umoja wa Mataifa ukiadhimisha
miaka 70 mwaka huu, pia utakuwa na matukio mengine matatu makubwa ambayo
ni kuhitimisha utekelezajii wa
Malengo ya Milenia, Kupitishwa kwa agenda mpya ya Maendeleo Endelevu
baada ya mwaka 2015 na kupitishwa kwa mkataba mpya wa Mambadiliko ya
Tabianchi utakaorithi Itifaki ya sasa ya Kyoto.
Awali
akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Leonidas
Gama, Mkuu wa Wilaya ya Moshi Vijijini, Mhe. Novatus Makunga alisema
kuwa Mkoa huo umejitahidi kuchukua hatua mbalimbali za kukabiliana na
uharibifu wa mazingira ya Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro ikiwemo kusitisha
vibali vya uvunaji wa miti ya mbao na kuni; kuhimiza matumizi ya
nishati mbabadala kwenye taasisi za shule, vyuo na magereza; kuhamasisha
wananchi kupanda miti kwenye vyanzo vya maji pamoja na kuhifadhi misitu
ya asili.”Tunapongeza Taasisi zote zilizoamua kuchagua Mkoa wetu kwa
maadhimisho haya ya upandaji miti kwani yameongeza uelewa na ari kwa
wananchi kuwa utunzaji mazingira ni jukumu la kila mmoja wetu”, alisema
Mhe. Gama.
Naye
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez
alisema kuwa Umoja wa Mataifa unajivunia miaka 70 ya mafanikio katika
kukabiliana na changmoto mbalimbali zinazoikabili duniani kama vita,
uharibifu wa mazingira, ukiukwaji wa haki za binadamu na kwamba maadhimisho hayo ni fursa ya kutathmini mafanikio hayo na kuongeza juhudi zaidi katika kukabiliana na changamoto hizo ili kuzimaliza kabisa.
Aliongeza
kuwa Umoja huo utaendelea kushirikiana kwa karibu na Tanzania ili
kuiwezesha kufikia malengo ya maendeleo na kutoa wito kwa Serikali
kuridhia Malengo mapya ya maendeleo endelevu.
Kwa
upande wake Kiongozi wa Mabalozi wa Umoja wa Ulaya nchini, Mhe.
Filberto Ceriani Sebregondi alisema kuwa Umoja huo utaendelea kusaidia
miradi mbalimbali ya maendeleo nchini ikiwemo ile ya utunzaji misitu,
maji na kilimo pamoja na kuimarisha wakala mbalimbali za taifa ili kweza
kukabiliana na Mabadiliko ya tabianchi.
Tukio
hilo la upandaji miti ambalo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya
Umoja wa Mataifa ambayo yatafikia kilele tarehe 24 Oktoba, 2015,
lilihudhuriwa na Watendaji kutoka Serikalini akiwemo Mkurugenzi wa Idara
ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy, Mabalozi na
Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa na Wananchi.
No comments:
Post a Comment