Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Bi. Fionnuala Gilsenan, akizungumzia kuhusu ufadhili kwa Watanzania wanaokwenda vyuo mbalimbali vya ndani na nje ya nchi. Sherehe hizo zimefanyika Alhamisi, Agosti 20, 2015 kwenye ofisi za ubalozi huo Masaki jijini Dar es Salaam. (Picha na habari na Daniel Mbega wa www.brotherdanny.com)
Baadhi ya wanufaika wa ufadhili huo wakimsikiliza Balozi wa Ireland (hayuko pichani).
Baadhi ya wafanyakazi na wageni waalikwa wakimsikiliza Balozi Gilsenan.
Deogratias Gabriel Rugarabamu, Ofisa Tabibu wa Wilaya ya Kilindi, akipokea cheti cha shukrani baada ya kuhitimu shahada ya uzamili ya Medical Entomology and Clinical Parasitology katika Chuo Kikuu cha Tumaini, KCMC .
Balozi Fionnuala Gilsenan wa Ireland akimpongeza Rubea Mohammed Ali, Mkuu wa Idara katika Wizara ya Kilimo na Maliasili, Zanzibar baada ya kuhitimu shahada ya uzamili katika Chuo Kikuu cha Sokoine katika Elimu ya Kilimo na Ushauri (Agricultural Education and Extension).
David Eliatosha Lekei, Ofisa Kilimo Wilaya ya Hai akipokea cheti cha shukrani kutoka kwa Balozi wa Ireland nchini, Bi.Fionnuala Gilsenan baada ya kuhitimu shahada ya uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine katika Elimu ya Kilimo na Ushauri (Agricultural Education and Extension).
Mshereheshaji akisoma majina ya wanufaika.
Stella Zakayo Munisi, Meneja Rasilimali Watu na Utawala wa Shirika la Sikika, akipokea hati ya ufadhili kwenda kusomea shahada ya uzamili kuhusu Organizational Development and Change katika Chuo Kikuu cha Dublin, Ireland.
Na Daniel Mbega
SERIKALI
ya Ireland kupitia Ubalozi wake nchini Tanzania, leo Agosti 20, 2015 imekabidhi scholarship
kwa Watanzania 14 ambao watakwenda kusomea kozi mbalimbali za shahada ya
uzamili (masters) ambapo wanne kati yao wakienda kusoma vyuo vikuu nchini
Ireland.
Akikabidhi
hati hizo za ufadhili wa masomo, Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Bi. Fionnuala
Gilsenan, alisema utaratibu wa kutoa ufadhili kwa wataalamu mbalimbali ni jambo
la msingi kutokana na ukweli kwamba ujuzi watakaoupata unaweza kuliletea taifa
maendeleo.
“Ufadhili
huu ni sehemu ya Mpango wa Mafunzo wa Kila Mwaka (Fellowship Training
Programme), katika sukuma mbele maendeleo ya nchi washirika wetu, tunadhani
tunao wajibu wa kusaidia pia kuwaelimisha watalaamu wao,” alisema.
Aliwataja wanufaika
wanne waliobahatika kwenda ng’ambo kuwa ni Stella Zakayo Munisi, Meneja
Rasilimali Watu na Utawala wa Shirika la Sikika, ambaye anakwenda kusomea
shahada ya uzamili (Organizational Development and Change) na Cosmas Joseph
Mworia, Ofisa Ushirika na Ofisa Ufuatiliaji na Ukadiriaji katika Kilimo wa
Halmashauri ya Wilaya Kondoa anayekwenda kusomea shahada ya uzamili katika
Kilimo Endelevu na Maendeleo Vijijini (Sustainable Agriculture and Rural
Development). Wawili hao wanakwenda katika Chuo Kikuu cha Dublin.
Flavian
Majenga Lihwa, Mratibu Programu ya Elimu wa Shirika la Care Tanzania yeye
anakwenda Chuo Kikuu cha Dublin Institute of Technology kuchukua shahada ya
uzamili katika Maendeleo Endelevu (Sustainable Development) na Zabron Elias
Masatu, Mganga Mkuu wa Wilaya (DMO) ya Misenyi yeye anakwenda Chuo Kikuu cha
Taifa cha Ireland Maynooth (NUIM) kuchukua shahada ya uzamili ya Immunolojia na
Afya (Immunology and Global Health).
Wanufaika
wengine 10 wa mwaka huu, kozi na vyuo wanavyokwenda vikiwa kwenye mabano ni, Siwajibu
Ally Selemani Malenge, Kaimu Ofisa Kilimo/Umwagiliaji na Ushirika wa Wilaya ya
Kigoma (Chuo Kikuu cha Sokoine – Elimu ya Kilimo na Ushauri ‘Agricultural
Education and Extension’); Edita Byangwamu Rutatora Kokwijuka, Ofisa Kilimo
Daraja la Kwanza kutoka Wilaya ya Muheza (Chuo Kikuu cha Sokoine – Kilimo); Doreen
Elias Mangesho, Mhasibu Mkuu wa CCBRT (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam – Utawala wa
Fedha); Elinlaa Michael Kivaya, Mchumi wa Kilimo wa Wilaya ya Ngorongoro (Chuo
Kikuu cha Sokoine – Kilimo na Uchumi Mtambuka ‘Agriculture and Applied Economics’);
na Joshua Julius Musimu, Mkufunzi wa Kilimo Daraja la Pili kutoka Wizara ya
Kilimo, Chakula na Ushirika (Chuo Kikuu cha Sokoine – Uchumi wa Kilimo ‘Agricultural
Economics’).
Wengine ni
Fredrick Pius Massawe, Ofisa Kilimo Daraja la Kwanza kutoka Ofisi ya Katibu
Tawala Mkoa wa Kilimanjaro (Chuo Kikuu cha Sokoine –Kilimo); Samuel Korinja
Olekao, Mratibu wa Kinnapa Development Programme (Chuo Kikuu cha Sokoine – Utunzaji
wa Maliasili na Kilimo Endelevu); Eva Emmanuel Mbambale, Ofisa Program wa
Sikika (Chuo Kikuu cha Makerere,Uganda – Afya ya Jamii); Iddi Alfani Shekabugi,
Mchumi Daraja la Kwanza katika Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika (Chuo
Kikuu cha Mzumbe – Uchumi na Fedha kwa Maendeleo); na Felix Lyope Lubuga, Ofisa
Utafiti wa Taasisi ya Afya Ifakara (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam – Afya ya
Jamii).
Awali,
Balozi Fionnuala aliwatunuku vyeti wanufaika wengine 10 waliomaliza mwaka 2013
na 2014 katika fani mbalimbali.
Hao ni
Deogratias Gabriel Rugarabamu, Ofisa Tabibu wa Wilaya ya Kilindi (Chuo Kikuu
cha Tumaini, KCMC – Medical Entomology and Clinical Parasitology); Pudensiana Clement Panga, Ofisa Uvuvi kutoka
Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi (Chuo Kikuu cha Sokoine – Sayansi ya
Chakula); Fatma Ally Mwasola Libaba, Ofisa Utafiti (Lishe) kutoka Taasisi ya
Chakula na Lishe (Chuo Kikuu cha Sokoine – lishe ya Binadamu); Rubea Mohammed
Ali, Mkuu wa Idara katika Wizara ya Kilimo na Maliasili, Zanzibar (Chuo Kikuu
cha Sokoine – Elimu ya Kilimo na Ushauri ‘Agricultural Education and Extension’);
na David Eliatosha Lekei, Ofisa Kilimo Wilaya ya Hai (Chuo Kikuu cha Sokoine –
Elimu ya Kilimo na Ushauri ‘Agricultural Education and Extension’).
Wengine waliohitimu
mwaka 2014 ni John Nobert Kirway, Mkufunzi Mkuu wa Mifugo wa Wizara ya Mifugo
na Maendeleo ya Uvuvi, Arusha (Chuo Kikuu cha Sokoine –Tropical Animal
Production); Teddy Frederick Dionis Mamboleo, Ofisa Utafiti (Lishe) kutoka
Taasisi ya Chakula na Lishe (Chuo Kikuu cha Sokoine – Lishe ya Binadamu); Adam
Khamis Haji, Ofisa Mipango na Utawala, Wizara ya Kilimo na Maliasili, Zanzibar (Chuo
Kikuu cha Sokoine – Maendeleo Vijijini); Jacob Polycarp Ngowi, Mkufunzi wa
Masuala ya Mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi (Chuo Kikuu cha
Sokoine –Tropical Animal Production); na Mussa Said Bakari, Meneja wa Maeneo
Tengefu – Pemba kutoka Wizara ya Kilimo na Maliasili, Zanzibar (Chuo Kikuu cha
Sokoine – Utunzaji wa Maliasili na Kilimo Endelevu).
Mpango huo
wa Mafunzo wa kila Mwaka unahusisha Mfuko wa Misaada wa Ireland (Irish Aid)
kupitia program ya maendeleo ya Ubalozi huo nchini Tanzania.
Wanufaika
wa mpango huo wameteuliwa na washirika wa maendeleo wa Ireland nchini Tanzania,
zikiwemo wizara mbalimbali za Serikali, halmashauri za wilaya na mashirika
yasiyo ya kiserikali, ambayo shughuli zao zinawiana na maeneo ya vipaumbele vya
Irish Aid, hususan Kilimo, Afya, Lishe na Utawala.
Aidha,
wanufaika wote ni watendaji wa kati ambao baada ya kuhitimu masomo yao
watarejea kwenye mashirika na taasisi zao kutumia ujuzi walioupata kwa manufaa
ya jamii.
“Kwa
wanufaika watakaokwenda kusoma nchini Ireland, program inatoa fursa nzuri ya
kujifunza katika hadhi ya kimataifa na kunufaika na hazina kubwa ya nyenzo za
tafiti zinazotolewa kwenye Vyuo Vikuu na Taasisi za Teknolojia za Ireland,” amesisitiza
Balozi Fionnuala.
Akaongeza:
“Inatarajiwa kwamba mafunzo ya wataalamu hawa yatachangia kwa kiasi kikubwa
maendeleo ya Tanzania, na kuendelea kuimarisha ushirika wa kielimu baina ya
Ireland na Tanzania.”
Ireland,
kupitia Mfuko wa Misaada (Irish Aid), imekuwa ikidhamini Mpango huo wa Mafunzo
nchini Tanzania kwa miaka 40 sasa ambapo program hiyo imekuwa msingi wa msaada
katika kuzijengea uwezo nchi zinazoendelea na inaendana na mkakati wa kupunguza
umaskini wa nchi washirika wa Ireland, hasa lengo likiwa kuwapatia wataalamu
elimu ya juu ili waendeleze taasisi zao.
No comments:
Post a Comment