Mwenyekiti Msaidizi wa Tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015 litakaloipigia kampeni CCM, Wema Sepetu akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam juu ya tamasha na kampeni zao. Kutoka kulia ni Wellu Sengo (Matilda). Mwenyekiti Msaidizi wa Tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015 litakaloipigia kampeni CCM, Wema Sepetu akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam juu ya tamasha na kampeni zao. Kulia ni Yobnesh Yusuph (Batuli) na kushoto ni Steve Mengele a.k.a Steve Nyerere wakiwa katika mkutano huo. Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mratibu wa Tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015 litakaloipigia kampeni CCM, Steve Mengele a.k.a Steve Nyerere akizungumza na waandishi wa habari leo juu ya tamasha hilo. Mwenyekiti Msaidizi wa Tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015 litakaloipigia kampeni CCM, Wema Sepetu (kulia) akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam juu ya tamasha na kampeni zao. Kutoka kulia ni Wellu Sengo (Matilda) na Yobnesh Yusuph (Batuli). Mwenyekiti Msaidizi wa Tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015 litakaloipigia kampeni CCM, Wema Sepetu akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam juu ya tamasha na kampeni zao. Kulia ni Yobnesh Yusuph (Batuli) na kushoto ni Steve Mengele a.k.a Steve Nyerere wakiwa katika mkutano huo. Baadhi ya wasanii na makada wa CCM ambao watajumuika katika tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015 litakaloipigia kampeni CCM wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mkutano na waandishi wa habari. Baadhi wa aandishi wa habari wakiwasikiliza wasanii hao na waratibu wa tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015.
WASANII
ambao ni makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameandaa Tamasha kubwa
kuzunguka nchi nzima kwa pamoja na kukinadi chama hicho tawala pamoja na
Sera zake ili kiweze kushinda Uchaguzi Mkuu onaotarajia kufanyika
Oktoba Mwaka huu (2015).
Tamasha
hilo litakalojulikana kama "MAMA ONGEA NA MWANAO 2015" limeandaliwa na
baadhi ya wasanii makada wa CCM wapatao 250 ambao watazunguka mikoa
zaidi ya 10 kukipigia kampeni chama hicho tawala ili kiweze kupewa
ridhaa tena na Wananchi ya kuendelea kuongoza nchi.
Akizungumza
leo jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari Mwenyekiti Msaidizi wa
tamasha hilo, Wema Sepetu alisema madhumuni ya tamasha la Mama Ongea na
Mwanao 2015 ni kulinda mazuri yote yalioasisiwa na CCM kupitia viongozi
wake akiwemo Baba wa Taifa Mwalimu Julias Nyerere na Sheikh Abeid Aman
Karume.
Msanii Sepetu akiyataja masuala hayo yalioasisiwa na CCM kupitia
viongozi hao kuwa ni pamoja na amani na utulivu uliopo hadi sasa,
maendeleo ya kijamii na kiuchumi yalioletwa hadi sasa, masuala ambayo
yanastahili kuendelezwa na wala si kubezwa.
Tamasha
hilo linajumuisha wasanii kama Odama, Davina, Wastara Juma, Keisha,
Wellu Sengo (Matilda), Bi. Mwenda, Mama Lolaa, Mama Nyamayao, Herieth
Chumila, Thea, Maya, Chuchu Hans, Steve Nyerere pamoja na wasanii
wengine wengi.
Aidha alisema kupitia tamasha hilo wasanii hao pamoja na wenzao
watazunguka katika mikoa zaidi ya 10 kwa pamoja kufanya kampeni kumnadi
mgombea wa urais kupitia CCM, Dk. John Pombe Magufuli, mgombea Mwenza,
Samia Hassan Suluhu pamoja na viongozi wengine ngazi mbalimbali
wanazogombea kupitia chama cha Mapinduzi.
Madhumuni
ya tamasha la Mama Ongea na Mwanao 2015 ni kulinda mazuri yote
yalioasisiwa na CCM kupitia viongozi wake akiwemo Baba wa Taifa Mwalimu
Julias Nyerere na Sheikh Abeid Aman Karume ambayo bila amani mama awezi
kujifungua salama, Bila mama hakuna familia, amani inapotoweka mama
hawezi kukimbia kilometa kadhaa na kuiacha familia yake, bila mama
hakuna ujasiliamali, mama ni kimbilio la baba, kaka, dada na
watoto...ikumbukwe kuwa mama ndio mpiga kura ndio maana tunasema mama
ongea na mwanao," alisema Wema Sepetu.
"Na
leo hii kuanzia sasa tunatambulisha kampeni yetu tunayoifanya
kuhamasisha vijana, kinamama, kinababa, mashabiki wetu wale wote wenye
sifa za kupiga kura wapige kura kwa kumchagua kiongozi bora anayetoka
Chama Cha Mapinduzi...chagua Dk. Magufuli, Samia Suluhu, wabunge na
madiwani wa Chama Cha Mapinduzi," alisema Sepetu.
Aidha wasanii hao wamempongeza Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete kwa kuongoza vizuri vikao vyote vya
chama hicho hadi kupatikana kwa mgombea bora wa urais kupitia chama
hicho (Dk. Magufuli), hivyo kuwataka wanaCCM wote ambao waligombea na
hawakupata nafasi kuungana na kukitumikia chama.
"...Mimi
Wema Abraham Sepetu nikiwa na baadhi ya wasanii wenzangu ambao
tuligombea tunasema muda bado tunao na siku tunazo kwa kukitumikia chama
tukipewa ridhaa kwa njia yoyote na kwa nafasi yoyote ndio maana hatuja
teteleka tupo imara kuwatumikia wananchi katika nafasi nyingine ndani ya
CCM," alisema Sepetu.
Imeandaliwa na www.thehabari.com
No comments:
Post a Comment