Mwenyekiti wa chadema Mkoa wa Arusha Amani Golugwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya mapokezi ya mgombea Urais Edward Lowassa kupitia CHADEMA yamekamilika kwa asilimia miamoja na tukio hilo kuliita la kiistoria ambalo litafanyika katika viwanja vya tindigani kata ya kimandolu jijini Arusha siku ya jumamosi.(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Mwenyekit wa CHADEMA Wilaya ya Arusha Magoma Derick Magoma akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema magari zaidi ya 75 yameshaandaliwa kwaajili ya msafara wa mgombea wao Lowassa
Naibu katibu mkuu waTimu Lowassa for president Ndama Jeuri akizungumza na waandishi wa habari juu ya ujio wa Lowassa
Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha kupitia chama cha CUF Salussingo Omari akizungumza na vyombo vya habari
Waziri
mkuu mstaafu Edward Lowassa ambaye ni mgombea Urais kupitia chama cha
demokrasia na maendeleo (CHADEMA)anatarajiwa kupokelewa kwa mapokezi
makubwa ikiwemo magari,pikipiki,katika uwanja wa ndege wa kia
hadi viwanja vya tindigani kata ya kimandolu jijini Arusha siku ya
jumamosi(kesho tarehe 15) ambapo atahutubia wananchi katika mkutano
ulioandaliwa na chama hicho
Akizungumza
mapema jana na waandishi wa habari katika ofisi za chama hicho juu ya
maandalizi hayo Mwenyekiti wa chadema Mkoa wa Arusha Amani Golugwa
alisema kuwa mapokezi hayo yamekamilika kwa asilimia miamoja na
tukiohilo ni la kihistoria
Alisema kuwa lengo la ujio huo ni kumtambulisha mgombea urais ambaye ataambatana na mgombea mwenza Juma Duni Hajji ,kwa kuwatambulisha kwa wananchi wa Mkoa wa Arusha sambamba na kupata udhamini wa wananchama waliojiandikisha kupiga kura
Pia alisema kuwa zoezi la udhamini umeshaanza Arusha na uongozi wa Tume umaelekeza mgombea kupata wadhamini 300 na jimbo la Moshi mjini wataoa wadhamini 300
Aidha
aliwataka ,wakazi wa jijili la Arusha na waliopo jirani kujitokeza kwa
wingi katika tukiohilo la kihistoria ambapo pia viongozi wakuu wa chama
hicho watahudhuria akiwemo Mwenyekiti wa Taifa Freeman Mbowe,wenyeviti
wenza wa ukawa kutoka NLD,NCCR pamoja na chama cha CUF,John Mnyika ,Nibu
katibu mkuuZanzibar Salum Mwalimu na viongozi wengine wengi
“Kwakushirikiana
na jeshi la polisi pamoja na vikosi vyetu suala la Amani,Utulivu,Ulinzi
na Usalama vitadumishwa katika msafara huo pamoja na mkutano
huo”Alisema Golugwa
Hata
hivyo baada ya mkutano huo kuisha msafara huo utaelekea katika jimbo la
Monduli ambapo pia Mh.Lowassa atapata wasaa wa kuhutubia wananchi
katika jimbo hilo
Kwa upande wake Naibu katibu mkuu waTimu Lowassa for president Ndama Jeuri alisema wamejiandaa vizuri kumpokea na wataendelea kuhamasisha watu kumuunga mkono Lowassa katika harakati zake za Urais
Katika
msafara huo zaidi ya magari 75 yataanzia katika ofisi za chadema hadi
katika uwanja wa ndege wa kia huku vikundi mbalimbali vya ngoma
vikitumbuiza wakati wa mapokezi ya Lowassa.
No comments:
Post a Comment