Meneja
Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi Injini Philbert Rweyemamu
akizungumza na wafanyabiashara wa mkoa wa Shinyanga wakati wa kikao na
wafanyabiashara hao kilichokuwa na lengo la kuwapatia ufahamu juu ya
masuala ya manunuzi.
|
Bwana Nixson Mlumba – AfisaManunuzi wa ACACIA akifafanua jambo wakati wa Kikao hicho |
Baadhi ya Wafanyabiashara wakifuatilia kwa makini maelezo ya kutoka kwa Uongozi wa Kampuni ya Acacia wakati wa Kikao hicho. |
Mmoja wa wafanyabiashara wa mkoa wa Shinyanga akichangia mawazo wakati wa kikao. |
Wafanyabiasha wa mkoa wa Shinyanga wakiwa katika picha ya Pamoja na mkuu wa Mkoa na viongozi kutoka kampuni ya ACACIA. |
Na Mwandishi wetu.
WAFANYABIASHARA
wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kuchangamkia Fursa
mbalimbali za biashara zinazotolewa na Mgodi wa Dhahabu Buzwagi
unaomilikiwa na kampuni ya Acacia.
Meneja
mkuu wa Mgodi huo Injinia Filbert Rweyemamu ametoa wito huo katika
kikao baina ya uongozi wa Mgodi wa Buzwagi na wafanyabiashara wa Mkoa wa
Shinyanga ambapo alisema mgodi wa Migodi inayomilikiwa na Acacia
imejikuta ikishindwa kufanya kazi na wafanyabiashara wa mkoani humo
kutokana na wengi wao kushindwa kukidhi vigezo vya taratibu za manunuzi
kutokana na wengi wao kuwa na mitaji midogo hali ambayo imepelekea
huduma nyingi za manunuzi kuwategemea wafanyabiashara wakubwa kutoka
maeneo mengine.
“Nia
ya Kampuni ya ACACIA ni kufanya kazi na wafanyabiashara wanaotuzunguka
lakini kuna chanagamoto ya wengi wenu kushindwa kufikia vigezo vya
manunuzi ambavyo ACACIA imejiwekea, niwaase kupitia vikao hivi ambavyo
vimelenga kuwapatia uelewa mkajipange na ikiwezekana jiungeni katika
vikundi ambavyo vitakuwa na mitaji mikubwa itakayowawezesha kuwa na
uhakika wa kufanya kazi na migodi yetu” Alisema Injinia Rweyemamu.
Injinia
Rweyemamu ameongeza kuwa kwa sasa huduma nyingi Pamoja na bidhaa
vikiwemo vipuli vya magali na mitambo wamekuwa wakitegemea wasambazaji
wakubwa kutoka nje, huku akisisitiza kuwa kama wafanyabiashara wa mkoa
wa Shinyanga wangeungana na kuwa na biashara hizo Migodi yetu
isingelazimika kuagiza bidhaa hizo nje.
Kwaupande
wake mtaalamu wa masuala ya manunuzi ya ndani na Maendeleo ya biashara
wa ACACIA Bwana Nixson Mlumba akitoa taarifa za namna ambavyo
wafanyabiashara wa Shinyanga wamekuwa wakishiriki kufanya biashara na
ACACIA amesema takwini zinaonyesha ushiriki mdogo sana wa
wafanyabiashara wa mkoa huo huku wengi wao wakishindwa kufikia vigezo
vya manunuzi ya ACACIA kutokana na wengi wao kuendesha biashara kinyume
cha Sheria.
“Kama
alivyosema meneja wa mgodi wa Buzwagi, Fursa zipo cha msingi zingatie
sharia za nchi na jiunge kwa Pamoja ili muweze kuongeza mitaji ya
biashara zenu, Hatupendi kufanyabiashara na mtu ambaye baada ya kumpatia
tenda atashindwa kutuhudumia kwa mujibu wa Mahitaji yetu” alisema Nixon
Kwa
upande wake mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Josephina Matiro alisema kuwa
fursa hii ambayo inatolewa na kampuni ya ACACIA haina budi kuchangamkiwa
na wafanyabiashara wote wa kanda ya Ziwa kwani itasaidia katika
kuongeza pato lao Pamoja na pato la Taifa.
Nae
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ally Nassor Rufunga awali alisema kuwa mgodi
wa Buzwagi umekuwa kifua mbele katika suala la shughuli za maendeleo
ndani ya Mkoa huo huku ukishirikiana na wakandarasi wa ndani ambao
wameonyesha uwezo mkubwa katika kutekeleza miradi ya ujenzi wa madarasa
na zahanati.
Aidha
Mkuu huyo wa Mkoa amesema licha ya wakandarasi wa shughuli za ujenzi
kuonyesha uwezo mzuri katika utekelezaji wa miradi mbalimbali, bado
wafanya biashara wengine wameshindwa kuchangamkia fursa hizo
zinazotolewa na Mgodi, hali ambayo imepekea fursa hizo kutumiwa na
wafanyabiashara wa maeneo mengine ya nchi na wakati mwingine
wafanyabiashara wa nje ya nchi.
Mkutano
huo uliofanyika katika hotel ya Submarine wilayani Kahama ulilenga
kuwasaidia wafanyabiashara wa mkoa huo kupata ufahamu juu ya masuala
mbalimbali ya manunuzi katika kampuni hiyo.
No comments:
Post a Comment