MKURUGENZI
wa Huduma na Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ya Jamii
Tanzania, NHIF, Eugine Mikongoti, akiwasilisha mada juu ya mpango wa
uchangiaji binafsi, KIKOA, wakati wa warsha ya siku moja iliyoandaliwa
kwa pamoja kati ya NHIF, na Mtandao wa Bloggers Tanzania, TBN, na
kufanyika kwenye ukubmi wa Baraza la Maaskofu Tanzania, Kurasini jijini
Dar es Salaam, Agosti 13, 2015
NA K-VIS MEDIA
MFUKO
wa Taifa wa Bima ya Afya ya Jamii Nchini Tanzania, NHIF, umekutana na wanachama wa chama cha waandishi wa
habari wa mtandao (TBN), na kuwapa elimu juu ya mpango wa uchagiaji wa “KIKOA”,
ambao unahusu watu binafsi walio kwenye vikundi.
Akitoa
mada juu ya mpango huo, Mkurugenzi wa
Uendeshaji wa Mfuko huo anayesimamia mpango wa uchagiaji binafsi, (KIKOA), Eugine Mikongoti, amesema, mfuko wa bima ya
afya chini ya sheria ya kuanzishwa kwa mfuko huo, sheria namba 8 ya mwaka 1999,
ni kusimamia upatikanaji wa huduma za kimatibabu kwa wananchi kwa utaratibu wa
kuchagia kabla ya kuugua na kupata matibabu kupitia Hospitali za Serikali,
Madhehebu ya dini, zan Binafsi na Maduka ya Dawa ambayo yamesajiliwa.
Alisema,
mwanachama wa KIKOA atachangia shilingi
76, 800/- kwa mwaka na atapatiwa kadi ya matibabu ya NHIF ambayo ataitumia
kupata matibabu katika vituo zaidi ya 6,000 vilivyosajiliwa na NHIF nchi nzima.
Pia
alisema, Mwanachama wa KIKOA anayo fursa ya kuwaingiza mwenza wake na nafasi
nne kwa ajili ya watoto (miaka 18 hadi 21) kama bado wanasoma na wazazi wake na
wazazi wa mwenza wake, kwa utaratibu ule ule ya kuwalipia kila mmoja shilingi
76,800/- kwa mwaka kwa kila mmoja
Mgeni rasmi Mkurugenzi
wa Masoko na Utafiti wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii ya Tanzania, NHIF,
Rehami Athumani, akifungua warsha hiyo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa TBN, Khadija
Kalili
Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo, wakifuatilia kwa makini
Rehani Athumani
Bloggers kutoka Bagamoyo
Bloggers wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa
No comments:
Post a Comment