Waziri
wa Afya na Usitawi wa Jamii,Dk Seif Rashid akizungumza na waandishi wa
habari hawaponi pichani juu ya Kuepuka kusalimiana kwa kushikana mikono
Kunywa maji yaliyo safi na salama – yaliyochemshwa au kutiwa dawa
Hakikisha usafi wa mazingira yako wakati wote ikiwa ni pamoja na chooni
Kutokula matunda au kitu chochote bila kukisafisha kwa maji safi na
salama Kuhakikisha unatumia choo kwa ufasaha na wakati wote Kuwahi
mapema na toa taarifa kituo cha huduma ya afya kilicho karibu na wewe
endapo utapatwa na ugonjwa wa kuharisha au kutapika
Katibu
Mkuu wa Wizari wa Afya na Usitawi wa Jamii.Dk Donan Mmbando akizungumza
na waandishi wa habari hapo pichani juu ya Usafirishaji holela wa
wagonjwa wanaohisiwa kuwa na ugonjwa wa kipindupindu. Ni vyema kutoa
taarifa iwapo kuna abiria mwenye dalili za ugonjwa huu ili ushauri
uweze kutolewa wa namna ya kumsafirisha.
Mwakilishi
wa Shilika la Afya Duniani( WHO) Dk Rufaro Chatora akizungumza na
waandishi wa habari hapo pichani juu ya Kufungua kambi za wagonjwa wa
kipindupindu katika Manispaa zote tatu za Dar es Salaam ambapo kwa
Kinondoni kambi ipo Mburahati, Ilala, kambi ipo kituo cha Afya Buguruni
na Temeke katika Hospitali ya Temeke. Kwa Mkoa wa Morogoro kambi
zimefunguliwa Sabasaba na St Thomas.
Waandishi wakimsiliza kwa makini Waziri wa Afya na Usitawi wa Jamii,Dk Seif Rashid.
Picha na Emmanuel Massaka.
IDADI
YA WAGONJWA WALIYORIPOTIWA KUAMBUKIZWA NA UGONJWA WA KIPINDUPINDU AMBAO
UMELIKUMBA JIJI LA DAR ES SALAAM PAMOJA NA MKOA WA MOROGORO IMEFIKIA
WAGONJWA 262 NA VIFO 8.
Idadi
ya wagonjwa waliyoripotiwa kuambukizwa na Ugonjwa wa Kipindipindu ambao
umelikumba jiji la Dar es salaam pamoja na Mkoa wa Morogoro imefikia
wagonjwa 262,huku vifo hadi sasa toka ugonjwa huo ugundulike Agost 15
mwaka huu vikifikia nane.
Taarifa
hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Daktari Seif
Rashidi wakati akizungumza nawaandishib wa habari ikiwa lengo ni kutoa
taarifa juu ya Ugonjwa huo hatarI ambao umeibuka kwa kasi jijini Dar es
salaam pamoja na Mkoani Morogoro.
Aidha
alisema kuwa hadi sasa idadi ya wagonjwa katika jiji la Dar es salaam
walioambukizwa ni 230 na vifo saba,ambapo Manispaa ya Kinondoni ina
wagonjwa 186,Manispaa ya Ilala wagonjwa 22 na Temeke 22 nakwamba
wagonjwa waliyolazwa kwenye kambi za matibabu ni 71 ambazo ni
Mburahati wagonjwa 47,kambi ya Buguruni 15 huku kambi ya Temeke ni
wagonjwa 9.
Aliendelea
kufafanua kuwa wagonjwa wengi wamekuwa wakitoka katika maeneo
mabalimabali ambapo katika Manispaa ya Kinondoni ni maeneo
ya makumbusho,kimara,Tandale,Manzese,Saranga,Magomeni,Mwananyamala,kibamba,kigogo,Goba,Burahati,Kinondoni
na Kijitonyama.
Manispaa
ya Ilala ni Buguruni,Majohe,Chanika,Ilala sharif shambana Tabata huku
Katika Manispaa ya Temeke wagonjwa wengi ni kutoaka katika maeneo ya kwa
Azizi Ally,Keko na Yombo Vituka.
Alisema
Mkoani Morogoro wagonjwa waliyoripotiwa Agost 24 mwaka huu ni 32 na
kifo kimoja ambapo pia wagonjwa wapatao 15 wamehifadhiwa kwenye kambi ya
Matibabu ya Sabasaba Mkoani humo.
Waziri
huyo wa Afya na Ustawi wa Jamii ametoa tahadhari kwa jamii kuchukua
tahdhari pamoja na kuzingatia kanuni za afya ikiwemo,kuzingatia usafi wa
mazingira,kuchemsha maji ya kunywa,kunawa mikono kwa sabuni kabla na
baada ya kula chakula,kuepuka kusalimiana kwa kushikana
mikoni,kuzingatia usafi wa vyoo pamoja na kula vyakula ambavyo
vimeandaliwa kwenye mazingira safi na salama.
Naye
mwakilishi mkazi wa shirika la Afya Duniani Daktari Rufaro Chatora
amesema kuwa lazima kuwepo na hatua za haraka za kusafisha visima kwa
kemikali maalumu na kuhamasisha jamii kutumia vidonge vya kusafisha maji
au kuchemsha maji.
Aidha
aliongeza kuwa mamlaka husika zichukue hatua za haraka na madhubuti
kushugulikia upatikanaji wa maji safi na salama pamoja na usafi wa
mazigira katika maeneo husika nakwamba suala hilo siyo la Wizara ya Afya
pekee bali ni ushirikiano na Wadau wengine ikiwemo sekta ya
Uchukuzi,Mawasiliano,Maji na Elimu.
No comments:
Post a Comment