Utalii Wetu : Matumizi Mabaya ya Ardhi Tishio kwa Uhifadhi - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

Thursday, 2 July 2015

Utalii Wetu : Matumizi Mabaya ya Ardhi Tishio kwa Uhifadhi

 Waziri wa Utalii na Maliasili Lazaro Nyalandu akihutubia viongozi wa Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori (WMAs) katika mkutano  kati ya Wizara na jumuiya hizo ,ulikua ukijadili uhifadhi wa mazingira na kuheshimu matumizi sahihi ya ardhi ili kulinda uhifadhi.
 Waziri wa Utalii na Maliasili Lazaro Nyalandu akihutubia viongozi wa Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori (WMAs) katika mkutano  kati ya Wizara na jumuiya hizo ,ulikua ukijadili uhifadhi wa mazingira na kuheshimu matumizi sahihi ya ardhi ili kulinda uhifadhi.Picha naFerdinand Shayo

Na Ferdinand  Shayo wa Wazalendo 25 Blog ,Arusha.

Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu amesema kuwa matumizi mabaya ya ardhi yasiyozingatia mpango bora wa matumizi ya ardhi  yamekua tishio kwa  maeneo uhifadhi hivyo kupelekea uvamizi wa maeneo hayo na kutumiwa kwa shughuli za ufugaji na kilimo kinyume cha utaratibu.

Nyalandu amesema hayo jana wakati akihutubia mkutano wa kati ya  Wizara na Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori (WMAs) uliofanyika jijini hapa,amesema kuwa ili kuwa na uhifadhi endelevu  utakaorithiwa na vizazi vijavyo  mpango wa matumizi bora ya ardhi hauna budi kuzingatiwa.

Waziri huyo amesema kuwa ujenzi wa miji katika maeneo ya uhifadhi ikiwemo Hoteli na kumbi za starehe unaathiri shughuli za uhifadhi hivyo amewataka wadau wa utalii kugawanya uwekekezaji  kwa kuwekeza nje ya hifadhi.

“Mtu anayefikiria kujenga miji ndani ya hifadhi anakua hajapiga hesabu vizuri  lazima tutawanye  uwekezaji hoteli zijengwe nje ya hifadhi” Alisema Nyalandu

Alisema kuwa kwa sasa Tanzania ina jumla ya Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori (WMAs) 21 ambazo ni kilometa za mraba 36237.7 na jumuiya nyingine  17 ziko katika hatua mbalimbali za uanzishwaji,amezitaka jumuiya hizo kuhakikisha kuwa zinawashirikisha wananchi katika kuhifadhi na kunufaika kwa mujibu wa sera ya wanayama pori ya mwaka 1998.

Mwenyekiti wa Chama cha Waongoza watalii nchini Wilbard  Chambulo alisema kuwa ili uhifadhi uweze kufanikiwa lazima wanakijiji wawe na hati miliki za maliasili ili waweze kuzitunza vyema.

Chambulo anaeleza kuwa ushirikishwaji wa wananchi katika uhifadhi ni nguzo muhimu sana kwa uhifadhi  itakayosaidia kuwa na utalii endelevu kwa vizazi na vizazi.

No comments:

Post a Comment