Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Global Peace Foundation (GPF), Arnold Kashembe
(katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es
Salaam leo, kuhusu kongamano kubwa la vijana litakalofanyika Zanzibar
kwa kipindi cha mwezi mzima kuanzia Julai 12 mwaka huu. Kongamano hilo
litahudhuriwa na marais wastafu na viongozi maarufu. Kulia ni Mwakilishi
Mkazi wa GPF nchini, Martha Nghambi na Mratibu wa kongamano hilo, Antu
Mandosa
Mwakilishi Mkazi wa GPF nchini, Martha Nghambi (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Balozi wa Amani, Risasi Mwaulanga na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Global Peace Foundation (GPF), Arnold Kashembe.
Balozi wa Amani, Risasi Mwaulanga akizungumza katika mkutano huo.
Mratibu wa kongamano hilo, Antu Mandosa akizungumza kuhusu kongamano hilo.
Mkutano ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale
SHIRIKA
la Global Peace Foundation limewataka Watanzania kudumisha amani
iliyopo ili nchi yetu isije ikakumbwa na machafuko kama nchi za jirani.
Akizungumza
leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Global Peace Foundation na
Mshauri wa Amani Afrika , Arnold Kashembe alisema Shirika hilo limeandaa
mkutano wa kujadili mkakati wa kudumisha amani utakao jumuisha nchi za
Afrika Mashariki (EAC).
"Shirika
la GPF limeandaa mkutano wa kujadili mkakati wa kudumisha amani utakao
jumuisha nchi za Afrika Mashariki (EAC) ambao utafanyika Zanzibar
kuanzia Julai 21- 24," alisema Kashembe.
Kashembe
alisema mkutano huo wa kipekee utawakutanisha maraisi wastaafu nane
akiwemo Keneth Kaunda na Amani Karume, viongozi wa dini, wafanyabiashara
na viongozi wengine kutoka nchi za Afrika Mashariki na nchi jirani.
Aidha
Global Peace Leadership Conference (GPLC) 2015 itatoa mafunzo na nyenzo
ili kuhimiza ushirikiano katika ukanda wa Afrika Mashariki na kujaribu
kupunguza tofauti na matatizo yanayowakumba.
Mada
nyingine ni kuwapongeza vijana 400 kutoka Afrika Mashariki
wanaotarajiwa kushiriki kuongeza nguvu katika mbinu za ujasiriamali na
kuwa mfano wa wanafunzi wa wengine huko watokapo.
Kujenga
mikakati imara ya kudumisha ukaribu na kusaidiana mbinu za kupambana na
umaskini, tatizo la ajira, HIV, Malaria na kuwezesha na kuzindua
misheni Maendeleo ya Afrika kama lengo kuu na kiini cha mabadiliko
kupitia Amani, Uongozi bora, na Uimara wa maendeleo kiuchumi.(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
No comments:
Post a Comment