
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe akitoa hotuba fupi ya
uzinduzi wa Magereza "Duty Free Shop" Gereza Kuu Lilungu, Mkoani Mtwara Julai 5, 2015 katika Viwanja vya Lilungu, Mkoani Mtwara.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe(kulia) akifurahia jambo
wakati wakiwa kwenye jiwe la Msingi mara tu baada ya kuzindua rasmi
duka hilo lenye bidhaa zisizo na tozo la Kodi(wa pili kushoto) ni
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir
Minja(kushoto) ni Mkurugenzi wa Transit Military Shop, Bw. Alfazar
Meghji. Uzinduzi huo umefanyika Julai 5, 2015 katika Viwanja vya Gereza
Kuu Lilungu, Mkoani Mtwara.
Bidhaa
mbalimbali zinazopatikana katika Magereza "Duty Free Shop" ya Gereza
Kuu Lilungu, Mkoani Mtwara kama inavyoonekana katika picha. Duka hilo
limezinduliwa rasmi na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias
Chikawe(hayupo pichani).
Muonekano wa nje wa Magereza "Duty Free shop" ya Gereza Kuu Lilungu, Mkoani Mtwara kabla ya kuzinduliwa rasmi leo Julai 5, 2015.
Maafisa
Waandamizi wa Jeshi la Magereeza kutoka Mikoa ya Lindi na Mtwara
wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa
Magereza "Duty Free Shop" Gereza Kuu Lilungu, Mkoani Mtwara.
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, John Casmir Minja(kulia) akiteta jambo na
Mkuu wa Wilaya ya Newala, Mhe. Christopher Magala(kushoto) kwenye hafla
ya ufunguzi rasmi wa Magereza "Duty Free Shop Gereza Kuu Lilungu, Mkoani
Mtwara.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe(katikati) akiwa katika
picha ya pamoja na Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza kutoka Mikoa
ya Lindi na Mtwara kwenye uzinduzi wa Magereza "Duty Free Shop" Gereza
Kuu Lilungu, Mkoani Mtwara(wa tatu kushoto) ni Kamishna Jenerali wa
Magereza, John Casmir Minja(wa tano kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani
Mtwara, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Mussa Kaswaka(wa pili kushoto)
Mkuu wa Wilaya ya Newala, Mhe. Christopher Magala(wa kwanza kushoto) ni
Mkurugenzi wa Transit Military Shop, Alfazar Meghji.
Na, Lucas Mboje, Mtwara
Maafisa
na Askari wa Jeshi la Magereza nchini wametakiwa kutumia fursa ya
maduka yenye bidhaa nafuu "Duty Free Shop" zilizofunguliwa katika
Magereza mbalimbali ili kupata vifaa vya ujenzi na kujenga makazi
yaliyobora na ya kudumu kabla ya kustaafu Utumishi wao Jeshini.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe
alipokuwa akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Magereza "Duty Free
Shop" ya Gereza Kuu Lilungu, Mkoani Mtwara.
Amesema
kuwa Maafisa na Askari wakitumia vizuri fursa ya maduka haya kwa
kununua bidhaa za vifaa vya ujenzi itasaidia kukwepa aibu inayowapata
baadhi ya Maafisa na Askari baada ya kustaafu hivyo kukosa nyumba za
kuishi wakitegemea kujenga kwa kutumia Mafao baada ya kustaafu.
"Serikali
iliidhinisha utaratibu wa Maafisa na askari wa Majeshi ya Ulinzi na
Usalama kusogezewa Huduma hizo za bidhaa muhimu katika maeneo yao kwa
gharama nafuu kwa lengo la kuwapunguzia makali ya maisha". Alisema
Waziri Chikawe.
Kwa
upande wake Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja amesema
kuwa Jeshi la Magereza limejipanga kuhakikisha kuwa linasambaza huduma
hizo nchi nzima kwa ajili ya kutoa huduma kwa Maafisa na askari nchini.
Hadi
sasa Jeshi hilo limekwisha kuzindua "Duty Free Shops" Nane katika Mikoa
ifuatayo Dar es Salaam - Ukonga na Keko, Mwanza - Butimba, Tabora -
Uyui, Kingolwira - Morogoro, Mbeya - Ruanda, Dodoma - Isanga na Mtwara -
Lilungu.
No comments:
Post a Comment