Shirikisho
la Mpira wa Miguu nchini (TFF) leo limefungua kozi ya makocha wa mpira
wa miguu kwa watoto na vijana kwa nchi nzima kwa lengo la kuhakikisha
vijana wengi wanapata nafasi ya kufundishwa mpira na kuucheza mpira
kuanzia katika umri mdogo.
Akifungua
kozi hiyo, Katibu Mkuu wa TFF Mwesigwa Selestine amesema ili nchi/Taifa
lifanikiwe katika soka ni lazima kuwekeza katika mpira wa watoto na
vijana ambao makocha hao ni sehemu ya uwekezaji huo.
“Tumekua
na mashindano ya Taifa U-13, kikosi cha timu ya Taifa ya U-15 ambayo
inashirikisha vijana wadogo, vijana hao wanapaswa kupata malezi na
mafunzo yenu waalimu ili wafikiapo kuchezea timu za Taifa wawe wamekua
kwenye msingi bora wa kuujua mpira wa miguu” alisema Mwesigwa.
Naye
mkufunzi wa FIFA wa kozi hiyo ya makocha kutoka nchini Ujerumani, Eric
Muller amesema hata ujerumani imefanikiwa baada ya kuwekeza katika soka
la vijana, mwaka 2000 kwenye fainali za Euro nchi yao ilishika nafasi ya
mwisho katika msimamo kundi lao kwa kupata poniti moja, lakini
uwekezaji walioufanya kwenye soka la watoto na vijana umewapelekea
kutwaa Ubingwa wa Dunia mwaka 2014.
Washiriki
wa kozi hiyo ni makocha wa timu za vijana za mikoa yoye Tanzania, ambao
watashirki na timu zao za mikoa katika michuano ya Copa Coca Cola mwaka
huu.
Kozi
hiyo ya makocha wa timu za watoto/vijana inayoendeshwa na wakufunzi wa
FIFA, Ulric Mathews kutoka shelisheli na Eric Muller kutoka nchini
Ujerumani itamalizika jumatatu tarehe 29 Juni, 2015.
STARS YAANZA MAZOEZI
Kikosi
cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kinachodhaminiwa na bia ya
Kilimanjaro Premium Lager kimeanza mazoezi leo asubuhi katika uwanja wa
Boko Veterani kujiandaa na mchezo wa marudaino kuwania kufuzu kwa CHAN
dhidi ya uganda mwishoni mwa wiki ijayo.
Stars
inayonolewa na makocha wazawa, Charles Mkwasa na msaidizi wake Hemded
Morocco, itakua ikifanya mazoezi asubuhi na jioni katika uwanja huo wa
Boko Veterani, huku timu ikiweka kambi yake katika hoteli ya Kiromo
mjini Bagamoyo.
Wachezaji
wote walioitwa wameripoti kambini tangu jana na leo wamefanya mazoezi
asubuhi isipokua Aggrey Morris ambaye ni majeruhi nafasi yake
imekuchukuliwa na Vicent Andrew (Mtibwa Sugar) na Jonas Mkude
aliyekwenda kufanya majaribio Afrika Kusini nafasi yake ikizibwa na
Mudathir Yahya (Azam FC).
TFF YAVIAGIZA VYAMA VYA MKOA KUWA NA VITUO VYA MPIRA WA MIGUU
Kufuatia
pendekezo la sekretariet ya TFF ambalo baadae lilipitishwa na Mkutano
Mkuu wa TFF kila mkoa unatakiwa kuwa na kituo chake cha kulea na kukuza
vipaji vya mpira wa vijana umri kuanzia miaka 8-17.
Kwa
mikoa ambayo tayari ina kituo ambacho inakiendesha yenyewe TFF inaonba
ipatiwe taarifa hiyo ikiwa ni pamoja na kufahamishwa jina la kituo, jina
la mwalimu na sifa zake na utaratibu wa mafunzo.
Kwa
mikoa ambayo haina kituo TFF inagiza mikoa hiyo kuingia ubia na kituo
kimoja ambacho tayari kina program ya kukuza na kuendeleza vipaji ili
kijulikane kuwa ni kituo maalum cha mkoa husika.
Katika
hilo TFF inaagiza kamati ya utendaji ya mkoa husika iandae muhtasari wa
kikao cha utendaji cha chama cha mkoa wa kupitisha maamuzi hayo, MoU
(makubaliano rasmi) yasainiwe kati ya chama cha mkoa na kituo husika na
hati hiyo nakala yake iletwe TFF.
MoU
hiyo ionyeshe majukumu ya chama cha mpira cha mkoa kama kutoa vifaa,
kutoa mwalimu, usimamizi nk na pia kuonyesha majukumu ya mwenye kituo
kama kutoa uwanja,ulinzi nk. MoU itaonyesha pia nani atafaidika na
vipaji vitakavyoibuliwa kati ya mzazi,kituo na chama cha mkoa.
TFF
itaandaa MoU ya mfano kwa ajili ya vyama vyote vya mikoa na ingependa
kufikia tarehe 31/Desemba/2015 kila mkoa uwe umetekeleza jambo hilo.
SITA ZAPANDA DARAJA KUCHEZA SDL
Abajalo
FC ya Tabora, Alliance FC (Mwanza), Changanyikeni Rangers FC (Dar es
Salaam), Coca-Cola Kwanza FC (Mbeya), Madini SC (Arusha), na Sabasaba
United FC (Morogoro) ndizo timu zilizopanda kucheza Ligi Daraja la Pili
(SDL) msimu wa 2015/2016.
Timu
hizo zimepanda daraja baada ya kufanya vizuri kwenye michuano ya Ligi ya
Mabingwa wa Mikoa (RCL) iliyomalizika hivi karibuni kwenye vituo vya
Lindi, Manyara na Rukwa na kushirikisha jumla ya timu 27.
SDL
inayoshirikisha timu 24 zilizogawanywa katika makundi manne inatarajia
kuanza kutimua vumbi Oktoba 17 mwaka huu. Ligi hiyo itachezwa kwa mtindo
wa nyumbani na ugenini, na timu itakayoongoza kundi ndiyo itakayopanda
daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kwa msimu wa 2016/2017.
Kundi A
lina timu za Abajalo FC (Tabora), Green Warriors (Dar es Salaam),
Milambo FC (Tabora), Mvuvumwa FC (Kigoma), Singida United (Singida) na
Transit Camp (Dar es Salaam) wakati Kundi B ni AFC (Arusha), Alliance FC
(Mwanza), Bulyanhulu FC (Shinyanga), JKT Rwamkoma FC (Mara), Madini SC
(Arusha) na Pamba SC (Mwanza).
Timu
za kundi C ni Abajalo FC (Dar es Salaam), Changanyikeni Rangers FC (Dar
es Salaam), Cosmopolitan (Dar es Salaam), Kariakoo FC (Lindi),
Mshikamano FC (Dar es Salaam) na Villa Squad (Dar es Salaam).
African
Wanderers ya Iringa, Coca-Cola Kwanza FC (Mbeya), Mkamba Rangers
(Morogoro), Sabasaba United FC (Morogoro), Town Small Boys (Ruvuma) na
Wenda FC ya Mbeya ndizo zinazounda kundi D.
Dirisha la usajili wa wachezaji limeshafunguliwa tangu Juni 15 mwaka huu, na litafungwa Agosti 6 mwaka huu.
VILBU VPL VYATAKIWA KUWASLISHA MAJINA YA MAKOCHA WA MAKIPA
Shirikisho
la Mpira wa Mpira wa Miguu nchini (TFF) linaviomba vilabu vyote
vinavyoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom kuwasilisha jina la kocha wa
magolikipa kufikia jumatatu ya tarehe 29 Juni, 2015 katika ofisi za TFF.
TFF
imeandaa kozi ya magolikipa hivyo inahitaji kupata jina la kila kocha wa
magolikipa ili kuweza kushiriki kwenye kozi hiyo itakayoanza tarehe 13 -
17 Julai, 2015 jijini Dar es salaam.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment