Mwanafunzi
wa Shule ya Kimataifa ya Fedha mwaka 11, Khalfan Kikwete (kulia) ambaye
alishinda medali ya dhahabu pamoja na mwenzake Seif Yahya Mhata
wakizungumza na waandishi wa habari.Mwanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Fedha mwaka 11, Seif Yahya Mhata (kulia) wakizungumza na mmoja wa waandishi wa habari Mwanafunzi Veronica Samuel Ndomba akielezea mchanganuo wake ulioshinda katika mashindano ya Genius Olympiad kwa wanahabari leo Wanafunzi
Goodluck Komba (kulia) na Sajjad El-Amin walioshinda na andiko la mradi
wa kutengeneza mkaa kwa kutumia makaratasi taka ambao ulishika nafasi
ya tatu katika mashindano ya Genius Olympiad wakizungumza na waandishi
wa habari.Mwanafunzi
Veronica Samuel Ndomba (kushoto) akifanyiwa mahojiano na mmoja wa
waandishi wa habari. Mwanafunzi
wa Shule za Fedha, Prince Mwemezi Muzamil Katunzi akielezea picha yake
ilioshinda katika mashindano ya Genius Olympiad kwa wanahabari
leo. Mwanafunzi
Veronica Samuel Ndomba akielezea (kulia) katika picha na abendera ya
nchi yake mara baada ya ushindi katika mashindano ya Genius Olympiad
hivi karibuni. Picha ya Mwanafunzi Prince Mwemezi Muzamil Katunzi aliyoipiga na kushinda katika mashindano ya Genius Olympiad.Kutoka
kulia ni mwalimu Metin Er wa Masomo ya Biashara, Fedha International
School na Meneja Uhusiano wa Ishik Medical & Education Foundation.
WANAFUNZI sita
wa Shule za Feza Tanzania wameshinda mashindano ya taaluma kimataifa
'Genius Olympiad' yaliyoshirikisha nchi mbalimbali katika vipengele
tofauti na kuzawadiwa medali za dhahabu, shaba pamoja na zawadi
mbalimbali. Wakizungumza na waandishi wa habari leo katika moja ya shule
za Feza iliyopo Kawe jijini Dar es Salaam Wanafunzi hao kuelezea
ushindi wao wameshauri wanafunzi wengine kupenda kushiriki katika
mashindano anuai ya taaluma kwani ni njia ya kuwaongezea maarifa
shuleni.
Wanafunzi
walioshinda na kupewa medali ni pamoja na Seif Yahya Mhata, Khalfan
Jakaya Kikwete, Prince Mwemezi Muzamil Katunzi, Goodluck Komba, Sajjad
El-Amin na Veronica Samuel Ndomba. Akizungumza mwanafunzi wa Shule ya
Kimataifa ya Fedha mwaka 11, Khalfan Kikwete ambaye alishinda medali ya
dhahabu pamoja na mwenzake Seif Yahya Mhata alisema wazo lao
lililoshinda lilikuwa ni la kutengeneza mfumo wa kuhifadhi mawasiliano
ya mtu kupitia simu za mkononi (A virtual business cards & New
generation business social media, Vcardin) andiko ambalo wameliwasilisha
na kushinda wote medali za dhahabu.
Alisema
utafiti unaonesha njia ya kutengeneza card za mawasiliano kwa kutumia
karatasi kwa wafanyabiashara na wafanyakazi zimekuwa zikileta madhara
kimazingira pamoja na kupotea baada ya muda, hivyo wao kubuni mfumo
(App) wa kuhifadhi mawasiliano hayo upitia simu za mkononi (iphone)
ambao ni bora na unatunza kwa uhakia.Wanafunzi
wa Shule za Feza Tanzania walioshinda mashindano ya taaluma kimataifa
ya 'Genius Olympiad' katika picha ya pamoja.Wanafunzi
wa Shule za Feza Tanzania walioshinda mashindano ya taaluma kimataifa
ya 'Genius Olympiad' katika picha ya pamoja na baadhi ya walimu wao.Wanafunzi Goodluck Komba na Sajjad El-Amin.
Mwanafunzi
Yahya Mhata ambaye kwa pamoja wamebuni mfumo huo, ameuelezea kuwa ni
mzuri na rafiki wa mazingira huku ukiweza kuhifadhi kumbukumbu za
mawasiliano kwa uhakika tofauti na ule wa kadi za makaratasi ambao wengi
hupoteza kadi hizo na kujikuta wakipoteza mawasiliano muhimu.
Wanafunzi
wengine wa Shule za Fedha ambao ni Prince Mwemezi Muzamil Katunzi,
Goodluck Komba, Sajjad El-Amin na Veronica Samuel Ndomba ambao kila
mmoja ameshinda medali za fedha katika makundi ya ushindani tofauti
chini ya usimamizi wa mwalimu Metin Er wa Masomo ya Biashara, Fedha
International School walieleza kunufaika na mashindano kitaaluma na
upeo.
Mwanafunzi
Mwemezi Muzamil Katunzi, ambaye aliwasilisha picha yenye ujumbe wa
mazingira na kushinda alisema picha hiyo aliipiga eneo la viwanja vya
Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam ikielezea namna binadamu
wanaathiri mazingira kwa kuchoma moto hovyo na kuleta matatizo mengine
duniani. Kwa upande wao wanafunzi Goodluck Komba na Sajjad El-Amin
waliwasilisha andiko la mradi wa kutengeneza mkaa kwa kutumia makaratasi
taka ambao ulishika nafasi ya tatu katika mashindano ya Genius Olympiad
yaliyofanyika jijini New York.
Mwanafunzi
Komba alisema mradi wao ni rafiki wa mazingira na ukitumika utaokoa
sehemu kubwa ya uharibifu wa mazingira. Kwa upande wake msichana pekee
aliyeshinda katika mashindano hayo, Veronica Samuel Ndomba alisema
andiko lake lilishinda kwenye kipengele cha 'Mazingira Yetu' na
aliandika kuonesha namna elimu ya mazingira inaweza kutolewa na kulinda
uharibifu mkubwa wa mazingira unaofanywa katika shughuli mbalimbali za
binadamu.
Naye
msimamizi wa wanafunzi hao, mwalimu Metin Er alisema kundi hilo la
wanafunzi mbali na kujijenga kimaarifa kwa wanafunzi hao wameiletea sifa
Tanzania kwani kwani mashindano hayo ya kitaaluma yalishirikisha nchi
mbalimbali zikiwemo USA, Romania, Nigeria, Tunisia, Holland,
Turkmenistan, Kazakhstan and Russia. Shule za Fedha International School
zimekuwa zikifanya vizuri kitaaluma kitaifa na kimataifa jambo
linaloendeleza umaarufu wa shule hizo kila uchao. *Imeandaliwa na
www.thehabari.com
No comments:
Post a Comment